Serikali, Maendeleo siyo kuipamba Dar es Salaam kwa gharama ya nchi nzima

Inawezekana wewe ni Muha, na unapenda tu kubisha, ngoja nikuache kwanza.

Kwa akili yako unadhani bajeti ilipangwa tu na barabara ya lami inatokea hapo hapo?

Unanishangaza unaposema miezi miwili umepita hapo hapo Koga unakwenda Tabora, na wakati huo huo unasema Koga haipitiki watu wanapitia Uvinza?

Daraja la mto Koga limesimama si Kwa maana halipitiki, limesimama Kwa maana ya nguzo za daraja jipya na la kisasa zimesimama na zege Limwagwe kama sehemu ya ujenzi wa barabara ya lami, toka Sikonge, Ipole, Koga, Utende hadi Mpanda magreda yapo yanajenga barabara, sasa ulitaka lami imwagwe kwenye majani na miti ya Rukwa rwafi?

Ndio, narudia kusema kwamba miradi ya barabara inayoendela kuzinduliwa - huko Mara, Kasulu, Kigwa - Tabora, Itigi - Chaya, Dodoma - Kondoa - Babati, Iringa - Dodoma, etc zilikuwa ni projects za awamu ya 4, na hii barabara ya Pangale - Mpanda, na Kimara - Kibaha, ndio barabara za kwanza za lami kujengwa katika awamu hii ya 5 (kama unabisha weka ushahidi).

Mwisho, nakushauri uwe unapenda kwenda kwenu kila mara, habari za kujificha miji mingine na kuongea vitu usivyovijua utakuwa unapotosha, kwa taarifa yako Mpanda ya sasa sio ya miaka ile ulivyoicha.
yawezekana mimi ni muha ila ww ni muhutu maana majibu yako sijui unayatoa wapi. nimekwambia ulitegemea daraja la koga lisijengwe ikiwa lililokuwepo lilimezwa na maji hadi kuwalazimisha kutumia barabara ya uvinza (kipindi hicho) mkuu uelewa umekupitiliza hebu soma kwa vituo nayo andika alafu soma majibu yako
 
Acha uchochezi. Juzi juzi Babati wamekamilishiwa bara bara ya lami inayowaunganisha na Dodima, zaidi ya bilioni mia mbili zimetumika. Hapo hapo pia ujenzi wa hospitali ya mkoa Babati unapamba moto.
Mbeya wanajengewa upya bara bara inayowaunganisha na Iringa, hizo ni zaidi ya bilioni miambili.
Iringa pia wamejengewa bara bara inayowaunganisha na Dodoma, zaidi ya bilioni mia mbili zimelala pale. Bara bara ya kwenda Tabora kama km 70 imekamilika kwa kiwango cha lami hizo ni bilion miia.
Bara bara ya kutoka Tunduma kwenda Sumbawanga imejengwa kwa kiwango cha lami, nasikia japo sijafika huko. Bara bara za kutoka Tabora kwenda Kigoma ujenzi unaendelea. Orodha ni ndefu inayopingana na nadharia yako kuwa Dar inapendelewa.
Umesahau na stand kuu kila mkoa, msamvu...n the list goes on!
 
Katika utawala uliopita tulishuhudia miradi mikubwa ikipangwa kutekelezwa jijini Dar na Pwani. Naikumbuka miradi ya Mloganzila, bandari ya Bagamoyo, by-pass ya daraja la salander, BRT, nk. Hii ni miradi mikubwa sana kwa umaskini wetu. Miradi hiyo ilikuwa mikopo ambayo inalipwa na wananchi wa nchi nzima. Naona tena kuna muendelezo wa miradi mikubwa ndani ya jiji letu bila kujali shida zilizoko mikoani. Rais ametoa tena ahadi ya ujenzi wa flyover zingine ndani ya jiji la Dar es salaam.

Sababu ya maamuzi kama haya haieleweki lakini huenda ni kwa sababu watoa maamuzi wana makazi jijini Dar na wanajisikia kupamba makazi yao. Mikoa ya kati yaani Dodoma, singida, Tabora hadi shinyanga haina hospitali hata moja ya rufaa. Je, kwa nini Muloganzila haikusogezwa mikoa hiyo? Tukumbuke mikoa ya kusini pia haina hospitali ya maana. Ile ya Mbeya ni alama ya malengo na wengi wanajikuta wakielekea hospitali ya wamisionari, Peramiho. Kuna kundi linasifia jiji la Dar na kusema ni kitovu cha biashara. Huo si ukweli. Dar ni njia ya biashara. Mapato yetu makubwa ni Utalii na madini. Utalii uko Serengeti na Kilimanjaro, madini yako kanda ya ziwa. Kwa nini tuendelee kutumia pesa nyingi kiasi hicho kwa hisia ya jiji tu, bila sababu ya maana?

