The Burning Spear
JF-Expert Member
- Dec 23, 2011
- 8,551
- 20,346
Habari ndiyo hiyo.
Ile akili iliyotaka kujenga bandari Bagamoyo imetuma tena ujenzi bandari Kizimkazi.
Lengo na nia ni kujiimarisha kiuchumi kwa watawala. Watoto wa Nyerere na Magufuli nadhani wanawalaumu sana wazazi wao.
===
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kukamilisha taratibu za kukamilisha michoro ya ujenzi wa Bandari ya Kizimkazi ambayo inatajwa kupunguza muda wa Kukaa Baharini kwenye Safari za Dar es salaam na Zanzibar.
Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Zanzibar Akif Ally amesema Bandari hiyo itakua ni kwa shuguli zote, Mizigo, abiria na mambo ya biashara ambapo ujenzi wa Bandari hiyo kunatajwa kufungua Mkoa huo kibiashara na Bandari hiyo kua kama daraja kwa wanaofanya kazi Dsm na Znz
Pamoja na mambo mengine Mkurugenzi wa Shirika hilo ameyazungumzia mafanikio ya Bandari ya Malindi baada ya Bandari hiyo kupewa Muwekezaji wa Kifaransa kuiendesha vilevile amesema Shirika Hilo lilikua likikusanya Bilioni 27 na kwa sasa limeongeza makusanyiko kwa kufikia Bilioni 33.
**
Mnamo mwaka 2023, iliripotiwa kuwa Kizimkazi inyokuwa kwa kasi, imepiga hatua kuelekea kuwa na bandari mpya, kufuatia makubaliano kati ya Serikali ya Zanzibar na Kampuni ya China Harbour Engineering Company (CHEC) kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa bandari.
Chini ya Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) yaliyosainiwa kati ya kampuni ya Kichina na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji ya Zanzibar, upembuzi yakinifu huo pia unajumuisha ujenzi wa Bandari ya Wete iliyoko kaskazini mwa Pemba.
Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za wizara, Kisauni, ambapo Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw. Shomar Omar Shomar, na Meneja Mkuu wa CHEC, Bw. Cheng Yongjian, walisaini makubaliano hayo. Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Dkt. Khalid Salum Mohamed, pamoja na viongozi wengine, walishuhudia utiaji saini wa makubaliano hayo.
Baada ya hafla ya utiaji saini, Dkt. Mohamed aliwaeleza washiriki kwamba serikali imeamua kuendeleza na kuboresha bandari zake, ikiwemo za Wete na Kizimkazi, kwa lengo la kuboresha usafiri, mawasiliano, mazingira ya biashara pamoja na kukuza uchumi wa nchi.