Serikali kutumia shs.bilioni 150 kuchunguza kwanini watoto wanamaliza hawajui kusoma wala kuandika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kutumia shs.bilioni 150 kuchunguza kwanini watoto wanamaliza hawajui kusoma wala kuandika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by politiki, Apr 10, 2012.

 1. p

  politiki JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Wanafunzi 5,000 waliofaulu hawajui kusoma, kuandika
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 09 April 2012 20:42
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0diggsdigg

  Fredy Azzah
  IMEBAINIKA kwamba wanafunzi 5,200 waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, hawajui kusoma wala kuandika.

  Kutokana na sababu hiyo, habari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zinasema kwamba wanafunzi hao wataachishwa masomo na Serikali inaangalia uwezekano wa kuchukua hatua za kisheria wanafunzi hao na wakuu wa shule wanazotoka ili kukomesha tatizo hilo.

  Wanafunzi hao wanatoka katika mikoa yote ya Tanzania bara, isipokuwa Kigoma ambao taarifa zake hazijafika katika wizara hiyo.

  Wanafunzi hao wamebanika kutojua kusoma wala kuandika baada ya kupewa majaribio ya kupima uwezo wao wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) baada ya kuripoti shuleni kama ilivyoagizwa na Serikali.

  Desemba 14, mwaka jana wakati akitangaza matokeo ya Mitihani ya Darasa la Saba, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo aliagiza wanafunzi wote watakaoingia kidato cha kwanza mwaka huu wapimwe kwanza uwezo wao wa Kusoma na Kuandika.

  Agizo hilo lilitokana na udanganyifu uliojitokeza kwenye mtihani huo na kusababisha watoto 9,736 kufutiwa matokeo.

  Wanafunzi waliofanya mtihani huo walikuwa 983,545 na waliofaulu ni 567,567. Kati yao wasichana walikuwa 278,377 sawa na asilimia 54.48 na wavulana walikuwa 289,190 sawa na asilimia 62.49.

  Akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) mwishoni mwa wiki, Mulugo alisema tathmini inaonyesha kuwa Mkoa wa Kilimanjaro umeongoza kwa kuwa na wanafunzi wengi wasiojua kusoma na kuandika.

  "Mkoa wa Kilimanjaro una wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika wapatao 660, Tanga 490 na Dar es Salaam 208," alisema Mulugo bila kutaja matokeo ya mikoa mengine.

  "Hili ndilo janga la kitaifa sasa. Siyo hayo mengine ambayo watu wanasema ni majanga ya kitaifa. Lazima tujiulize kwa nini watoto wanamaliza darasa la saba wakiwa hawajui kusoma wala kuandika na halafu wanafaulu?" alihoji kuongeza:

  "Je, siku hizi hakuna tena somo la kusoma na kuandika? Kwa nini mtoto amalize shule bila kuwa na maarifa ya KKK? Mitaala (mitalaa) mnayoandika kwa nini hamsaidii mtoto katika hili? Nataka leo nijue tatizo liko wapi, mengine (matatizo) ya Serikali; walimu, vitabu, miundombinu na majibu yake sisi tunayo."

  "Jambo la kusikitisha kuna mpaka baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tatu, ambao hawajui kusoma wala kuandika. Tulipofikia siyo pazuri hata kidogo, lazima tuwe makini jamani. Tuheshimu Baraza la Mitihani (Necta) tupate ufumbuzi wa mambo haya taifa hili ni letu sote, lazima tuhakikishe linasimama imara."

  Alisema Serikali kwa upande wake, imejipanga kufanya utafiti na kujua chanzo cha tatizo na kuwa imepata Sh150bilioni kutoka Global Partnership for Education (GPE), kwa ajili hiyo.

  Kaimu Mkurugenzi wa TET, Habib Fentu alisema mitalaa waliyoandika imesisitiza mwalimu kufanya tathmini ya kile alichofundisha kila baada ya mada husika kumalizikia.