Najaribu kujiuliza, MV Nyerere imepoteza maisha ya watu kwa umaskini wao. Je, leo hii rais hawezi kutangaza maamuzi magumu na kuhamisha hizo pesa za flyover mpya za Dar pamoja na daraja la salander akijumulisha na pesa ya kivuko kipya kilichoahidiwa ili kuwajengea wana Ukara daraja refu kwa safari ya kisiwa chao? Je hatuwezi kuunganisha visiwa vya Jamuhuri hii kwa madaraja badala ya flyover mpya?

Flyover ni nzuri lakini tuwe na kiasi. Tugawane maendeleo badala ya kupamba jiji moja ndani ya nchi kubwa kama hii. Maamuzi mabovu kama haya husababisha ukuaji wa jiji moja na kuongeza wahamiaji kutoka mikoani kila siku. Mifano ya maamuzi kama hayo ziko ktk nchi zetu za kimaskini: Kongo DRC, Afrika ya kati, nk. Huko kila mtu anataka akaishi mji mkuu wa nchi maana hakuna mji mwingine wa maana!

Nchi haiendelei kwa kuipamba Dar. Tunahitaji maji safi, shule za kiwango, hospitali na barabara kwa nchi nzima.
hawaipambi dar wanafanya miradi ya lazima kwa dar es salaam, hayo yoote unayotaja ni mambo ya lazima kwa dar ilipofikia
 
Nimekuacha jinsi ulivyo, ila jitahidi uwe unaenda kwenu mara moja moja.

Mpanda na Katavi ya miaka miwili iliyopita si ya leo, there is tremendous development.

And Kwa hakika haitawezekana kujenga flyover Mpanda au Katavi yoote kabla hata ya Tabora.
yawezekana mimi ni muha ila ww ni muhutu maana majibu yako sijui unayatoa wapi. nimekwambia ulitegemea daraja la koga lisijengwe ikiwa lililokuwepo lilimezwa na maji hadi kuwalazimisha kutumia barabara ya uvinza (kipindi hicho) mkuu uelewa umekupitiliza hebu soma kwa vituo nayo andika alafu soma majibu yako
 
Nimekuacha jinsi ulivyo, ila jitahidi uwe unaenda kwenu mara moja moja.

Mpanda na Katavi ya miaka miwili iliyopita si ya leo, there is tremendous development.

And Kwa hakika haitawezekana kujenga flyover Mpanda au Katavi yoote kabla hata ya Tabora.
mkuu una ujuaji wa kijinga sana (nahisi shuleni ulikuwa john kisomo) iyo katavi unayo nisimulia ni ipi? now kuna ujenzi wa barabara za ndani chini ya casco nipo hapa naona, majuzi nimetoka kugoma lami inaanzia kabungu hadi mjini (barabara iko kwenye matengenezo)

Yaani bado una ujuaji wa zamani sana, nimekuuliza wapi barabara ya katavi-tabora wamesha weka lami hujibu.

unaleta braah braah za upembuzi yakinifu wapi nimesema nataka lijengwe daraja la juu mpanda (ikiwa tu barabara hazipo)
 
Kwanza, Kubali kuwa haupo Katavi au ulishawahi kuishi Katavi na umehama/ umeondoka.

pili, napenda ufahamu mkoa wa Katavi umetokana na jina la National Park, tukiachana na originality ya jina kuhusu kutambika, hivyo hakuna sehemu au eneo utakalofika na kupoint kuwa sasa hapa ndio katavi, unless uende national park, hoja yangu ni kwamba unaposema kuna barabara za ndani zinazojengwa Katavi, zinajengwa maeneo yapi.

Tatu, narudia tena, bajeti inapopitishwa tu - barabara haitatokea tu hapo kama kuwasha umeme.

Nne, sasa ondoka barabara Mpanda - Tabora, angalia kinachoendelea, halafu sema lami imewekwa au bado.

hahhahahaha we jamaa ni john kisomo sana unasoma mambo mengi hadi wapitiliza nimekwambia barabara za ndani zinajengwa na kampuni ya casco waniuliza barabara gani tena aya madukani barabara zote zile anzia ya istqam hdi hosp. njoi hii ya kwenda benki (nmb) barabara ya msakila kwenda kazima, barabara ya town pale kushuka mahakamani, barabara ya sokoni kupita nyuma ya uwanja, msakilia kupita tanesco (ilipo hamishiwa sasa) kwenda mikocheni

niko katavi huwa nakuja kulima huku mkuu, unahisi nakupa porojo hadi nikupe ushaidi wa picha
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Asante nimeelewa kumbe huwa unaenda huko kulima

