MANI
Platinum Member
- Feb 22, 2010
- 7,320
- 6,376
JK ndo wa kuondoka maana ni dhaifu sana
Hoping this to be true !
JK ndo wa kuondoka maana ni dhaifu sana
Kuna tetesi kwamba mtoto wa mkulima kesho anaachia ngazi kwani tatizo la madaktari limekuwa gumu kwake na kwa kifupi limemshinda hivyo ni bora akaachia ngazi kwani mpaka sasa hawezi kubadili lolote na hivyo watanzania wataendelea kupoteza maisha asipofanya hivyo.
My take
Tusubiri kesho lakini mwishi Vipi?
Usalama
yeah
kunakipindi ni lazima serikali ifanye maamuzi magumu ili kunusuru maisha ya watu wake
ukisikia mtu mzima anasema NA LIWALO NA LIWE tutegemee maamuzi magumu kutoka kwa serikali
Dakika 120 zimekwisha, timu hazijafungana na sasa tunaelekea kwenye penati. Mshindi lazima apatikane
Hana jipya,
Mh. Zambi anahoji kuwa japokuwa kesi mahakamani madaktari wameendelea kugoma serikali inasemaje?
Pinda kasema kesho watalitolea maamuzi na kasema LITAKALO KUWA NA LIWE. Hivi kwa kauli hii tuna waziri mkuu kweli??
Atakuja na kusema kuwa hakusema chochote kama ilivyokuwa wakati wabunge walivyohatarisha kibarua chake bungeni walipoungana kuwawajibisha mawaziri kwa kujihusisha na ufisadi.Baada ya Mhe. Zambi kutaka majibu ya Serikali (leo Bungeni) Waziri Mkuu ameahidi kesho serikali italitoa majibu/tamko kesho. Tutarajiwe nini Great Thinkers?
Huyu Pinda Amepinda na kauli zake! Ama kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa!
By Mpendamabadiliko
Watanzania wenzangu hizi kauli tunazozitoa zinaweza kuonekana ni nyepesi sana lakini madhara yake yanaweza kuwa makubwa sana na yakaathiri watu wengi wasiokuwa na hatia. Tuhuma ya kuteka mtu kwa nia ya kumuuwa kijasusi ni shutuma kubwa sana. Ni lazima mtu anayetoa kauli kubwa kama hiyo awe na ushahidi wa kutosha.
Sijui kati yetu tunaongea kwa kumsisitizo tuna ushahidi wowte wa kuonesha ni nani kutoka serikali na kwa amri ya nani kahusika na utekaji huo? Kama hatuna ushahidi kwa nini tusifanye uchunguzi kwa chini chini na hatimaye tukipata ushahidi ndio tuwe na haki ya kuzungumza?
Mbali ya kusoma magezetini na kusikia katika maredio na vyombo vingine vya habari ni ushahidi gani mwingine tulionao wa kueleza chimbuko la utekaji na sababu zake?
Kwa nini tusingoje vyombo vya usalama vikafanya uchunguzi na hatimaye tukawa na sauti ya kusemea? Muenendo huu tunaoanza kuuzoea ni mbaya sana na unaleta dalili mbaya katika mstakbari wa amani yetu. Ni bora moderator kama yupo akachuja habari kama hizi.
Mimi ni mmoja kati ya waliosikitishwa na kuhuzunishwa na tukio lililompata ndugu yetu. Natoa changamoto kwa vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina na kupata chanzo na wahusika katika tukio hili la kinyama na ambalo liko tofauti na mazingira ya Tanzania. Naungana na watanzania wenzangu pia kumtakia matibabu mema ndugy yetu na Mungu amponeshe mapema
Acha uoga, uko nyumbani jisikie huru.