Serikali kumlima barua balozi wa china nchini!

mageuzi1992

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
2,503
252
'' Serikali imesema mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini wanapaswa kutambua kuwa, wanawajibika kuheshimu Mkataba wa Kimataifa wa Vienna unaoainisha taratibu za Kidiplomasia...............Hii ni kutokana na wiki iliyopita balozi Lu Younqing wa China kujitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Shinyanga, huku amevalia moja ya sare za chama Hicho. Akizungumzia kitendo hicho Naibu Waziri wa mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, mahadhi Juma Maalim, alisema serikali inajiaandaa kumwandikia barua ya kumkumbusha wajibu wake na kwamba itafanya hivyo baada ya kukusanya taarifa''''' Mwisho wa Kunuukuu kutoka ''Mwananchi , Jumatano , Septemba , 18 ,2013''
Baada ya kusoma habari hii ndio ninapopata shida na uwezo wa Nape.....Na pia nashangaa baadhi ya wachangiaji humu JF waliokuwa wanawapiga vijembe wote waliokosoa jambo hili! Shame on Them!!!
 
Ukipewa uongozi wa juu wa magamba lazima upitishwe MIREMBE kwa siri ili uendane na mfumo wa kujitoa ufahamu wako wa asili..NAPE NI KAMA KIBUYU.
 
Tujikumbushe kauli ya Nape:

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimesikitishwa na hatua ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumshutumu Balozi wa China, Dk. . Lu Youqing kwa kuhudhuria mikutano ya CCM.

Kimewataka watanzania kupuuza madai ya Chadema kikisema hayana msingi kwa maendeleo ya taifa na watu wake.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu.

Alisema ni wazi Chadema kinataka kutumia matatizo ya wananchi kuyageuza agenda ya siasa.

Chadema haina budi itambue kuwa chama tawala cha China (CPC) kimekuwa na urafiki wa muda mrefu na CCM ikizingatia Balozi Dk. Lu pia ni kiongozi wa chama hicho.

Nape alisema hatua ya Balozi huyo kuhudhuria mkutano huo ni mafanikio ya ziara ya iliyofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana China mapema mwaka huu.

“Balozi Dk. Lu amekuja kuleta ukombozi kwa watanzania hasa wa Kanda ya Ziwa kwa kuleta wawekezaji katika Mkoa wa Shinyanga kwa kujenga viwanda wa nyuzi, pamba, nyama, maji na ngozi ambako ajira zaidi ya 1000 zitapatikana.

“Watanzania wapuuze madai haya kwani si dhambi kwa Balozi wa China kuhudhuria mkutano wa CCM… urafiki wetu hakuanza leo ni wa muda mrefu katika historia ya nchi hizi mbili tangu na baada ya Uhuru,” alisema Nape.

Nape alisema CCM imepitaka kila eneo la yakiwamo majimbo yanayoongozwa na wapinzani na kubaini kuwapo changamoto nyingi.

Aliitaka Chadema kwenda kutatua haraka matatizo hayo badala ya kufanya mikutano Dar es Salaam pekee.
 
Kumjadili napenda ni kupoteza muda bila sababu na kumpa promo asiyostahili!! Shida ipo kwa aliyemteuwa kwenye huo wadhifa huwa najiuliza jamaa yuko sawasawa kweli huko upstairs???
Hata baada ya madudu yote ya nape bado yupo tu kwenye wadhifa, hakika ccm wanachimba kaburi lao kwa mikono yao wenyewe
 
nape hana akili yule,tokea lini baloz akafanya kazi za siasa badala za kidiplomasia?hata km ni mwanachama wa chama tawala cha china lkn hapa anawakilisha nchi instead of chinese ruling party:yell:
 
Last edited by a moderator:
Atakuja NAPE hapa atasema "serikali inafanya upotoshaji, inataka kugeuza matatizo ya wananchi kama ajenda ya kisiasa" afu anaweza akaipa serikali siku saba iwe imefuta kauli yake. Kwani anashindwa yule..! Akija na Mwigulu nae ataweka yake, baadae watamalizia thatha Lizaboni chama, Ritz HAMY-D rais mpya , kati kati , Mtela Mwampamba , ZeMarcopolo masopakyindi faiza foxy Rejao, WABHEJASANA, Mamndenyi na wengineo kufunga kazi na kupigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la serikali.
Haya ni maoni yangu ya kwanza kabisa juu ya sakata la balozi wa China kuingia katika mpango wa buku saba.
Simlaumu balozi huyo maana ameingizwa mkenge na wajuaji ndani ya Lumumba, kitu ambacho hata wao inaelekea walikuwa wamepitiwa.
Balozi yeyote kuchangia katika local politics ni makosa.
 
Hiyo barua alimwe na Serikali ya Magamba ambayo humpangiaga Speaker namna ya kuendesha Bunge!!!!!!!???????
 
Atakuja NAPE hapa atasema "serikali inafanya upotoshaji, inataka kugeuza matatizo ya wananchi kama ajenda ya kisiasa" afu anaweza akaipa serikali siku saba iwe imefuta kauli yake. Kwani anashindwa yule..! Akija na Mwigulu nae ataweka yake, baadae watamalizia thatha Lizaboni chama, Ritz HAMY-D rais mpya , kati kati , Mtela Mwampamba , ZeMarcopolo masopakyindi faiza foxy Rejao, WABHEJASANA, Mamndenyi na wengineo kufunga kazi na kupigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la serikali.

kweli kabisa Nape Nnauye lazima awape siku 10 serikali kubatilisha hiyo barua.
 
Last edited by a moderator:
Haya ni maoni yangu ya kwanza kabisa juu ya sakata la balozi wa China kuingia katika mpango wa buku saba.
Simlaumu balozi huyo maana ameingizwa mkenge na wajuaji ndani ya Lumumba, kitu ambacho hata wao inaelekea walikuwa wamepitiwa.
Balozi yeyote kuchangia katika local politics ni makosa.

Nakushukuru kwa kuwa objective na kuuona ukweli..
 
Back
Top Bottom