Serikali kulipa madai ya Watumishi wa Umma, yatalipwa February pamoja na mshahara! Soma hapa majina..

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Waziri wa fedha na Mipango Dr.Philip Mpango amesema Serikali italipa madeni inayodaiwa ya Zaidi ya shilingi bilioni 43 ambazo imezihakiki na kuona kuwa ni madeni halali ambayo wanadaiwa kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2017 na watumishi wa umma wakiwemo Walimu.

Waziri Mpango amesema fedha hizo zitalipwa kwa mkupuo na watumishi watakaolipwa madai hayo ni elfu ishirini na saba mia tatu themanini na tisa na yatalipwa sambamba na mishahara ya mwezi huu wa pili.

Waziri Mpango amesema awali watumishi elfu themanini na mbili mia moja kumi na moja waliwasilisha madai ya shilingi bilioni mia moja na ishirini na saba ,milioni mia sita na tano laki moja na ishirini na nane,mia nane na sabini na mbili na senti themanini na moja.

Kwa mujibu wa Waziri Mpango,Serikaki imeokoa shilingi bilioni themanini na nne na milioni mia mbili na laki mbili kufuatia uhakiki huo ambazo ni sawa na asilimia 66 ya madai yote yaliyokuwa yamewasilishwa awali.

Malipo ya madai haya ambayo mengine yana zaidi ya miaka 10, majina ya walipwaji yatatangazwa kwenye magazeti kuanzia kesho tarehe 10 Februari
===========================

Serikali kupitia mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara (Human Capital Management Information System – HCMIS) kufikia tarehe 01 Julai 2017 ilikuwa na madai ya malimbikizo ya mishahara yenye jumla ya shilingi 127,605,128,872.81 kwa watumishi 82,111 Wakiwemo walimu 53,925 waliokuwa wanadai shilingi 53,940,514,677.23 sawa na asilimia 42.27 ya madai yote, na wasiokuwa walimu 28,186 waliokuwa wanadai jumla ya shilingi 73,664,614,195.58 sawa na asilimia 57.73 ya madai yote. Madai haya yalikuwa ya muda mrefu mengine yakiwa ya kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2017

Madai haya yalijumuisha mishahara isiyolipwa, tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu na nyongeza za mishahara zilizotokana na kupandishwa vyeo na kuchelewa kurekebishiwa mishahara.

MATOKEO YA UHAKIKI WA MADAI YA SHILINGI BILIONI 127,605,128,872.81 KWA WATUMISHI 82,111
  • Madai ya watumishi 27,389 kati 82,111 yenye jumla ya shilingi 43,393,976,807.23 ikiwa ni asilimia 34 ya madai yote ya shilingi bilioni 127,605,128,872.81 yaliyohakikiwa yameonekana ni sahihi na yanastahili kulipwa bila marekebisho.
  • Madai yanayostahili kulipwa yanajumuisha shilingi bilioni 16.25 kwa walimu 15,919 na shilingi bilioni 27.15 kwa watumishi wasiokuwa walimu 11,470
  • Madai yote yaliyoonekana kuwa sahihi ya shilingi bilioni 43.39 yatalipwa pamoja na mshahara wa mwezi Februari 2018 kwa mkupuo mmoja. Malipo ya Madai haya ambayo mengine yana zaidi ya miaka kumi majina ya walipwaji wote yatatangazwa kwenye magazeti kuanzia kesho tarehe 10 Februari, 2018.
Kwa matokeo hayo ya uhakiki, mazoezi yaliyofanyika likiwemo zoezi la kuwaondoa kwenye Mfumo wa malipo ya mshahara (“payroll”) watumishi hewa, vyeti feki na wasio kuwa na sifa na uhakiki wa madai ya malimbikizo ya mishahara uliofanyika limeweza kuokoa jumla ya shilingi bilioni 84.22 ambazo ni sawa na asilimia 66 ya madai yote ya malimbikizo ya awali ya shilingi bilioni 127.61 yaliyokuwa kwenye mfumo ambazo bila zoezi la uhakiki kufanyika zingelipwa wakati zilikuwa hazistahili kulipwa.
Serikali itaendelea kulipa madai ya watumishi kadiri yanavyojitokeza ili kuondokana na malimbikizo ya aina hii ambayo yanaweza kuisababishia Serikali hasara kwa kulipa madai yasiyostahili.

Fungua kiambatanisho au bonyeza HAPA Kupata Majina ya Watumishi wa Umma kwa kundi la kwanza wnaostahili Kulipwa Madai ya Malimbikizo ya Mishahara
 
Attachments

  • ORODHA YA MAJINA.pdf
    3.3 MB · Views: 598
Kutoka Bungeni Leo:

Waziri wa Fedha na Mipango, Philip I. Mpango amesema Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni 43.39 kitalipwa. Awali deni hilo lilikuwa shilingi bilioni 127.6.

Kiasi hicho ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu. Madai hayo yanayostahili kulipwa yanajumuisha madai ya Walimu 15,919.
Mbona ni walimu tuu...???
Au Manesi na Madaktari hawatalipwa madai yao...???
 
Kutoka Bungeni Leo:

Waziri wa Fedha na Mipango, Philip I. Mpango amesema Serikali imesema imekamilisha uhakiki wa madai ya Watumishi wa Umma na kwamba kiasi cha shilingi Bilioni 43.39 kitalipwa. Awali deni hilo lilikuwa shilingi bilioni 127.6.

Kiasi hicho ambacho ni madai halali kitalipwa kwa mkupuo pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu. Madai hayo yanayostahili kulipwa yanajumuisha madai ya Walimu 15,919.
Naona tu jinsi dereva na videreva wanavobadilisha gia bila crachi mara utaona indiketa inawashwa bila sababu

Nasubiri mwingine apige honi tujue kama na yeye yupo.
Na mafuta ndo yanayoyoma, abiria kazi tunayo tutafika Kwelii???
 
  • Magufuli atoa bilioni 200 kulipa madeni ya wafanyakazi na watoa huduma_144p.3gp
    1.4 MB · Views: 55
Naona tu jinsi dereva na videreva wanavobadilisha gia bila crachi mara utaona indiketa inawashwa bila sababu

Nasubiri mwingine apige honi tujue kama na yeye yupo.
Na mafuta ndo yanayoyoma, abiria kazi tunayo tutafika Kwelii???

Zile Promotion elf 59 mpaka Sasa wameishiwa kupewa makaratasi ya kupandishwa vyeo, Mshahara umeomgezwa elf 10 tu Kama annual increament sio ingezeko la Promotion

Hahahahaha , usiponyooka awamu ya tano hunyooki mpaka unakufa
 
Kwann ananza na walimu wenzanke..??Kwani sisi Madaktari na Manesi hatuna haki ya kulipwa stahiki zetu ikiwamo Malimbikizo ya mishahara,Kupanda madaraja baada kuongeza elimu,Allowance baada ya kwenda kutoa tiba sehemu zisizo na huduma..??????
Charity begin at home na Mzee anaujua huu usemi

Malimbikizo anaanza kwa Walimu wenzake
Vyeo kwa Wasukuma na Wakristo wenzake
 
Back
Top Bottom