Serikali kukataza wenye nyumba kukusanya kodi ya miezi 6, yasema inaumiza wengi

15% ya loan board iliongezeka kutoka 8% kimasihara masihara hivi hivi, hata hili litapita tu
 
mimi ukinilipa kodi yangu miezi sita au mmoja mie poa tu mradi ikifika mda wa kunilipa usinizengue manake hatutaelewana kabisa
 
Pumbavu tuu
Wangejua na adha ya wapangaji kuhusu ulipaji wa kodi nadhani wangejiuliza mara mbili. Zamani hakukua na miezi sita wala mwaka lakii adha ilipozidi wenye nyumba wakaamua hivyo. Wana huruma na wapangaji washushe bei nyumba zao watu wapate kumudu. Leo kaulize bei ya nyumba ya NHC uone cha moto.
 
Kukataza tu si dawa, wa inject hela kwenye shilika la nyumba ili ziwe nyingi tatizo litaisha natural death vinginevyo ni kutafuka kiki.
 
[/QUOTE]
Utalipa tu kodi ya miezi sita, mwenye nyumba hatakataa. Sheria hii itakuwepo kukutetea wewe pale utakapokuwa huna uwezo wa kulipa zaidi ya mwezi mmoja na mwenye nyumba akakulazimisha. Bila shaka haitatekelezeka pale mwenye nyumba na mpangaji wamekubaliana, hata kama itakuwa ni kwa miaka kumi, isipokuwa pale mpangaji atakaposhindwa ndipo atashitaki na sheria itachukua mkondo wake...
 
Utalipa tu kodi ya miezi sita, mwenye nyumba hatakataa. Sheria hii itakuwepo kukutetea wewe pale utakapokuwa huna uwezo wa kulipa zaidi ya mwezi mmoja na mwenye nyumba akakulazimisha. Bila shaka haitatekelezeka pale mwenye nyumba na mpangaji wamekubaliana, hata kama itakuwa ni kwa miaka kumi, isipokuwa pale mpangaji atakaposhindwa ndipo atashitaki na sheria itachukua mkondo wake...[/QUOTE]
Ndio hivyo hapo serikali imelenga wale wasio na uwezo wa kulipa miezi sita kwa mkupuo ila uwezo wao ni kulipa kwa kila mwezi.
 
HABARI,
Mimi binafsi nakubaliana na serikali kuanzisha mamlaka hiyo ila sikubaliani na mpango wa kuwapangia watu jinsi ya utaratibu wa muda wa kulipia kod,Mamlaka hiyo ni muhimu ili kuwasajili wapangishaji wote ili kuwe na mfumo bora wa kurahisisha ulipaji wa kodi bila kukwepa ila haiwezekani kumpangia mtu utaratibu wake wa kulipa mtu ametafuta pesa kwa nguvu yake ana mamlaka ya kuweka utaratibu hata kupanga bei atakayo serikali inatakiwa kufanya kitu kimoja tu kuhakikisha inaweka mkazi 18% ya kodi inakwenda serikalini hilo tu.Najua kuna watu watashangilia sana ial kama huwezi kulipa pesa ya miezi 6 au mwaka kama huna ni huna tu.Ila mpango huu unaweza kuwa msaada mkubwa kwa wafanya biashara wanaokodisha maeneo ya biashara kwani wataweza kulipa pesa ya muda mfupi ya pango huku wakitimia nyingine kuongea mtaji,
Inakuwa ngumu nikodishe nyumba yangu kwa balozi wa marekani alafu nimwambia anilipe kila mwezi hata kwake itakuwa usumbufu kama kuna watu wako tayari kulipa kwa mwaka serikali haiwezi kunilazimisha mtu anilipe kwa mwezi wakati mimi nimewekeza pesa nataka nilipwe ya mwaka nikafanye mambo mengine haiwezekani nikalazimishwa kwenye hela yangu kama serikali imenipa mkopo nikajenga nyumba yabishara na wakanipa masharti hayo sawa.

Ila pia naweza kusema yapo maeneo ambayo yanagombaniwa sana na maeneo ambayo hayagombaniwi sana kwenye upangishaji kama huna pesa huwezi kulazimisha kukaa mahali kwenye watu wenye hela laima uende kwenye daraja lako.

Na pia hiyo serikali wakipisha itakuwa ni aubu kuwaingilia watu uhuru wa biashara,Serikali ndio inayotakiwa kuwekeza kwenye nyumba za bei ndogo kwa mfano yale magorofa ya pale pale urafiki kwa wanao yajua.Serikali kama ikijemga majengo kama yale ya kutosha na wakapangisha watu kwa bei nzuri wanaweza kuweka utaratibu huo na najua ndi utaratibu ambao serikali unautumia sana kwenye nyumba zake za NHC.Lakini lazima ijue watu binafsi wamewekeza wengine wanamikopo wanataka hela ya miezi 3,6 au mwaka wakawekeze kwenye biashara zao na wateja wapo pia kuna baadhi ya wapangaji wapo wanaokubali pesa za miezi michache mpaka wengine mwezi mmoja kinachoangalia mahitaji ya serikali.Hata leo serikali akitokea mtu anataka kupanga NHC anataka kulia pesa y mwaka na mwingie anataka kulipa ya miezi 3 ni lazima wa mwaka ndiye atakaye pewa.

