Serikali iwatupie jicho kali BASATA

Serikali iwatupie jicho kali BASATA

Joined
Apr 27, 2006
Posts
26,584
Reaction score
10,464
- Well, nilidhani BASATA inatakiwa kuinua Vipaji vya Wasanii na kuvikuza vipande juu zaidi lakini wanachokifanya sasa hivi sio kabisa ni wakati muafaka wa Serikali kuwatupia jicho kali na kuwarekebisha sasa na mapema kabla hawajafika mbali na kuvuruga sanaa nchini, kwa mfano:-

1. MISS TANZANIA:- BASATA wameifungia Miss Tanzania kwa sababu ambazo kama ni kweli zipo zinawahusu tu Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania lakini haziwahusu Vijana wadogo wa kike ambao hawana kosa lolote, sasa BASATA wameifungia Miaka Miwili nia na madhumuni ni nini hasa? Kuwakomoa Viongozi au Wasichana? Halafu Taifa linafaidikaje na kuwafungia Vijana wadogo kufanya mashindano ambayo kabla hayajafungiwa yamewaletea mafanikio makubwa kimaisha baadhi ya washiriki, Wasichana kama Hoyce Temu, sasa hivi ni Balozi wa Umoja wa Mataifa na pia ni mfanya biashara mkubwa anayemiliki Club maarufu ya 327 hapa mjini wala sio siri haya mafanikio yake kimaisha yametokana na kushinda kwake haya mashindano, wapo wengi kama Miriam Odemba ambaye sasa anaishi Paris, France anakofanyia kazi zake za Modelling na yeye alitokea kwenye haya haya mashindano, Millene Magese, Faraja Kota, Klyn, I mean I can go on and on wote wametokea kwenye haya mashindano.

- Majuzi Msichana mdogo Doris Mollel amefungua Foundation ya kusaidia watoto premature, uzinduzi umefanyika Kempisk Hotel na alichangiwa karibu Shillingi Millioni 100 now huyu msichana amepitia mashindano haya haya mwaka jana tu, I mean leo kuna wasichana wengi sana ambao walikuwa wanasubiri na wao wapate nafasi ya kushiriki haya mashindano na wao watimize ndoto zao, ni kawaida ya mataifa yote huru Duniani kuwaruhusu wananchi wake kutumia all available resources kujisongeza mbele kimasha, sasa kwa kuwafungia miaka 2 exactly BASATA wana accomplish what?

2. TUZO ZA WATU:- Majuzi BASATA wamesimamia hizi tuzo ambazo matokeo yake yalikuwa ni maajabu ya Dunia, kwenye TUZO zote Duniani za WAsanii hata zikiwepo kura bado lazima kuwepo na vigezo vingine, kwa mfano kura zinatakiwa kushika kama 30% 50% Ubora wa kazi za Msanii 20% ni kukubalika kwa Msanii ndani na nje ya Nchi, lakini haiwezekani ukahukumu kazi za Msanii kwa kutumia kura 100% that is the biggest joke of my life, I m,ean kuna makosa mengi sana yamefanyika kwenye hizo Tuzo na huwezi kusema ni Tuzo ndogo no way ikishawajumlisha WAsanii maarufu kama Diamond, Mzee Majuto na JB hizo ni Tuzo kubwa sana na ni muhimu kwenye CV ya Msanii,

- CATEGORY ya Blog:- Seriously kama kweli BASATA na watayarishaji wa zile TUZO wangekuwa serious hakuna Blog au website Tanzania inayoizidi Jamiiforums nasema hakuna, Jamiiforums ndiyo website peke yake inayopitiwa na Viewers wengi with straight numbers bila kurudia rudia, kwa mfano ukiona kuna website namba zake zinaonyesha imepitiwa na viewers Laki Mbili kwa siku maana yake ni kwamba wamepitia Viewers Laki moja wakarudia rudia kuingia na kutoka, lakini only Jamiiforums ndiyo ina wasiojirudia staright in numbers kama Laki Mbili ni hizo hizo Mbili sasa leo hata kwenye nomination haikuwemo, WHY?

