Serikali kuwaajiri walimu 9,000

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Serikali kuwaajiri walimu 9,000


Na Edmund Mihale

SERIKALI imerudisha matumani ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu waliomaliza katika nyuo, mbalimbali hapa nchi baada ya kutangaza kuwaajiri wote waliko mitaani.Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na
kuasiniwa na Waziri wa wizara hiyo, Dkt Shukuru Kawambwa, ilieleza jana kuwa walimu wa watakaoajiriwa serikalini kwa mwaka wa fedha 2010/11 ni 9,226.

Alieleza kuwa miongoni mwao wamo wenye shahada 4,920 na wenye stashahada ni 4,306 hivyo kufanya walimu watakaoajiriwa mwaka huu kuwa 9,039 ambao wamepangwa kufundisha katika shule za sekondari na walimu 187 wamepangwa kufundisha katika vyuo vya ualimu.

"Katika mwaka wa masomo 2009/10 jumla ya wanafunzi 19,652 walihitimu mafunzo ya ualimu wakiwemo ngazi ya shahada 12,120 na stashahada 7,532. Kati ya wanafunzi hao jumla ya wanafunzi 17,684 walihitimu na kufaulu masomo yao, wenye shahada wakiwa 12,095 na wenye stashahada 5,589.

"Uchambuzi wa sifa za wahitimu 17,684 waliohitimu na kufaulu mitihani yao umeonesha kuwa jumla ya wahitimu 8,857 wametoka kazini (in-service). Idadi hiyo inajumuisha wenye shahada 7,437 (25 kutoka Zanzibar) na wenye stashahada 1,420. Walimu hao wamerudi kwa waajiri wao ili wapangiwe kazi kulingana na elimu yao," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Alieleza kuwa kuna wahitimu 328 kutoka Zanzibar wakiwemo 303 tarajali na 25 kutoka kazini ambao wanatarajiwa kuajiriwa katika shule na vyuo vya Zanzibar. Hivyo, wahitimu wanaobakia ambao wamepangwa kufundisha katika shule za sekondari na vyuo vya ualimu Tanzania Bara ni 8,524 wakiwemo wenye shahada 4,355 na wenye stashahada 4,169.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza wahitimu 8,524 waliohitimu na kufaulu mitihani yao wataajiriwa na serikali katika mwaka huu wa fedha. Kwakuwa wilevile serikali imekubali kuajiri walimu 702 wakiwemo 565 wenye shahada na 137 wenye stashahada waliomaliza mafunzo yao miaka ya nyuma ambao wameomba kuajiriwa serikalini.

Walimu wote wa shule za sekondari wamepangiwa katika halmashauri mbalimbali kwa kutumia kigezo cha upungufu wa walimu katika halmashauri husika.

"Hivyo, kila mwalimu anatakiwa kuripoti katika halmashauri aliyopangwa kwa kuwa fedha za mshahara wake zimekasimiwa kwenye halmashauri alikopangwa na si vinginevyo. Orodha ya walimu hao na halmashauri walikopangwa zimetumwa kwenye mikoa na halmashauri.

"Orodha hiyo inapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (WELCOME TO MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING OFFICIAL WEBSITE:::::::::) na tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa www.pmoralg.go.tz)," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Walimu wote wapya wametakiwa kuhakikisha kwamba wanaripoti katika halmashauri ya vyuo vya ualimu walikopangwa ifikapo Januari 24 mwaka huu na kuwataka watendaji na wasimamizi wa elimu kwenye halmashauri na vyuo vya ualimu watakuwepo kuwapokea.

Taarifa hiyo ilitoa onyo kwa mwalimu yeyote atakayeshindwa kuripoti kwenye kiyuo chake cha kazi alichopangiwa baada ya siku saba (7) tangu tarehe anayotakiwa kuripoti atahesabika kuwa amekataa kukubali nafasi ya ajira aliyopewa na serikali.

Ilieleza kuwa baada ya kuripoti kwenye halmashauri au vyuo waajiri watatakiwa kuwajazia walimu hao fomu maalumu zenye taarifa ya kiutumishi ya Mtumishi (Personal Data Form) na kuziwasilisha Ofisi ya Rais, Ofisi ya Utumishi na barua ya ajira ya mtumishi.

Ilieleza kuwa taarifa hizo zinatakiwa kuwa katika “hard” na “soft copy” ziwasilishwe utumishi kabla au ifikapo Januari 29, mwaka huu ili watumishi hao waingizwe katika mfumo wa malipo (Payroll). Na waajiri wanakumbushwa kwamba “Computer Data Sheet” hazitahitajika katika shughuli hiyo.

Ilielkeza kuwa waajiri Wakurugenzi wa Halmashauri na Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi watawalipa malipo stahili kwa mujibu wa nyaraka na miongozo ya serikali kuhusu waajiriwa wapya.

 
It is a struggle of supply-siders that will never succeed..................
 
Back
Top Bottom