Serikali izifute Yanga na Simba

Serikali izifute Yanga na Simba

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,850
Reaction score
9,423
Timu hizi ni mzigo na hazina mipango endelevu zaidi ya kudorore soka LA Tanzania. Hizi ni timu kongwe lakini hazina hata uwanja wa mazoezi kwa miaka yote ya uwepo wao.

Hizi timu zinamiliki club. Ni aibu timu kubwa kama Azam kuwa ni tawi rasmi LA Simba.

Ndani ya vilabu vya soka kuna hujuma. Timu zinajitoa kafara kwa Simba na Yanga. Hizi timu hazina tija kwa mustakabali wa soka let.

Tunataka soka LA kisasa.
 
Hivi kumbe Simba na Yanga zinamilikiwa na serikali??

Chondechonde usije ukaiomba serikali iifunge Fyatanga bar kwa kuwa haina mipango endelevu ya kuchoma kitimoto

Serikali yenyewe imechemsha kujiongoza sioni tofauti yake na hizi timu mbili kongwe.
 
Kwa kuwa kila mmoja ana uhuru binafsi wa kuweka bandiko lake hapa acha tuendelee kuweka hata kama halina umuhimu.
 
Yani azam inamilikiwa na simba?makubwaa
 
Hivi kumbe Simba na Yanga zinamilikiwa na serikali??

Chondechonde usije ukaiomba serikali iifunge Fyatanga bar kwa kuwa haina mipango endelevu ya kuchoma kitimoto

Serikali yenyewe imechemsha kujiongoza sioni tofauti yake na hizi timu mbili kongwe.

yeye anafikiri kila kitu ni selikari, La saba wamemaliza mtiani tutachoka muno na thread zenye akili mgando.
 
kabla ya kuleta hoja hapa JF lazima uifanyie analysis ya kutosha, sio kukurupuka kurupuka tu
 
Serikali ndiye msajili wa taasisi na asasi zote za kijamii vikiwemo vilabu vya michezo ikiwemo Simba na Yanga

hoja yako haina mashiko kabisa, tumekuambia thibitisha kuwa Azam ni tawi la Simba umeshindwa, kama huna evidence huna ruksa ya kuongea, kaa kimya.
 
Hizi ni timu kongwe lakini hazina hata uwanja wa mazoezi kwa miaka yote ya uwepo wao.
Ni aibu timu kubwa kama Azam kuwa ni tawi rasmi LA Simba.
Kwa hiyo serikali ikizifuta Yanga na Simba (automatically ikalifuta na tawi lake la Azam), ni timu gani yenye uwanja wake binafsi itakayokuwapo? Nadhani uliandika kabla haujatafakari
 
kipigo cha jana bado kinawapa tabu mashabiki wa simba
 
Back
Top Bottom