Serikali kulipa madai ya Watumishi wa Umma, yatalipwa February pamoja na mshahara! Soma hapa majina..

Wengine tumeongezewa 5000 mkuu sawa na wastani wa166.66 kwa siku ...sasa hii jiti unayomuongezea MTU mzima kwa kusema gharam za maisha zimepanda ni akili au matope kama sio bhange au pombe

Kabla ya 2015 tulikuwa tunaomba tupate Rais Mwenye Maamuzi magumu au sahihi?
 
SERIKALI IJITAHIDI KUWAPA WALIMU MOTISHA

Kalamu. Picha/MAKTABA

Na TAHARIRI YA MWANANCHI

Imepakiwa - Friday, February 9 2018 at 09:09

Kwa Mukhtasari

Hatimaye kilio cha muda mrefu cha walimu kutopandishwa vyeo kimesikika.

HATIMAYE kilio cha muda mrefu cha walimu kutopandishwa vyeo kimesikika.

Juzi, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Joseph Kakunda alisema Serikali imeshamaliza mchakato wa mapitio ya upandishaji madaraja walimu uliokuwa umesimamishwa kwa muda mrefu.

Kakunda alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalumu Susan Lyimo (Chadema), aliyetaka kujua hatima ya mchakato wa kupandisha walimu madaraja aliosema umekwama kwa siku nyingi.

Walimu pamoja na mambo mengine wamekuwa wakilalamika kuhusu kusitishwa upandishwaji wa madaraja jambo ambalo kwa wengi lilikuwa ikiwavunja moyo wa uwajibikaji.

Hii bila shaka ni habari njema kwa walimu ambao siyo tu kwamba watapumua kwa kupandishwa madaraja lakini pia Serikali imeeleza kuwa walimu hao watapandishwa madaraja kwa mserereko ili kusiwepo urukwaji wa madaraja kwa wahusika. Tunapongeza hatua hiyo ya Serikali kwa kuwa inaleta faraja kwa walimu ambao sasa tunaamini kuwa siyo tu watafarijika lakini pia hatua hiyo ni motisha kwao ya kuwajibika zaidi.

Pamoja na usemi kuwa ualimu ni wito lakini kiukweli moyo wa uwajibikaji kwa walimu hukua zaidi pale mwajiri wao anapowathamini ikiwamo kuwapandisha madaraja.

Tafiti na uzoefu vimeonyesha kuwa walimu wakipewa motisha kwa namna mbalimbli, ari yao ya kufundisha huongezeka na hivyo kuleta matokeo chanya katika ufundishaji na ujifunzaji shuleni.

Mathalan repoti ya utafiti wa kujifunza iliyotolewa na Shirika la Twaweza mwishoni mwa mwaka 2017 ilionyesha kuwa asilimia 91 ya walimu waliohojiwa walikiri kuwa motisha kwao inachochea kiu ya kufundisha na mwishowe kufaulisha wanafunzi.

Tunaamini upandishaji wa madaraja ni mfano mmoja wa aina za motisha ambazo Serikali inapaswa kutoa kwa walimu tena mara kwa mara.

Serikali ikiwa mwajiri wa walimu haina budi kukumbuka kuwa kusitisha upandishaji wa madaraja, na kulimbikiza stahili zao ni vichocheo vya kukwaza jitihada za walimu ambao kimsingi hapa nchini bado wanafanyakzi katika mazingira magumu. Serikali inaweza kukwama kuwajengea walimu nyumba, ikashindwa kuwaendeleza kielimu lakini inapojihimu kuwapandisha madaraja na kuwalipa stahili zao kunawapa walimu ari ya kuwajibika.

Hatuna budi kukubali kuwa kiuhalisia katika shule nyingi, uwajibikaji wa walimu sio wa kuridhisha na ndio kwa kiwango kikubwa unachangia kuporomoka kwa kiwango ha kujifunza na mwishowe elimu yetu kwa jumla.

