#COVID19 Serikali kuandaa wiki ya uchanjaji

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Serikali inaandaa utaratibu wa wiki ya uchanjaji ambayo inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Septemba au mwanzoni mwa mwezi Oktoba.

Msigwa ameyasema hayo Jumapili Septemba 12, 2021 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya wiki.

''Serikali moja ya vitu ambayo inaviangalia kwasasa ni kuhakikisha tunakuwa na wiki ya uchanjaji. Utaratibu huu sasa unaandaliwa bila shaka mwishoni mwa mwezi wa 9 au mwanzoni mwa mwezi wa 10, tutakuwa na wiki ya uchanjaji, ambapo viongozi wa nchi nzima watashiriki kwenye wiki hivyo kuhakikisha Watanzania wengi wanapata chanjo,'' amesema Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali.

Aidha ameeleza kuwa ''Wataalam wetu wanatuambia watu ambao hawajachanjwa wakiugua Uviko-19 wanapata madhara makubwa na wengine wanapoteza maisha lakini waliochanjwa wanatibiwa na wanarudi nyumbani''.

Kuhusu mwenendo wa chanjo, Msigwa amesema, ''Tumefika asilimia kama 34 ya zile chanjo Milioni 1,054,400 zilizoletwa. Watanzania takribani laki 345,000 wameshapata chango hiyo, lakini pia Serikali inaendelea kuangali namna ya kuleta chanjo zingine ili watanzania waweze kupata chanjo''.

Chanzo: EATV
 
Waweke mpunga mezani tutaenda kuchanja, wakifanya kila kichwa Tshs 300,000 itakua poa
 
sasa watu laki 3 kwenye watu milioni zaidi ya 60 hata hamjishtukii ?

hachanjwi mtu hapa mpaka madozi yenu yata _expire mtaenda kuyatupa baharini samaki wajichanje kudadeki au muwarudishie waliyoyaleta 😀😀😀
 
Weka sheria tu, mfano hakuna kuingia ofisi yeyote ya serikali bila kuwa umepata chanjo au upime na kupima ni hela, au hakuna kuingia mpirani bila chanjo, au, au, au
Tuone kama hawatachanja
 
Kuwepo na wiki ya watu wasiochanjwa. Hii Serikali inasimama upande Mmoja. Hata watu wasiotaka kuchanjwa wana haki pia kutendewa vizuri.
Ubaghuzi ni hatar sana
 
sasa watu laki 3 kwenye watu milioni zaidi ya 60 hata hamjishtukii ?

hachanjwi mtu hapa mpaka madozi yenu yata _expire mtaenda kuyatupa baharini samaki wajichanje kudadeki au muwarudishie waliyoyaleta 😀😀😀
Mazezeta tu ndio yatachanjwa huo upuuzi.
 
Back
Top Bottom