masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,901
- 13,196
Hizi habari kutoka mkoani Kilimanjaro ambako watoto toka sehemu nyingine nchini wanachukua "mafunzo" ya dini , suala hili linaleta wasiwasi mkubwa.
Kwanza kabisa suala hili linafanywa kwa kificho, na pili watoto hawa ni kama wanalazimishwa kufanya hivyo.
Tatu ni mafunzo gani mema ya kidini yanayofanywa kwa kificho?
Conclusion yangu ni moja tu, preparation of suicide bombers!
Hawa watoto malaika masikini ni lazima wanafundishwa na kukaririshwa kuwa wajitayarishe kwenda peponi wakati ukiwadia.
Naomba serikali safari hii ifungue macho maana yale ya Tanga , Amboni yalianza kwa wananchi kulalamika kuwa huko kuna watu wanachukua mazoezi ya kutia shaka.
UPDATE
=====
[h=1]Watoto wengine 11 wakutwa wamefichwa
Posted Ijumaa,Marchi13 2015 saa 10:35 AM[/h]Kwa ufupi
Hii ni mara ya pili katika muda usiozidi wiki moja baada ya polisi kubaini nyumba iliyohifadhi watoto 18 kwa lengo kama hilo Jumamosi iliyopita.
Moshi. Mambo mazito zaidi yamezidi kubainika mkoani Kilimanjaro baada ya polisi kugundua nyumba nyingine yenye watoto kumi na mmoja waliokusanywa kutoka mikoa mbalimbali kwa ajili ya kufundishwa dini.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela alisema tukio hilo linafanya wapelelezi kuumiza vichwa kwa kuwa mikoa waliyotoka ndio ile ile waliyotoka watoto 18 waliokutwa kwenye nyumba moja mjini Moshi.
Nyumba hiyo imebainika wakati kukiwa na madai kwamba baadhi ya misikiti katika maeneo ya Pasua, Njoro na Kibosho yanaendesha mafunzo ya judo na karate.
Kamanda Kamwela alieleza kuwa kama ilivyokuwa awali, watoto waliobainika juzi wanatoka katika mikoa ya Tanga, Dodoma, Singida, Tabora na Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, watoto hao waligunduka katika nyumba iliyoko eneo la Lyamungo wilayani Hai. Alisema umri wao ni kati ya miaka 14 na 17 na walikuwa wanafundishwa dini na ushonaji.
Alisema kituo hicho ambacho hakijasajiliwa, kinaitwa Umm Sukhail na kinamilikiwa na mwalimu mstaafu, Abubakar Juma (64) mkazi wa Tanga ambaye kwa sasa anaishi maeneo ya Kibosho Mweka.
Kamwela alisema watoto hao wamechukuliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi ili kujua sababu za wao kuishi katika eneo hilo pia kubaini ukweli wa mafunzo yanayotolewa kwenye kituo hicho.
"Kutokana na kugundulika kwa mafunzo haya yasiyo rasmi yanayotolewa na walimu ambao pia si rasmi, lazima tuchunguze kama baada ya kuhitimu wanapewa vyeti na wanafanya kazi wapi," alisema.
Kamwela pia alisema polisi wanafanya uchunguzi ili kubaini kama watoto hao walipata elimu ya msingi kama sheria inavyoelekeza na kama walifaulu ama la na kwanini hawakuendelea na masomo. Kamanda alisema upo uwezekano wa watoto 18 waliokutwa Pasua kuhamishiwa kituo cha Narumu na kwamba jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kubaini kama wenye vituo hivyo wanafanya kazi pamoja.
Kuhusu watoto 18 wa Pasua, Kamanda Kamwela alisema wametambuliwa na wazazi wao na kuchukuliwa, lakini bado uchunguzi unaendelea kujua uhusiano wao na mmiliki wa nyumba hiyo.
"Tunachunguza kujua kama wazazi walikuwa wakifahamu maisha wanayoishi na sababu za kuwatoa kwenye shule za Serikali na kuwapeleka kwenye shule za dini wakati elimu ya msingi ni ya lazima," alisema.
Gazeti : Mwanananchi 14/3/2015
UPDATE
=====
BAKWATA: Hatuvitambui vituo vinavyohifadhi watoto
Baraza la Waislamu (BAKWATA) mkoani Kilimanjaro limesema halivitambui vituo viwili vilivyogundulika hivi karibuni katika maeneo ya Pasua na Kibosho ambavyo vinatumika kuhifadhi watoto na kwamba kinachofanyika katika vituo hivyo kina lengo la kuichafua dini.
Kauli hiyo ya Bakwata inakuja siku moja baada ya kugundulika kwa kituo kingine katika eneo la Lyamungo, wilayani Hai kikiwa na wasichana 11 wenye umri kati ya miaka 14 na 17 na kufanya idadi ya watoto hao kufika 28.
Katibu wa Bakwata mkoani hapa Rashid Mallya , aliliambia TZDaima kuwa hawavitambui viyuo hivyo kwa kuwa wana maeneo maalum ya kufundishia dini na si katika nyumba za watu binafsi.
"Maeneo ya kufundishia dini yetu yana julikanana si nyumbani kwa mtu, madrasa zetuzinapatikana mahala panapofahamika, ziko misikitini na zina utaratibu wake kama hazipo misikitini ziko katika maeneo tunayoyatambua" alisema Mallya.
TzDaimaMachi 14 , 2015, pg 3