Tunaishauri Serikali kuwa hatua hii ya kupandisha madaraja iwe mwanzo wa kuzifanyia kazi kero mbalimbali zinazowasibu walimu nchi nzima.

Inatia moyo kwa mfano kuona Serikali ikilipa malimbikizo ya walimu ambapo hadi Juni 2017 Waziri Kakunda alisema Serikali ilishalipa 14,236 bilioni kati ya TSh69,461 bilioni ambazo walimu walikuwa wakiidai Serikali hadi kufikia mwaka 2015/16.

Hata hivyo, Serikali isiishie kulipa malimbikizo au kupandishwa madaraja pekee. Ni lazima iendelee kuwatazama walimu kwa jicho la karibu kama kada muhimu ya utumishi wa umma na mhimili wa maendeleo ya Taifa letu.

Tahariri ya Mwananchi,
 
Kutoka Bungeni Leo:

Waziri wa fedha na Mipango Dr.Philip Mpango amesema Serikali italipa madeni inayodaiwa ya Zaidi ya shilingi bilioni 43 ambazo imezihakiki na kuona kuwa ni madeni halali ambayo wanadaiwa kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2017 na watumishi wa umma wakiwemo Walimu.

Waziri Mpango amesema fedha hizo zitalipwa kwa mkupuo na watumishi watakaolipwa madai hayo ni elfu ishirini na saba mia tatu themanini na tisa na yatalipwa sambamba na mishahara ya mwezi huu wa pili.

Waziri Mpango amesema awali watumishi elfu themanini na mbili mia moja kumi na moja waliwasilisha madai ya shilingi bilioni mia moja na ishirini na saba ,milioni mia sita na tano laki moja na ishirini na nane,mia nane na sabini na mbili na senti themanini na moja.

Kwa mujibu wa Waziri Mpango,Serikaki imeokoa shilingi bilioni themanini na nne na milioni mia mbili na laki mbili kufuatia uhakiki huo ambazo ni sawa na asilimia 66 ya madai yote yaliyokuwa yamewasilishwa awali.

Malipo ya madai haya ambayo mengine yana zaidi ya miaka 10, majina ya walipwaji yatatangazwa kwenye magazeti kuanzia kesho tarehe 10 Februari
 
Sawa
 
Zile Promotion elf 59 mpaka Sasa wameishiwa kupewa makaratasi ya kupandishwa vyeo, Mshahara umeomgezwa elf 10 tu Kama annual increament sio ingezeko la Promotion

Hahahahaha , usiponyooka awamu ya tano hunyooki mpaka unakufa
Ila hii awamu mimi imenipa akili sana badala ya kutegemea mshahara tu imetupa elimu ya kujiongeza kutafuta vyanzo vingine na pia imetuondolea hofu ya kuogopa kuacha kazi.Kazi ni dhamana ya kukopea tu then unaingia kitaani kupambana unafanya kazi ya serikali kwa muda 10% na 90% unafanya mishe zako huku ukisubilia mshahara wa bure
 
Miaka saba tangu nifanye kazi halmashauri sijawahi kulipwa pesa ya likizo wala kupata promotion.Na huenda hadi serikali hii imalize muda wake wa miaka 14 ndipo nitapata promotion na labda pesa ya likizo.Hata hivyo namtumaini Mungu,ipo siku yangu tu
 
Hahahahaha
Tamko rasmi limeshatoka, mfuatilie Msemaji wa Serikal kishatangaza rasmi kuwa mnofu wa 50 M ndo tunautafuna kwny Elimu bure tusiulizane Tena
Pohamba ni wewe kweli mkuu!!. Mbona kama unaikejeli serikali yetu?
 
Hawa watu hawafai kuwaamini....kama jana wamesema washatoa milioni 50 kila kijiji kwa kujenga flyover....nafkir hizo pesa watasema wamewalipa watumishi wa umma kwa kununua bombardier
 
Back
Top Bottom