Serikali kutishia jela wanasiasa juu ya Katiba ni kukandamiza Demokrasi, ni uimla | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kutishia jela wanasiasa juu ya Katiba ni kukandamiza Demokrasi, ni uimla

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Candid Scope, Apr 7, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hoja ya Katiba imeibuliwa na wanasiasa kipindi cha Kampeni Mwakajana. Hatimaye hoja ikaungwa mkono na wananchi baada ya kuelimishwa umuhimu wake. Faulo iliyofanywa na serikali kufinyanga matokeao ya uchachuzi kupitia tume ya uchaguzi imehamasisha zaidi wasomi, wanavyuo, wanachi na wanasiasa kudai mabadiliko ya Katiba.

  Waangalizi wa kimataifa hasa wa kutoka Jumuiya ya Ulaya waliweka bayana jinsi uchakachuaji wa uchaguzi ulivyofanywa na serikali kupendelea waliopo madarakani, na hivyo kupendekeza mabadiliko katika sheria za uchaguzi maana yake mabadiliko ya katiba inayotendea haki wananchi wote bila kujali chama cha kisiasa ili kila raia awe na uhuru wa kugombea na haki katika kulinda na kutangaza matokeo ya uchaguzi.

  Viongozi wa kisiasa ndio weledi wa kuelimisha wananchi na ndio wanaoeleweka kwa kutafsiri vizuri kuliko kutumia vyombo vya serikali ambavyo hutumia nguvu bila weledi wa kuelimisha umma. Kutumia watumishi wa serikali tu maana yake watakuwa na jukumu la kulinda maslahi ya wakubwa wao waliowaweka madarakani. Wanasiasa ndio wanaofahamu zaidi matatizo yanayojilia nchini na ndio wanaosikiliza matatizo ya wananchi, sasa iweje wawekwe kando maana yake kuna kiinimacho kinachokusudiwa kufanywa ili kuendelea kulinda himaya ya watawala waliopo.

  Mswada wa Katiba mpya utafsiriwe katika lugha ya kitaifa, lugha ambayo Watanzania wanaijua, na hivyo wananchi watakuwa na fursa ya kuisoma na kuelewa kilichomo ndani ya mswada, na hii itajenga uelewa wa yaliyomo, wananchi kuchangia maoni yao baada ya kusoma, kuujadili na kuuelewa.
  Katu wananchi tusikubali kudangwanywa tena safari hii, na hakuna sababu ya kukimbiza mswada wa katiba hadi wananchi waelewe.

  Rais, Wabunge, wawakilishi wengine pamoja na watumishi wa serikali ni waajiriwa na wawajibikaji kwa wananchi waliowapa udhamini wa kuwatumikia, kwa msingi huo wasitumie nafasi walizopewa na wananchi kunyang'anya haki yao ya msingi ya kuchangia uundwaji wa katiba ya nchi.

  Hakuna mtu atakayepinga kwa namna ye yote hata kupeleka pingamizi mahakamani kama kila mtu ameshirikishwa ipasavyo, la sivyo ni usanii tu unaokusudiwa kurudiwa katika uundwaji wa Katiba kama ilivyozoeleka kuundwa tume mbalimbali huko nyuma na kisha kuishia ikulu tu.

  Vitisho vya kupelekwa jeja kwenye mswada uliopelekwa Dodoma viondolewe mara moja bila masharti kwa kuwa kufanya hivyo ni kukandamiza demokrasi nchini na inaweza sababisha machafuko ambayo yanaepukika.
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Kama kweli wataipisha hiyo mswada itakuwa ni kali ya mwaka! sijui watakuwa wanafikiri nini maana tutakuwa tunajaribu kwenda stone age wakati kila aina ya upepo wa mabadiliko inatupeleka information age.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana nawe maana sasa tunarudia kwenye enzi za stone age, na ole wako useme dunia huzungukia jua unauawa kwa mawe ndo enzi za utawala wa Tanzania awamu ya nne
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hivi Serikali mabadiliko makubwa ya kidemokrasia yanayotokea hasa bara la Afrika na middle east bado wanafumbia macho na kuendekeza usanii wa zilipendwa?
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu.