- MWANAMUZIKI MWANAUME ANAYEPENDWA TANZANIA KULIKO WOTE:- Please nani Tanzania ya leo anayeweza kumshinda Diamond? I mean eti ameshindwa kwa sababu hakupata kura, hizi kura zinatusumbua sana Tanzania kila siku kwenye siasa ni ugomvi kisa kura leo unazileta tena kwenye kuamua ubora wa kazi za msanii? That is a shame now BASATA hawawezi kukwepa hii lawama kwa sababu walikuwepo na ni lazima walihusika, watayarishaji sio tatizo sana lakini tatizo ni kushiriki kwa BASATA kwenye zile Tunzo kunawabana sana na FULL RESPONSIBILITY ya kila kilichofanyika kwa uzuri na ubaya, uzuri ni kwamba ni muhimu sana kuwepo kwa hizi Tunzo lakini ubaya ni kwamba BASATA haina watu competent enough wa kusimamia Vipaji vya wasanii,

- BASATA wanahitaji kupunguzwa nguvu now kabla hawajaharibu kabisa hii field ya Sanaa, cause tukiendelea na huu mfumo wa kupiga kura kuhukumu kazi za wasanii maana yake ni kwamba tunafungua miaanya wa watu kuanza kuvuta rushwa tu, Msanii afanye kazi zake zionekane lakini tusimpe mzigo wa kuanza kutafuta kura za kuhukumu ubora wa kazi zake hapana, kipaji chochote kinatakiwa kuhukumiwa na matokeo ya kazi zake mbele ya jamii.

- Now kwa hayo yote ninarudia tena kusema Diamond hakushinda kura kwa hiyo sio MSanii anayependwa sana na jamii ni njia rahisi sana ya kuua vipaji vya sanaa yetu, ninasema BASATA wamekosea na wanatakiwa kuangaliwa na Serikali now kabla hawajatufikisha kurudi kule kule tulikotoka kwenye kushangilia kina Kandabongoman MWanamuziki ambaye huko kwao hawezi kupiga dansi la peke yake akajaza watu mpaka aje Tanzania, siku hizi tumepigana tumeinua Vipaji vyetu ndio maana hawa wageni hawaji tena yale mambo ya bendi za Wakongo kusumbua hapa mjini hamna tena, sasa wanakuja BASATA na kutaka kuivuruga Sanaa, SErikali ni lazima iingilie kati tena sasa!!

Le Mutuz

-


Bro thread nzuri ila wote tunafahamu hasira zote hizi ni kwa sababu Ali Kiba alimbwaga Diamond kwenye Tuzo za Watu. Nilitegemea msomi kama wewe unaelewa tuzo zinazoendeshwa kwa mfumo huu kura za mashabiki ndio zinaamua mshindi kwa 100%, tafadhali pitia kwa waanzilishi wa Marekani People's Choice Awards: Fan Favorites in Movies, Music & TV - PeoplesChoice.com uangalie utaratibu wao kisha linganisha Tanzania People Choice Awards hakuna tofauti,

popular vote ndio inaamua mshindi. Tuzo kama Kili ndio zinahusisha majaji kwa sababu toka hatua za awali zinahusisha Academy kwa hiyo kunahitajika majaji watakaohakiki. Kitu pekee ninachoweza kukwambia umshauri rafiki yako Diamond na team yake ni kuwa waache kudharau hizi tuzo za ndani. Majina yalipotangazwa Ali Kiba alipost Instagram na Facebook kuomba kura kwa mashabiki na team yake ilikuwa mstari wa mbele kupiga kampeni Instagram ikiwatumia watu wengine maarufu kumuombea kura.

Upande mwingine Diamond hakuwa na time kabisa, ndio kwanza akaanza kuziponda tuzo za Kili mara baada ya Wema na Jokate kuanza kumpigia debe Kiba. Bado wiki mbili upande wa Kili kura zifungwe na ninakuhakikishia kuna kila dalili ya Diamond kuangukia pua kwa mara nyingine kama ataendelea na kiburi cha kutegemea eti kwa kuwa ni maarufu au ndiye mwanamuziki anaetambulika kuliko wote kwa sasa kwamba basi atapewa tuzo. Akamuulize Fid Q ambaye alikuwa na mentality hiyo hadi aliposhtuka mwaka jana baada ya kina Fella na Babu Tale kuendesha kampeni ya kumuombea kura na akapata tuzo mbili.

