Serikali: Kilometa 6,000 za barabara Tanzania ni lami kati ya kilometa 86,472 za barabara zote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali: Kilometa 6,000 za barabara Tanzania ni lami kati ya kilometa 86,472 za barabara zote

Discussion in 'Major Projects in Tanzania' started by VIKWAZO, Jul 13, 2011.

 1. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  SERIKALI imesema Tanzania ina kilometa 6,318 za barabara za lami kwa nchi nzima.

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe alisema kilometa hizo za barabara za lami ni miongoni mwa kilometa 86,472 za barabara zote zilizo kwenye mtandao wa barabara nchini.

  Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM) aliyetaka kufahamu sababu za Serikali kushindwa kuweka lami barabara inayokwenda katika Wilaya ya Chamwino ambako ni nyumbani kwa Waziri Mkuu mstaafu, Samwel Malecela kama njia ya kumuenzi.

  Dk. Mwakyembe amewaeleza wabunge mjini Dodoma kuwa, Serikali imejipanga ifikapo mwaka 2017/2018 iwe imekamilisha kuunganisha makao makuu ya mikoa kwa barabara za lami na baada ya hapo itaangalia barabara nyingine.

  Akijibu swali la msingi la Lusinde, aliyetaka kufahamu lini Serikali itatengeneza barabara ya lami kutoka Dodoma mjini hadi Hospitali Teule ya Mvumi yenye kilometa 40, alisema kwa sasa Serikali haina mpango wa kuweka lami barabara hiyo.

  Alisema, Wakala wa Barabara (Tanroads) ataendelea kuifanyia matengenezo barabara ya Dodoma hadi Mvumi kwa kiwango cha changarawe ili iendelee kupitika kwa urahisi majira yote ya mwaka.
   
 2. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  malecela alitufanyia nini watanzania mpaka wilaya hiyo ipewe kipaumbele? yeye alikuwa wapi kuchochoa maendeleo?

  kwa takwimu hizi ni asilimia 7.31 tu ya barabara zote ni lami duh
  kazi ipo
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Lusinde anapigania Baba yake aenziwe!! Basi tutaenzi wengi!
   
 4. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Halafu watu wakisema kwamba baada ya miaka 50 ya uhuru maendeleo yaliyopo hayalingani na umri wa nchi, watu wa CCM wanakasirika....Ama kweli ukweli unauma!
   
 5. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  moyoni ccm wanajua wanamefanya maendeleo maana wengi ni wezi wa kuzaliwa, hiko damuni
   
Loading...