Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,698
- 4,693
Ukisoma meseji za hapa JF ndo utagundua ujuha tulionao. Kuna watu wanadhani iko siku Dar itakuwa kama London au New York. Ukiwauliza wansema tuwe kama nchi za wenzetu. Halafu wanasema eti Dar ni jiji kubwa lakini, hawajiulizi ni kwa nini iwe hivyo. Hawajui matatizo ya kuifanya Dar iwe hivyo. Hawajui kwamba hakuna siku Dar itakuwa nzuri maana kila maskini anakimbilia huko akiamini atafaidika. Maji hakuna, Nyumba ni vibanda, barabara hoi, hospitali uchafu tu!Hatimaye leo humu JF nimekutana na mtu mwenye mtazamo kama wangu. Nadharau sana kuona jiji la Dar lina wakazi almost milioni 5 wakati linalofuatia, hata robo ya watu halifiki. Ukihesabu skyscrapers za Dar, ujaribu kulinganisha na Majiji yanayofuatia kwa skyscrapers - Arusha na Mwanza, utagundua namna tulivyo bado vilaza kama Nchi.
Wazungu hasa wa Uingereza na Ufaransa, wanajilaumu sana kwa namna walivyoruhusu London na Paris kudominate kila kitu katika maisha ya mataifa hayo na kuyafanya maeneo mengine kuwa marginalized.
Angalao by 1960s - 1990s London ilikuwa inapungua kutokana na uwekezaji kusambaa maeneo yote ya Nchi. Leo hii, watu wabasifia Ujerumani kwa kuwa na balance katika maendeleo bila ya kuwa na dominant metropolitan city - Berlin (East), Hamburg (North), Munich (south), Frankfurt (central) na Cologne (west): yote hiyo inazidiana katika sifa tofauti tofauti.
Ndiyo umuhimu wa Sera ya Majimbo ya CHADEMA huwa naiona inaleta maana.
Ndiyo maana naunga mkono kwa zaidi ya asilimia 100% HQ kwenda Dom angalao kubalance maendeleo kwa maeneo ya mbali.
Ajabu ni kuwa, Kanda ya Ziwa yenye watu zaidi milioni 16, haina Chuo Kikuu cha Umma, kweli?
Nilishangaa sana Watanzania wenzangu wanaodai kuumia na wingi wa abiria kwenye kivuko cha MV Nyerere. Waambieni waende Ukerewe na Uzinza (Maisome, Kome) wataelewa hasara ya kukalia kujenga eneo moja na kusahau mengine - wakazi wa Visiwa hivyo wanezoea shida hizo na wanaona kawaida. Kanda ya Ziwa wanashukuru sana anachofanya Magufuli hasa kutangaza kujenga meli mpya ya kwenda Bukoba na pia kivuko kingine cha Ukara.
Umetoa mfano mzuri sana!! Anayeishi Berlin, Ujerumani anaweza kutofika Frankfurt kwa miaka 20! Hana sababu maana kila kitu kipo anapoishi. Leo hii TZ hii kufika Dar au kuishi Dar eti ni sifa. Hata kama anakesha kifua wazi kwa kukosa hewa. Serikali lazima iwe makini. Serikali huendeshwa na watu wachache sana lakini wawe ni wenye akili na maono muhimu sana. Siyo hawa wachangiaji wanaojiandikia kwa hisia za mitandaoni na kuona filamu za Hollywood. Bado tunahangaika kupanua barabara wakati ulaya wanapunguza barabara na kuboresha usafiri wa umma! Halafu tunasema jiji linapendeza.
Wale mbumbumbu nawaomba wafike Lagos, waone flyover kwa wingi halafu waseme kama hizo zimeondoa vurugu za usafiri.