Serikali kutafuta dawa ya kansa ya kizazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kutafuta dawa ya kansa ya kizazi

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Sep 12, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Jakaya Mrisho Kikwete

  Burhani Yakub,
  Tanga

  SERIKALI imesema katika kipindi cha miaka mitano
  ijayo, Serikali yake itaelekeza nguvu zake kupambana na tatizo la kansa ya shingo ya kizazi ili kuokoa vifo vingi kwa wanawake.

  Hayo yalisemwa na Rais Jakaya Kikwete wakti akitoa ahadi hiyo jana alipokuwa akizungumza na wakazi wa Jiji la Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani.

  Alisema kutokana na kansa ya shingo ya kizazi kwa kuwa ni tatizo kubwa, Serikali imeamua kuelekeza nguvu zake katika
  kutafuta chanjo ya uhakika ili kuonda kabisa tatizo hilo.

  “Chanjo ya kansa ya shingo ipo,katika nchi za wenzetu,hivyo na sisitumeona hatuwezi kuachia wanawake wazidi kuteketea tutaifuata iliko ili tatizo hilo baadaye liweze kutoweka nchini,”alisema Kikwete.

  Alisema matayarisho ya kutoa chanjo hiyo, imeanza na kwamba ifikapo mwakani wanawake wataanza kuchanjwa ili wasiweze kupata maradhi hayo.
  Rais Kikwete alidokeza kuwa Serikali imejenga maabara kubwa na ya kisasa katika hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo ambayo ina uwezo wa kupima aina mbalimbali za magonjwa.

  “Maabara ya Bombo ni kubwa na ya kisasa yenye uwezo wa kupima magonjwa mbalimbali,”alisema.
  Alisema maabara hiyo imetolewa kwa msaada wa taaisi ya ABBOT ya Marekani na Serikali kuamua ijengwe katika Hosptaliya Bombo.

  Kuhusu ugonjwa wa malaria, Rais Kikwete alisema tayari serikali imepokea idadi ya vyandarua 14,000,000 na
  kwamba itahakikisha kila kaya inapewa ili kutokomeza ugonjwa wa
  malaria.

  chanzo : Serikali kutafuta dawa ya kansa ya kizazi
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kwa msaada wa watu wa marekani!!!!
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Sep 12, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Oh yeah America rocks!!! Hivi hii dunia leo hii ingekuwaje bila Marekani?
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hili jamaa ongo sana! Jamaa wa Abbot waliamua kujenga hiyo maabara Tanga sababu wana kazi zao na NIMR Tanga, wasingekubali kujenga sehemu nyingine yeyote (Bagamoyo) kwa shinikizo la serikali. Wanamaabara nyingine nzuri tu pale Muhimbili kule Bacteriology, sababu kuna tafiti za Wamarekani kutoka Havard. Wananchi wamedanganywa eti serikali iliamua, this is very low again from Kikwete! Siajabu kwa kauli hii ya uwongo wananchi walishangilia
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mkuu kuna long term strategy ya supplies and services contracts let alone philanthropic deed.... abbott is not only building hizi lab tanga, hata mnh wamefanya hivyo na kama unakumbuka prof lema alidai hawawezi tumia baadhi ya mashine... hii si siasa mazee
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  yeah they rock.... no wonder ilani ya chama pia ni kwa msaada wa watu wa marekani
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jamaa hana mpya ameamua kuingiza kwenye ahadi zake kisiasa! Kule CPL (Central Pathology Lab) jamaa wa Abbott wametengeneza maabara ya kisasa sana pale Muhimbili hospital nadhani ni miongoni mwa maabara nzuri nchini. Wanafanya serology tests nyingi tu,bacteriology tests na hata molecular assays. Jamaa kila kitu kizuri wanaweka kisiasa. Nakumbuka sana Prof Lema na hadithi zake, kinachotakiwa pale ni kuwapa vijana ajira na malipo ya kueleweka wafanye kazi. Nadhani Dir wa ile maabara ni dada mmoja wa South Afrika.
   
Loading...