  "Kwa hiyo hapa sasa suala la uwajibikaji linakuja, inakuwaje mtoto amalize darasa la saba akiwa hajui kusoma, kuandika wala kuhesabu na mwalimu wa darasa yupo, mwalimu wa taaluma, mwalimu mkuu na kamati ya shule vipo?"

  Katika matokeo ya darasa la saba yaliyotangazwa mwaka jana, Mkoa wa Manyara uliongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliofutiwa matokeo ukifuatiwa na Arusha.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  MY TAKE: Pesa hizi zingeweza kutumika kujaza vitabu vya kiada, kuongeza waalimu na kuongeza madarasa ili
  kupunguza idadi ya wanafunzi kujazana ktk darasa moja.
   
 2. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Duh! Haiingii akilini kabisa!?
   
 3. M

  Mwanyava JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Unapofanya utafiti kwa jambo lilowazi unatafiti nini?
  Walimu morari ya kufundisha imeshuka kama siyo kufa kabisa. Na watoto wasipofaulu shule au mkuu wa shule anawajibishwa na mabosi wake. Kukwepa adhabu, kwanini mwalimu au walimu wasiwafanyie mitihani wanafunzi na shule yao ikaonekana imefaulisha? Fedha hizo zingetumika kuwa jengea mazingira mazuri walimu na shule ili walimu hawa warudishe imani kwa serikali yao kuwa inawajali katika masirahi yao. Pandisha mishahara ya walimu na wapewe vitendea kazi tuone kama hilo tatizo halijaisha.
   
 4. p

  politiki JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  wanilipe mimi wala siitaji kufanya utafiti nitawashauri wazalishe waalimu wa kutosha, wana improve maslahi ya waalim, waongeze vifaa vya kufundishia na kujenga madarasa ili kupunguza idadi ya wanafunzi kwenye darasa moja ili waalim wawe na one to one discussion na wanafunzi wao
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Waziri anakiri kwamba anajua matatizo ya walimu, vitabu, madarasa na mengineyo. Sasa kama anajua hayo matatizo, uchunguzi/utafiti ni wa nini?

  Labda kama anataka kutafiti kwamba inakuwaje mwanafunzi ambaye hajui kusoma wala kuandika anafaulu na kuchaguliwa kuingia sekondari.

  Lakini kiini cha kutojua kusoma na kuandika ni hicho alichokitaja hapo. Shule unakuta ina mwalimu 1 au 2, atafundishaje madarasa 7 ambapo kuanzia darasa la nne, kila darasa lina wastani wa masomo 8? Hakuna vitabu na wanasomea chini ya mti. Mtoto akiamua kwenda shule mara moja kwa wiki utamlaumu?

  Mara nyingi huwa nasema Tanzania tuna fedha nyingi sana ili hatujui priorities na matokeo yake tunaishia kutumia kwenye warsha, semina na makongamano na huo utafiti mbuzi wa kutafiti kitu ambacho majibu yake yako obvious.
   
 6. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Duh! Haiingii akilini kabisa!? Huu ni ufujaji uliopitiliza kiasi kama ni kweli basi hatuna serikali! kinachothibitika hapa ni kwamba baada ya viongozi kubanwa kila angle wasiibe pesa ya nchi mathalani kulipa DOWANS. Sasa wanajaribu kila njia kuiba au kupata chanel ya kuiba ambayo ni justifiable!
   
 7. C

  Chokler Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii nikuonyesha dhahiri kabisa kwamba serekali ya JK haiko makini hata kidogo kwa sababu zifuatazo huwezi kuwapata waalimu wa mteremko (crash program) walio-fail form four kuja kufundisha watu unotarajia wafauli wakiwa wanauwezo zaidi ya mwalimu, haiwezekani wakaguzi wa elimu na wizara wakaridhika kwa maelezo ya hao waalimu juu ya kufeli kwa hao wanafunzi.
   
