Serikali kutisha na kuwafunga jela watumishi wa dini wanaojihusisha na siasa

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
Katika mpango wa kupambana na viongozi wa dini wanaoyumbisha serikali ya Kikwete na wanausalama wameamua kutumia nguvu kupita kiasi na inategemewa kuanza kuwasakama mapandri, maaskofu na mashehe wanaopingana na serikali kwa kiwango kikubwa.

Katika mpango wa kwanza ni kuwazushia vyesi zikiwemo za madawa ya kulevya, ubakaji na kuwatengenezea ajali za magari ili kuzima mpango wao wa kutofautiana na serikali.

Kwa ushauri wetu mpango huu ukitekelezeka kwa kiwango kikubwa unaweza kuipeleka nchi pasipotakiwa na kuyumbisha serikali zaidi kwani kuna kundi kubwa na mahusiano makubwa ya wanaharakati ndani ya dini zote na wameunda mitandao yao na kama wakishambuliwa kutakuwa na madhara makubwa.
 
Habari za kutunga au? Leta source hapa

Tayari kuna ujumbe wa barua pepe iliyotumwa kwa Askofu Kakobe ukiwa na vitisho na kumwamuru aachane na siasa la sivyo wanamyumbisha na kusimamia kesi yake ili kuhakikisha anashindwa .
source:mazungumzo ana kwa ana na Kakobe
 
Sawa mkuu,kama hali ndio hii basi Jk ameanza kuonesha Udikteta wake wazi na jambo la ajabu kwa nn hawataki kukosolewa wakati hawafanyi kile kinachotakiwa kufanywa,lakn Mungu atawalaani tu kwa kutishia watumishi wa Mungu
 
Kazi karibia inaanza sasa! Mwaka jana mwanzoni tulisemaga tu ya kwmb katu katu mambo kama haya hayana budi kutokea. Hii ni cha mtoto! Tusubirie siku ya mbele tutaona mengi. Kisa serikali legelege na matawi yake yote.
 
Oohoo kama ni kweli mwambieni mkuu wetu jakaya aachane na watumishi wa Mungu maana hao ni mboni ya jicho la Mungu, asije akaanguka ghafla na asiamke tena..! Mafisadi wamemshinda sasa anataka kupambana na watumishi? au mleta habari umeleta habari hapa ili watu wamchukie mkuu JK? em funguka..
 
Inamaanisha serikali ya ccm imekuwa mwendo wazimu kiasi hicho. Yaani serikali inalinda wezi wa rasili za umma na kuwashambulia wale wasiyo na hatia. Kama habari hii ni ya kweli basi vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotea kule Rowanda na Burundi hapa Tz ziko mbioni kutokea, no doubt at all. Go to hell ccm and its gvt!!!
 
Tayari kuna ujumbe wa barua pepe iliotumwa kwa mchungaji kakobe ukiwa na vitisho na kumwamulu aachane na siasa la sivyo wanamyumbisha na kusimamia kesi yake ili kuhakikisha anashindwa .

source:mazungumzo ana kwa ana na Kakobe

Mwambie akupe hiyo barua utuwekee hapa kwa uthibitisho...Otherwise ni uzushi mtupu... pengine huyo Kakobe anatishiwa na waumini wake tu ukiwemo wewe katika kesi ya kugombania mapato ya sadaka za waumini. Lete hiyo barua utuwekee hapa ndugu!
 
Sijawahi kusikia mashehe wakiwa kinyume na serekali ya ccm..hivyo nina wasiwasi na taarifa yako
 
wewe unakurupuka na kuja hapa na habari za kwenye vikao vyenu vya kahawa na kule saluni mnakosukana unatuletea hapa af bado unataka tukuite great thinker.................nyie ndo mnaotuharibia jamii forum nyie..........kajipange upya.
 
Katika mpango wa kupambana na viongozi wa dini wanaoyumbisha serikali ya Kikwete na wanausalama wameamua kutumia nguvu kupita kiasi na inategemewa kuanza kuwasakama mapandri, maaskofu na mashehe wanaopingana na serikali kwa kiwango kikubwa.
Katika mpango wa kwanza ni kuwazushia vyesi zikiwemo za madawa ya kulevya, ubakaji na kuwatengenezea ajali za magari ili kuzima mpango wao wa kutofautiana na serikali.

Kwa ushauri wetu mpango huu ukitekelezeka kwa kiwango kikubwa unaweza kuipeleka nchi pasipotakiwa na kuyumbisha serikali zaidi kwani kuna kundi kubwa na mahusiano makubwa ya wanaharakati ndani ya dini zote na wameunda mitandao yao na kama wakishambuliwa kutakuwa na madhara makubwa.

Naona umeanzisha harakati za kuwasafisha MAPUSHA , PENGO and Co.
 
Tayari kuna ujumbe wa barua pepe iliyotumwa kwa Askofu Kakobe ukiwa na vitisho na kumwamuru aachane na siasa la sivyo wanamyumbisha na kusimamia kesi yake ili kuhakikisha anashindwa .
source:mazungumzo ana kwa ana na Kakobe

Siyo kweli! Huu ni uzushi wa mchana kweupe! Mimi nimezungumza na Askofu Kakobe, sasa hivi, na amesema; na ninamnukuu, "Huo siyo ukweli, ni uzushi. Mimi sijapata barua pepe yoyote ya namna hiyo. Wala hakuna awezaye kunibabaisha kwa vitisho vya namna hiyo. Wanaujua msimamo wangu thabiti. Mimi ni mtu mzima, siwezi kutishiwa nyau! Ndugu huyo, huenda ana hoja ya msingi, hata hivyo, anapaswa ku "support" hoja yake kwa "verified facts", na siyo mambo ya kutunga." Mwisho wa kumnukuu.

Yeyote yule hapa JF, anaweza kuthibitisha kauli hii ya Askofu Kakobe, kwa kuzungumza naye kwa Namba 0765922198.
 
Tayari kuna ujumbe wa barua pepe iliyotumwa kwa Askofu Kakobe ukiwa na vitisho na kumwamuru aachane na siasa la sivyo wanamyumbisha na kusimamia kesi yake ili kuhakikisha anashindwa .
source:mazungumzo ana kwa ana na Kakobe
HABARI YAKO NI YA UONGO , NAKUSHAULI UTAFUTE NJIA NYINGINE YA KUMUTETEA BOSI WAKO!!!!
KWANZA KABISA HUNA JEURI YA KUONGEA NA ASKOFU KAKOBE ANA KWA ANA: uNAWEZA KUTUDANGANYA KATIKA YOTE UKAFANIKIWA LAKINI SI HILI LA KUZUNGUMUZA NA KAKOBE ANA KWA ANA!!!
HAPA UMECHEMUSHA!!!

NAADHA KUPATA MAJIBU KWAMBA WEWE NI MUUMINI WA PENGO KWA JINA GODWINE!!!
USIHUSISHE VITA YA PENGO KWA KUWATUMIA MAASKOFU WENGINE, MWACHE PENGO AJITETEE!!!!!!!!!!
 
serikali dhaifu hutumia resource na pe3sa kubwa kupambana na wqanaowakosoa wakat pesa izo na resource zake zingetumika kwa mambo ya msingi nchi ingepata maendeleo!
 
Back
Top Bottom