Naomba kushauri serikali iunde hiyo mamlaka ila isiwabane namna ya upangishaji ila iwabane wapangishaji wote walipe kodi kila mmoja pamoja na kodi za majengo nnchi nzima hizo kodi serikali iandae mpango maalumu wa ujenzi wa myumba za gorofa mbili au tatu za bei ndogo kama zile za urafikia au zaidi hapo kwa nyumba hizo wanaweza wakaruhusu wapangaji kulipa kwa mwezi mmoja ingawaje wapo wapo watakao weza kulipa zaidi ya mwezi mmoja.Pia kwa nyumba hizi zitapunguza mhitaji ya nyumba ndani ya mika michache watu binafsi nao itawalazima hata wao kufata utaratibu huo lakini sio kumlazimisha mtu binafsi jinsi ya kupanga.

USHAURI WANGU BINAFSI


LUMUMBA
Maelezo mareeefu ila hoja zako za kibinafsi. Utakuwa umeguswa kimaslahi. Ndio mabadiliko Hayo. Kenya tu hapo utaratibu Huu unaopendekezwa ndo unatumika na hakuna shida yoyote. Tatizo real estate sector yetu imekua ghafla sana bila usimamizi madhubuti, matokeo yake mpangaji hana wa kumtetea. Wamiliki huamua wanavyotaka. Muswada Huu ndio mwarobaini. Ifike mahali mpangaji awe na nafuu kwa kuamua anataka kulipa vipi.
 
Me ningefurahi sana kama serikali yetu itajenga nyumba nyingi na kuwapangisha wananchi wake tukalipa tena kwa bei nafuu kuliko huku kwa watu binafsi kila mkataba ukiisha utaambiwa na kodi imepanda yani tabu tupu
Nakubaliana na wewe 100%. Serikali bado ina wajibu mkubwa sana wa kupunguza makali ya maisha kwa kujenga nyumba za bei nafuu za kupanga. Tatizo NHC wako kibiashara sana, hawana tofauti na private sector. Hii haikubaliki.
 
Swala hapa ni kumpatia mpangaji unafuu na sio mwenye nyumba,inaonekana mkuu wewe hii imekugusa,ukifikiria vibanda vyako 73 ulivyowekeza halafu unaambiwa leo ulipwe mwezi mwezi unaona hailipi kabisa,pole sana...

Mkuu, ni sawa mpangaji awe na haki ya kulipa kila mwezi. Sikatai hiyo suggestion, na wakiweka sheria kuhusu hiyo swala ni vizuri. Lakini pia kama mpangaji na mwenye nyumba wanaweza kuwa na makubaliano mengine hiyo pia iruhusiwe. Anyway, kodi ya mwezi mmoja na amana ya miezi mitatu nisawa na mtu akilipa kodi ya miezi mitatu au minne in advance.

Yaani mtu akilipa kila mwezi sheria inamlinda vizuri kabisa na akiamua kulipa kwa miezi sita, mwaka mmoja au miaka miwili hayo ni makubaliano binafsi kati ya hawa watu wawili. Siyo kama mpangaji hawezi kulipa kwa mwezi mmoja anafukuzwa, no, sisemi hivyo ila kuwe na flexibility kidogo.

Mkuu kuna wapangaji wengine wanapenda kulipa kwa miezi sita, wengine hata kwa mwaka.
 
Issue hapo siyo kodi ya miezi 6 mwaka ama la issue hapo ni kuanzisha chanzo kipya cha kodi za Serikali ambayo isipoaangaliwa sawa sawa itakuwa sawa na kodi ya miamala ya fedha ambayo inamwumiza mtumiaji wa mwisho.Tutegemee kama hilo litapita tutegemee kupanda maradufu kwa kodi za pango.
.....Kwa historia ya bunge hili sitegemei hata siku moja muswaada uwe tabled halafu usipite....RIP 6.....
 
Hii sheria imechelewa sana...Nchi nyingi Duniani hakuna huu mfumo tunao tumia sasa wakulipa kodi miezi sita au zaidi...

India kwa mfano unaweka Deposit ya sawa na kodi ya miezi miwili au mitatu then unalipa kodi kila mwezi ila siku unapoamua kuondoka baba mwenye nyumba anakata 10% ya ile hela ya Deposit kama gharama za uchakavu wa nyumba then kiasi kinachobaki anakurudishia unaenda na hamsini zako....!!!
 
Ikishatungwa sheria hutokuwa na budi bali kuifata tu. Kwa hali hii miezi 6 ni kuumiza watu
.....Sheria ya kutoa na kupokea rushwa ilitungwa lini vile??? Je rushwa imeisha? Strangely law enforcers (traffic, police, mahakimu etc) ndiyo vinara wa rushwa....
 
Wenye nyumba (ukiacha NHC) hawana monopoly yoyote. Ni soko lenye ushindani wa kawaida tu. Sioni haja ya kuanza kutungia sheria mambo ambayo yanapaswa kuwa contractual terms.

Actually, wakilazimisha mwezi kwa mwezi, inaweza kuongeza bei kwa sababu wenye nyumba watataka ku factor in non-payment risks!
 
Back
Top Bottom