Bugando Hospital ilikuwa ijengwe Bukoba kwa msaada wafadhili wakatoliki duniani waliomupa Mwadhama Karidinali Lauliani Rugambwa wa kwanza barani Africa lakini kwa busara za Mwalimu Nyerere na Karidinali Rugambwa msaada huo waliamuwa ijengwe Mwanza hili watu wote wa kanda ya Ziwa wapate huduma za matibabu.Ndugu zangu daima tujali vipa umbele vyetu kusaidia watu wanyonge na masikini.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
uwanja upo tu hauna maana sana zaidi ya vindege vya watalii na kunyunyiza sumu mbugani huko.

barabara ya katavi-tabora haina lami, katavi-kgm (iko kwenye matengenezo lami km 10 tayar)

katavi ni mkoa flani ukitaka kusafiri (iwe kuingia au kutoka ) unajiuliza sana usafiri ama uache tena masika ndo balaa.
Umesahau kusema kwamba barabara ya Mpanda - Tabora km 360 ipo katika matengenezo, kwamba kuna wakandarasi 03 wako site ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami unaendelea.
 
Huyo zipompa sio mkazi wa huko, hana details
mkuu umeamua kutoelewa tu, tangu mwanzo nimesha sema siku zikikamilika ntasema ila mpaka sasa katavi bado haijaunganishwa kwa lami upnde wa tabora na kigoma (zote ziko kwenye matengenezo)

mimi nsha kua mkazi wa huku nna miaka 3 sasa na sasa ivi nipo huku
 
Umesahau kusema kwamba barabara ya Mpanda - Tabora km 360 ipo katika matengenezo, kwamba kuna wakandarasi 03 wako site ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami unaendelea.
bado haijakamilika ikikamilika tutasema mkuu wala usipate shida
 
Katika utawala uliopita tulishuhudia miradi mikubwa ikipangwa kutekelezwa jijini Dar na Pwani. Naikumbuka miradi ya Mloganzila, bandari ya Bagamoyo, by-pass ya daraja la salander, BRT, nk. Hii ni miradi mikubwa sana kwa umaskini wetu. Miradi hiyo ilikuwa mikopo ambayo inalipwa na wananchi wa nchi nzima. Naona tena kuna muendelezo wa miradi mikubwa ndani ya jiji letu bila kujali shida zilizoko mikoani. Rais ametoa tena ahadi ya ujenzi wa flyover zingine ndani ya jiji la Dar es salaam.

Sababu ya maamuzi kama haya haieleweki lakini huenda ni kwa sababu watoa maamuzi wana makazi jijini Dar na wanajisikia kupamba makazi yao. Mikoa ya kati yaani Dodoma, singida, Tabora hadi shinyanga haina hospitali hata moja ya rufaa. Je, kwa nini Muloganzila haikusogezwa mikoa hiyo? Tukumbuke mikoa ya kusini pia haina hospitali ya maana. Ile ya Mbeya ni alama ya malengo na wengi wanajikuta wakielekea hospitali ya wamisionari, Peramiho. Kuna kundi linasifia jiji la Dar na kusema ni kitovu cha biashara. Huo si ukweli. Dar ni njia ya biashara. Mapato yetu makubwa ni Utalii na madini. Utalii uko Serengeti na Kilimanjaro, madini yako kanda ya ziwa. Kwa nini tuendelee kutumia pesa nyingi kiasi hicho kwa hisia ya jiji tu, bila sababu ya maana?

Najaribu kujiuliza, MV Nyerere imepoteza maisha ya watu kwa umaskini wao. Je, leo hii rais hawezi kutangaza maamuzi magumu na kuhamisha hizo pesa za flyover mpya za Dar pamoja na daraja la salander akijumulisha na pesa ya kivuko kipya kilichoahidiwa ili kuwajengea wana Ukara daraja refu kwa safari ya kisiwa chao? Je hatuwezi kuunganisha visiwa vya Jamuhuri hii kwa madaraja badala ya flyover mpya?

Flyover ni nzuri lakini tuwe na kiasi. Tugawane maendeleo badala ya kupamba jiji moja ndani ya nchi kubwa kama hii. Maamuzi mabovu kama haya husababisha ukuaji wa jiji moja na kuongeza wahamiaji kutoka mikoani kila siku. Mifano ya maamuzi kama hayo ziko ktk nchi zetu za kimaskini: Kongo DRC, Afrika ya kati, nk. Huko kila mtu anataka akaishi mji mkuu wa nchi maana hakuna mji mwingine wa maana!