Kuhusu website maarufu, tambua kwamba Jamii Forums walikuwa wadhamini wa tuzo na hiyo moja kwa moja ilikuwa inawaondoa katika kinyang'anyiro. Na kama ulikuwa hujui website zenye traffic kubwa kwa sasa Tanzania ni Jamii Forums, Millard Ayo, Issa Michuzi, Global Publishers na Raha Tupu (ile ya ngono). Pamoja na hayo kura ndio ilikuwa inaamua kama wapenzi wa website tajwa hapo juu ukitoa JF na Millard hawakupiga kura kwa wingi usitegemee wataingizwa kwa kuwa tu ni "mafaza".

Miss Tanzania sifahamu sana, ila ninavyoelewa inaendeshwa na kampuni iliyopewa leseni na Miss World kwa hiyo BASATA hawana uwezo wa kuwaambia jamaa wawanyang'anye leseni ni sawa na Wizara ya Michezo isivyokuwa na uwezo wa kuwaambia CAF au FIFA wamtimue Malinzi.
 
Hayo mashindano hayana faida yoyote.

Ni udhalilishaji wa kijinsia. Ni kuwauza binaadam, hususan wanawake kwa njia za kisasa.

Mwanamke kufanya jema lolote si lazima apitie mashindano hayo. Hao wanaofanya mashindano hayo wanatengeza fedha kwa kuwaanika wanawake.

Yafungiwe maisha.
 
BASATA nimuendelezo wa uozo uliopo kwenye tasnia ya michezo tz ... yanayofanyika fft ni ajabu .... unasikia mtu kapigwa ban ya miaka 7, mara kafungiwa miezi sita etc ... yaani napata picha kuwa walioko huko ni genge fulani ....
 
mkuu wewe uko kundi gani ndani ya chama? 'ukawa' ile ya ndani ya chama ama ?
 
Hivi mbona unahangaika sana tangu wakutose kwene ukuu wa wilaya unaonekana una mhemko wa akili.

- Sijawahi kuomba wala kugombea Ukuu wa Wilaya, I am a business man karibu sana ofisini kwangu hapa Tancot House 2nd Fl, gharama tu ya kuendesha ofisi yangu inaweza kua ni mshara wa Mkuu wa Wilaya mara tatu so sio mimi kaka mtafute mwingine mwenye hizo lawama za Ukuu wa Wilaya, hahahahahaha U know

Le Mutuz
 
Hayo mashindano hayana faida yoyote.

Mi udhalilishaji wa kijensia. Ni kuwauza binaadam, hususan wanawake kwa njia za kisasa.

Mwanamke kufanya jema lolote si lazima apitie mashindano hayo. Hao wanaofanya mashindano hayo wanatengeza fedha kwa kuwaanika wanawake.

Yafungiwe maisha.

- Tanzania sasa Ni Capitalism sio Communist tena kwenye ubepari kila mwananchi anapewa nafasi ya kujaribu anachoweza Wasichana waachiwe wafanye wanayoweza na wanaume wafanye wanayoweza!!

Le Mutuz
 
Naona umenyimwa fursa za kupiga picha na vidosho sasa unalia lia na BASATA. Nani kakwambia Diamond anapendwa na wengi peke yake kumbuka Alikiba naye anapendwa sana. Halafu jamiiforum sio blog usiiweke kwenye hiyo category unaidhalilisha, kwa millard ayo sawa acha wivu
 
Wrong Platform. Dogo, huku sikuhizi wanaCCM wenzako wananyukana tu kuhusu mgombea wao aliyetangaza nia jana. Njoo nawe unyukane na akina Lizaboni, Msalani na wengine wengi. Au mpaka ulipwe posho yako kwanza? Manake jamaa anagawa mihela kama hana akili nzuri, halafu anasema ni michango ya rafikize eti tusiwe na wasiwasi ingawa hatuelezi hao rafikize atawalipaje au atawafidia vipi. Njoeni mnyukane wana ccm.
 
Hayo mashindano hayana faida yoyote.

