chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,969
Serikali imepanga kuunganisha taasisi zote zinazofanya kazi zinzazofanana ili kuendelea kubana matumizi zaidi, hayo yamesemwa na waziri Angela Kairuki alipokuwa anajibu swali la mbunge wa viti maalum Ruth Molel aliyetaka kujua serikali imeokoa kiasi gani kwa kuunganisha wizara.
Amesema serikali inafanya uchambuzi kujua taasisi zinazofanya majukumu yanayofanana na kisha kuunganishwa na wafanyakazi wake kuondolewa.
Amesema pia kama kuna idara na taasisi ambazo zitakuwa hazina majukumu ya kutosha kuhalalisha majukumu yake zitaondolewa.