  Udhaifu ulioneshwa na CDM katika kuunda upinzani unaotanua wigo kwa kuingiza vyama vyengine vya upinzani vitatugharimu vibaya sana katika kudai demokrasia ya kweli. Udhaifu huu umeinufaisha CCM kuburuza au kufanya mambo vile wanataka na wanapenda.

  Sasa CDM walisema milango iko wazi ya mashirikiano na vyama vyengine siku za usoni.Je wakati haujafika bado?

  CDM pekee kama chama makini kitaweza kuzuia bunge lenye wabunge wengi wa CCM wasiupitishe?, ambao tunajua kuwa wapo pale kulipa fadhila kwa Chama, kuupitisha hata kama ni kwa kuwaweka sawa wabunge wa CCM kupitia semina elekezi kuwa waupitishe.

  Wakuu..Katika kupitisha sheria basi mwananchi wa kawaida kuambiwa atoe maoni yake ni geresha tu...shughuli iko Bungeni na bunge ndio hivyo ni bunge la CCM.

  Bado upinzani hauoni umuhimu wa kushirikiana katika hili pia?
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ushirikiano wa vyama vya upinzani ni propaganda za CCM kwa kuwa wana vyama vyao vya upinzani walivianzisha strategically kuvuruga upinzani na agent wao wakubwa ni Mrema na John Cheyo na hivi karibuni wamemnasa Hammad Rashid.

  CHADEMA wanauwezo wa kuzuia muswada huu hata kama ukipita kwa kuwa Umma upo nyuma yao uwingi wa wabunge wa CCM haimaanishi kuwa wanawakilisha majority ya wananchi kwani ukweli kamili unajulikana kuwa ni wabunge wa NEC ambao majority hawakuchaguliwa na wananchi na wao wanalijua hilo usiku na mchana.
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Nafurahi kusikia kuwa CDM wanao umma nyuma yao au bege kwa bega...lakini umma huu sio utakaopiga kura ya kuupitisha huo mswada. Kura kama itapigwa basi ni bungeni...maana yake bunge la CCM huweza hata kuamuliwa kuwa sauti tu ya ndio bila kuhisabu kura.

  Well. soon tutajua uwezo huo. Nataka kujipa moyo kuwa mswada hautapitishwa kama ulivyo.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Serikali ya sisiem na sisiemu yenyewe wamekalia kuti kavu. Wanachofanya sasa ni kuruka jivu na kukanyaga moto. Nguvu ya umma ni zaidi ya wabunge 300 wa sisiem.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wananchi wakichachamaa kudai haki yao nakuambia Dodoma hapatoshi, je nchi nzima utamshika nani?
   
 10. N

  Nonda JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Wananchi wepi unaozungumzia wewe?
  Wanaopigwa bomu la machozi hawapo tena sehemu ya Tukio?
  Au sasa wananchi hawa wamekuwa born anew?

  Mkuu, nguvu ya umma sio hii ya keyboard, it should be on the ground.

  Unayosema nakubaliana nayo lakini bado sijamuona mwananchi mwenye sifa uliyoitaja hapa.
   
 11. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu, nimesoma tena na tena, mswada unasema hauruhusu 'vyama vya siasa na asasi husika (affiliates) sio wanasiasa, kwa uelewa wangu mdogo wanasiasa wanaruhusiwa!
   
 12. N

  Nonda JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Ninafarajika kuona bado tuko optimistic.

  It needs to be translated in action. In theory yes... nakubaliana na wewe.

  Wananchi ndio wenye nchi..lakini unaona jinsi serikali, kikundi kidogo tu kinavyotupigisha mchaka mchaka.
  Au nguvu za wananchi pia zimechakachuliwa?
  In TZ every thing but "maisha bora" is possible.
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,533
  Likes Received: 81,947
  Trophy Points: 280
  Mafisadi wameshauteka nyara mjadala wa katiba mpya. Kwa maoni yangu katiba itayopatikana itakuwa imejaa UPUUZI NA USANII MTUPU toka kwa mafisadi. Watanzania tuupinge kwa nguvu zetu zote mjadala huu wa katiba mpya ambao tayari mafisadi wameshauteka nyara na hauko huru kama ambavyo wengi wetu tulivyotarajia ili kutunga katiba wanayoitaka wao ili waendelee kutawala milele.
   
Loading...