Hawa jamaa wakiongezewa mkataba basi nitajua hii nchi ya wasengerema! Bahati nzuri tuna fursa ya kushawishi hawa jamaa wasiongezewe muda. Shime wote tutenge siku tupeleke barua zetu za kupinga kwa mkono, posta na EMS (mimi binafsi nitapeleka kwa mkono na DHL). Wanaharakati na wanasiasa mliowahi kukemea wizi huu wa mchana, hii ni nafasi yenu ya kuitisha mikutano na hata maandamano (Yuvisisimizi mnaweza kuruhusiwa na polisi) kupinga hawa mumiani kupewa nafasi nyingine ya kutuibia.
Na hapa ndo kuna kipimo cha rais wetu, hawa wezi wenye suti wakipewa tena mkataba basi tusisikie tena kelele za ufisadi. Kampuni hii imetudhalilisha kama nchi, imetuibia sana kupitia bei ya umeme ambayo haiingii akilini. Mim kama mwananchi, nipo radhi kukosa umeme kwa nyakati fulani au nyakati zote ili mradi mumiani kama IPTL na wengineo wameondoka ktk sekta ya umeme.