Nchi haiendelei kwa kuipamba Dar. Tunahitaji maji safi, shule za kiwango, hospitali na barabara kwa nchi nzima.
Hatimaye leo humu JF nimekutana na mtu mwenye mtazamo kama wangu. Nadharau sana kuona jiji la Dar lina wakazi almost milioni 5 wakati linalofuatia, hata robo ya watu halifiki. Ukihesabu skyscrapers za Dar, ujaribu kulinganisha na Majiji yanayofuatia kwa skyscrapers - Arusha na Mwanza, utagundua namna tulivyo bado vilaza kama Nchi.
Wazungu hasa wa Uingereza na Ufaransa, wanajilaumu sana kwa namna walivyoruhusu London na Paris kudominate kila kitu katika maisha ya mataifa hayo na kuyafanya maeneo mengine kuwa marginalized.
Angalao by 1960s - 1990s London ilikuwa inapungua kutokana na uwekezaji kusambaa maeneo yote ya Nchi. Leo hii, watu wabasifia Ujerumani kwa kuwa na balance katika maendeleo bila ya kuwa na dominant metropolitan city - Berlin (East), Hamburg (North), Munich (south), Frankfurt (central) na Cologne (west): yote hiyo inazidiana katika sifa tofauti tofauti.
Ndiyo umuhimu wa Sera ya Majimbo ya CHADEMA huwa naiona inaleta maana.
Ndiyo maana naunga mkono kwa zaidi ya asilimia 100% HQ kwenda Dom angalao kubalance maendeleo kwa maeneo ya mbali.
Ajabu ni kuwa, Kanda ya Ziwa yenye watu zaidi milioni 16, haina Chuo Kikuu cha Umma, kweli?
Nilishangaa sana Watanzania wenzangu wanaodai kuumia na wingi wa abiria kwenye kivuko cha MV Nyerere. Waambieni waende Ukerewe na Uzinza (Maisome, Kome) wataelewa hasara ya kukalia kujenga eneo moja na kusahau mengine - wakazi wa Visiwa hivyo wanezoea shida hizo na wanaona kawaida. Kanda ya Ziwa wanashukuru sana anachofanya Magufuli hasa kutangaza kujenga meli mpya ya kwenda Bukoba na pia kivuko kingine cha Ukara.
 
Safari ni hatua,
1. Dar es salaam ni zaidi ya mkoa, ni lango la nchi mbalimbali - Kenya, Zambia, Malawi, DRC, Zimbabwe, Rwanda, Burundi, Uganda, Sudan Kusini, n.k kwa hio eneo hili lisiangaliwe Kama mkoa wa Ruvuma, au Tandahimba.

2. Dar es salaam, capital ambapo taasisi za kitaifa na kimataifa zimebase, si kama huko Njombe, Musoma ama Simanjiro lazima facilities za msingi kama hizo ziwepo kwa umuhimu huo, hii ni kanuni ya ulimwengu wote.

3. Mtu kutokuwa na choo ni uzembe wake, kama sio utashi wake, hata huko kwingineko watu wanajisaidia kwenye majani.

4. Tabora, Mtwara, kahama, Kibaha, Kigoma, Mpanda, Bariadi maeneo mengine mengi hayakuwa hivi - yameemdelea kwa maana ya barabara na majengo mazuri na other facilities za kijamii na kiuchumi katika miaka 10 iliyopita.

5. Safari ni hatua,
Tunachojadili kinahitaji mtu anayeweza kuwaza mambo ya maana. Usijibu tu kama insha ya darasani.
Dar ni lango la nchi, sawa! Kuna aliyelalama ujenzi wa airport? Kuna asiyeridhika upanuzi wa bandari? nani asiyependa SGR ianzie Dar? Ukumbuke lango kuu la Burundi linaweza kuwa liko Kigoma! Lango kuu la Uganda ni Kagera na hivyo hivyo lango kuu la Kenya linaweza kuwa liko Tarime au Arusha. Ukiulizwa nini kinapitia Dar toka Burundi unaweza kueleza au basi tu ulisikia clouds FM?

Tusichotaka ni kuweka hizo flyover kwa nadhalia kwamba eti foleni za Dar zinatia hasara ya bilioni kadhaa. wakiulizwa ni hesabu gani hiyo, hakuna anayefahamu namba hizo wanazipataje. Wengine wansema jiji linapendeza!

Halafu kila unachokumbuka unajiandikia tu! Taasisi gani za kimataifa ziko Dar? Au ulimaanisha Nairobi?
 
Hivi list ya mikoa 10 inayochangia kiasi kikubwa kwenye pato la taifa unaijua? Itafute kwanza afu ndipo uje kubishana kwa facts na sio chuki binafsi. Asante
Uliisikia Clouds FM? Nawe ukabeba habari bila kujiuliza. Nilishavuka kiwango hicho:
 
Tukubaliane kwanza, nani anasahihisha hizi insha?

Back
Top Bottom