 8. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jamani huu ni ulaji wa watu na vigogo tu hakuna lolote. Hizo hela waboreshe maslai ya walimu tu hapo ndio watoto wataanza kufundishwa lazivyo mgomo baridi bado utaendelea na taaluma itazidi kushuka. Hata leo bungeni swali aliulizwa hawa gasia kwanini graduate mwalimu na daktari mishahara yao tofauti ni kubwa na waziri alivyojibu ni dhahiri dharau kwa taaluma ya ualimu. Kazi tunayo hizo hela za kula bata eti utafiti na tatizo linajulikana. Wadanganyika.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Jamani, wanafunzi hawana vitabu, madawati, walimu na library mnaunda tume ili ifanye nini?
   
 10. J

  John W. Mlacha Verified User

  #10
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  kikwete aliulizwa kwa nini AFRIKA MASKINI AKASEMA NI KWA VILE HAINA PESA ETI.
  MTU HAJUI KUSOMA NA KUANDIKA SASA NANI HAUI SABABU? KWELI HII NCHI HAMUIPENDI KWELI MMESHAJISAHAU KABISAAAAA
   
 11. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Ujinga mtupu....haya ni matumizi mabaya ya fedha ya walipa kodi....wanataka wapige deal kwenye hizi pesa kama walivyozoea....Tatizo la watoto kumaliza wakiwa hawajui kusoma na kuandika serikali wanalijua sana tu......mbona zamani haikuwa hivi????jibu la tatizo hili ni kuwahudumia waalimu tu.....hamna ujanja mwingine....wewe leo unataka watoto wajue kusoma na kuandika wakati wale unaotgemea wawafundishe(waalimu)unawadharau na huwalipi vizuri..unategemea nini???na bado...kama itaendelea hivi itakuja kufika watoto wanamaliza form four hawajui kitu.....dawa ni waalimu tu.....hudumieni waalimu watoto wenu wafundishwe vizuri...
   
 12. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #12
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwanini wagharamike kufanya utafiti wakati inaeleweka wazi kuwa walimu wapo kwenye mgomo baridi siku nyingi.
   
 13. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #13
  Apr 10, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Haya ndo matokeo ya serikali isiyo makini katika kusimamia sera na mipango
   
 14. Lavie

  Lavie Member

  #14
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nyie endeleeni tu kutoa misharaha midogo kwa walimu, mtaona kama matatizo ya elimu yatapungua. Na bado huu ni mwanzo, si mmeamua kuwekeza kwenye madarasa, semina, n.k. Bila kujali mishahara ya walimu? mgomo kama kawa unaendelea, hadi siku mtakapoamua kuwathamini walimu ndio mtaona changes. Si huwa mnashughulikia ya madokta kwa sababu wataua miili ya watu, walimu wameamua kuua akili.
   
 15. C

  Campana JF-Expert Member

  #15
  Apr 10, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mitihani yenyewe ni multiple choice ABCD hadi hisabati.

  Nani atafeli? Labda Mwanaasha type
   
 16. N

  Njaare JF-Expert Member

  #16
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Upuuzi mtupu! Hajui kuwa walimu wako kwenye mgomo toka Mkoba autangaze kabla ya 2012!!!!!!????? Hizo hela si mlipe madai ya walimu!!!!
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kweli wacha wenye meno watafune mifupa kwa kuwa bado meno ipo! Utafiti wa kutumia 150 billion uko wapi? Hizo pesa ni za kugawana tu. Wanipe million moja tu kesho nawapa sababu kwa kuwa ziko wazi na hazihitaji utafiti.
   
 18. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #18
  Apr 10, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hivi unadhani hawalijui hilo?? Wanajua fika? CCM sasa wanatapatapa kutafuta watakapochota mabilioni ya uchaguzi 2015. Chunga sana tabia ya CCM. Hakuna kitu kama hicho eti hawajui kwanini wanafunzi wanafeli.
  Kwanza huyo Waziri anastahili kuwajibishwa kabla ya yote, hakafu hatua zianze kuchukuliwa.
  Mengi tutayafahamu tunavyozidi kukaribia 2015.
   
Loading...