Serikali kulalamika ni dalili za kushindwa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kulalamika ni dalili za kushindwa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Mar 17, 2011.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Katika maisha siku zote yule anaye lalamika ni yule ambae kakata tamaa. Ni dalili kwamba mtu kakabiliwa na matatizo sasa hajui cha kufanya basi anaishia kulalamika. We chunguza tu na uta gundua siku zote mtu anaye lalamika ni mtu ambae hawezi na kashindwa kutatua matatizo yake.

  Sasa pale serikali inapo anza kulalamika ina leta picha gani? Ukiwa mtoto kwenye nyumba baba akianza kulalamika ina leta picha gani? Kama serikali ime fika hatua ina lalamikia matatizo basi ni dalili kwamba imeshindwa kuya tatua. Kwa maana maneno ni dalili ya kushindwa vitendo.

  Ninacho ishauri serikali ni kwamba iangalie sana picha inayo wapa wananchi. Siku zote raisi aki lalamika basi ana onekana ni mnyonge na mnyonge hata siku moja hawezi kabiliana na matatizo kama ya Tanzania.

  Chadema si tatizo. Hata kidogo! Kwa maana mume uki kamatwa nje ya ndoa mtu akaenda kumuambia mkeo usimlalamikie alioenda kusema kwa maana bila matendo yako basi huyo mtu asinge kuwa na la kusema. Mheshimiwa raisi bila sukari kupanda bei, bila nauli kupanda bei, bila gharama za maisha kupanda bei basi upinzani isinge kua na cha kusema. Kwa hiyo usi walalamike wale wanao enda kwa wananchi kuwaambia. Jiangalieni nyie na matendo yenu.

  Kama mwananchi naombea serikali ifanikiwe iwe ya CCM au chama chochote. Kwa maana serikali kushindwa ni hasara kwa wanancho wote pasipo kuangalia dini wala kabila. Kwa mantiki hiyo basi ilimradi Mh. JK ndiyo raisi na CCM ndiyo inaongoza serikali basi nawa takia mafanikio na nawaombea kwa Mungu. HUKUMU 2015!
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Serikali inapaswa kuonekana inawajibika na kutatua matatizo yanayowakera wananchi wake. Kama Kikwete alidhani awamu yake ya pili itakuwa kama awamu yake ya kwanza basi hapo ana "rude awakening." Huwezi kulalamika kama wewe umepewa usukani wa kuendesha nchi. Achukue somo kwa mwenzake Obama ambaye hajawahi kulalamika lakini anapambana kwa uwezo wake wote na matatizo aliyoyarithi alipoingia mamlakani hapa Marekani. Huo ndio tunaouita uongozi.
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu Jasusi,

  Ni kweli mkuu. Nilipo muona mheshimiwa ana lalamika tena mbele za kamera I was very disappointed. Tena kutoka kwa mtu aliye kuwa mwanajeshi. Kiongozi hata siku moja hapaswi kulalamika in public. Kama binadamu natambua ana stress lakini hizo stress azitolee kwenye faragha lakini si mbele ya wananchi wake.

  Ila kati ya hii ya juzi ya JK na ile ya Pinda kulia bungeni nisha anza kuona kwamba viongozi wetu wapo weak sana. Yani kila kitu Tanzania kipo reverse. Viongozi ni mabosi wa wananchi badala ya watumishi. Viongozi wanalia lia wakati wananchi ndiyo wana pambana na hali ngumu ya maisha. Etc.

  Tanzania ni lini tuta pata kiongozi wa kweli?
   
 4. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 652
  Trophy Points: 280
  Obama always complains about so many things...like on march 12th he said he wish he was Hu Juntao! cos nobody complains about him!..presidents are just people and they always complain about issues that bother them,I know you guys like Chadema but they always complain about food prices like they were brought about by the president,c'mon! grow up! POLICIES ARE MADE BY BUNGE WHILE THE EXECUTIVE BRANCH(SERIKALI) EXECUTES THOSE POLICIES!! Think about that,then talk!
   
 5. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Uongozi si kutegemea huruma ya unaowaongoza. Kiongozi na safu yako unatakiwa kutoa muongoyo/maelezo yanayoeleweka pale panapotokea matatizo yanayowagusa wananchi. Kiongozi unatakiwa uwe safi kimatendo/kiuendeshaji na uwe mstari wa mbele kukemea na kuwawajibisha viongozi wanaokusaidia/watendaji wako pale wanapokwenda kinyume. Pale panapotokea malalamiko juu ya watendaji wako (tena wa karibu), ni vema kumuwajibisha maramoja ama kama malalamiko si za kweli basi shurutisha kupatikana kwa ukweli utakaowaridhisha wananchi unaowaongoza. Mbona kipindi cha Nyerere hali ilikuwa mbaya lakini wengi walikuwa na imani na serikali? Kiongozi ukibaki kulalamika paisipo kutekeleza yale yanayokuhusu, ama wananchi wanayotegemea ni dhahiri hawatakuwa na imani na wewe hata kidogo. UONGOZI SI LELEMAMA.
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Tatizo siasa zimezidi mno hadi katika mambo ya msingi.
  Kiongozi anapolalamika mbele ya hadhila hii inamaanisha wananchi wamwonee huruma yeye na chama chake ili uchaguzi ujao wananchi wasiwatupe.
  Mfano swala la mfumuko wa bei na rushwa linahitaji utendaji zaidi na sio kulalama kwa wananchi ili uonekane wewe na chama chako hamuhusiki.
   
 7. M

  Mindi JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  note the highlighted. Policies made by bunge? You are not serious! The winning party forms the government to implement the election manifesto of the party. the government machinery, eg. ministries, oversee the creation of policies (e.g. Kilimo kwanza, agricultural policy, etc) the government machinery creates bills which are brought into the Bunge which may demand modifications/additions/deductions and then passes them into law. the bunge oversees the executive but does not create policies!

  On Obama, you cannot compare Obama with JK. they are two people separated by an ocean of differences. I would recommend JK to join zecomedi after his term ends. that is where he belongs and can make a true contribution. he can make policies that can at least make us laugh candidly and he can get paid for it. fair enogh?
   
 8. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Hata huko zecomedy nako hakumfai!!
   
 9. T

  Tata JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Wrong. The Bunge you are talking about is defined under article 62 of the constitution which states that the BUNGE shall have two parts namely members of parliament and the President. So in fact the President is part and parcel of our BUNGE.
   
Loading...