Serikali kulipa madai ya Watumishi wa Umma, yatalipwa February pamoja na mshahara! Soma hapa majina..

Naona majina yametoka ila taasisi nyingi hazimo.
 

Attachments

  • ORODHA YA MAJINA YA WATUMISHI WA UMMA WANAOSTAHILI KULIPWA MADAI YA MALIMBIKIZO.pdf
    3.3 MB · Views: 370
Wangetoa majina yote ya wanaodai na waseme ni vigezo gani vimechukuliwa kubatilisha deni la mtu. Maana naona wananyakua nyakua tu, case moja ila mwenzangu analipwa mi naachwa.
 
Haya mambo ya kuandika majina kwenye magazeti ni kudhalilishana!
Mbona wenyewe wanapolipana huko bungeni huwa hawaandiki majina kwenye magazeti?
Majina yangetumwa kwa wakurugenzi wa halmashauri tu na wahusika wangeyaona huko! Sasa sijui wataorodhesha majina na kiasi anachopata MTU? Hii ni kuwachonganisha watumishi na ndugu zao na jamii kwa ujumla!
 
Duh nimeona Orodha ya Wilaya moja ya Mkoa wa Mbeya wanaistahili kulipwa wapo 18 tu, utata mtupu hapo
 
Orodha ya majina inaonesha ni malimbikizo ya mishahara , ni Vipi kuhusu madai mengine Kama Likizo,uhamisho,posho ya kujikimu n.k? AMA nayo itakuwa na orodha inayojitegemea au ndiyo mambo ya Viwonder!!!!!
 
Naona kuna madai halali yamefanywa kuwa madai yasiyo halali...

Watoe na majina ya waliokuwa wanaidai serikali ila hawatalipwa. Na serikali ieleze ni kwa sababu gani kila mmoja wa waliokuwa wanaidai hapaswi kulipwa.

Vinginevyo tunaoidai serikali bado tupo.
Mkuu nimeona jina lako namba

9979

Likarudiwa tena kwenye namba

9980.
 
Takriban kila mdai atapata milioni moja na laki tano! Ingependeza kama wangelipa na riba maana zechelewa sana kulipwa na thamani yake halisi imeshuka. Mwaka 2005 milioni moja na nusu ingefanya mambo mengi, lakini Leo hiyo ni pesa ya mboga tu!!!
 
Orodha ya majina inaonesha ni malimbikizo ya mishahara , ni Vipi kuhusu madai mengine Kama Likizo,uhamisho,posho ya kujikimu n.k? AMA nayo itakuwa na orodha inayojitegemea au ndiyo mambo ya Viwonder!!!!!
Safari bado ni ndefu sana aisee
 
Mkilipwa basi Bomba zitatoa maziwa Nchi nzima. Huu sio wakat wa kuwaamini hawa Wapiga Ramuli wa g....t
 
Back
Top Bottom