Mi udhalilishaji wa kijensia. Ni kuwauza binaadam, hususan wanawake kwa njia za kisasa.

Mwanamke kufanya jema lolote si lazima apitie mashindano hayo. Hao wanaofanya mashindano hayo wanatengeza fedha kwa kuwaanika wanawake.

Yafungiwe maisha.

Kijensia= Ki-jinsia
 
- Tanzania sasa Ni Capitalism sio Communist tena kwenye ubepari kila mwananchi anapewa nafasi ya kujaribu anachoweza Wasichana waachiwe wafanye wanayoweza na wanaume wafanye wanayoweza!!

Le Mutuz

Waandaji wa hayo mashindano wamejawa tamaa ya ngono kama wewe kupiga picha na warembo ndio maana tunapata warembo wasio na sifa. Kuhusu kufungiwa mda ukifika shindano litafunguliwa tena kwa sasa tumestopisha. Kazi zipo nyingi sio umiss peke yake
 
Haaa haaa hicho kiofisi chako tuna taarifa zake kupitia kwa mzazi mwenzako alishakuumbua siku nyingi.JK kabakiza miezi mitano magogoni jumuiya zote za chama zilipeleka majina kwaajili ya kuteuliwa ukuu wa wilaya jina lako likatoswa nasikia ulilia sana. JK tayari kampa ulaji Mama Malecela unaibu waziri bado mnataka ukoo mzima mbebwe kama watoto.

Halafu usitake kujifanya hamnazo tangu lini ukuu wa wilaya ukagombewa hizi ni nafasi kwaajili ya wale wote waliokosa ubuge,wapayukaji mjengoni.


- Sijawahi kuomba wala kugombea Ukuu wa Wilaya, I am a business man karibu sana ofisini kwangu hapa Tancot House 2nd Fl, gharama tu ya kuendesha ofisi yangu inaweza kua ni mshara wa Mkuu wa Wilaya mara tatu so sio mimi kaka mtafute mwingine mwenye hizo lawama za Ukuu wa Wilaya, hahahahahaha U know

Le Mutuz
 
unataka miss tz ifunguliwe ili uendeleze ukuwadi wako??? utalaumu sana lakini miaka miwili itapita ukiwa alosto mkuu pole....
 
Hayo mashindano hayana faida yoyote.

Mi udhalilishaji wa kijinsia. Ni kuwauza binaadam, hususan wanawake kwa njia za kisasa.

Mwanamke kufanya jema lolote si lazima apitie mashindano hayo. Hao wanaofanya mashindano hayo wanatengeza fedha kwa kuwaanika wanawake.

Yafungiwe maisha.

Alshabaab!/philosophy
 
Sijui alikuwa anamaanisha nini maana yeye ndiye bingwa wa kuwananga wenzie kwenye typing error FaizaFoxy

Huwa sisahihishi "typing" error, huwa nasihihisha Kiswahili kinapopotoshwa, hususan kwenye "R" na "L". Lakini nnafurahi ikiwa nimekosea "typing" na mtu akanionesha, huwa nnakwenda kurekebisha.

Siku hizi wewe hukosei kwenye "R" na "L" umefaidika sana na darsa la FaizaFoxy.
 
Last edited by a moderator:
Haaa haaa hicho kiofisi chako tuna taarifa zake kupitia kwa mzazi mwenzako alishakuumbua siku nyingi.JK kabakiza miezi mitano magogoni jumuiya zote za chama zilipeleka majina kwaajili ya kuteuliwa ukuu wa wilaya jina lako likatoswa nasikia ulilia sana. JK tayari kampa ulaji Mama Malecela unaibu waziri bado mnataka ukoo mzima mbebwe kama watoto.

Halafu usitake kujifanya hamnazo tangu lini ukuu wa wilaya ukagombewa hizi ni nafasi kwaajili ya wale wote waliokosa ubuge,wapayukaji mjengoni.

- Haya yote ulkiyoandika hayanihusu hakuna Jumuiya inapeleka majina ya WAgombea ingakuwa kweli Wangepata wengi sana kutoka Jumuiya na hata wewe ungepata, hahahahahahaha eti unasema jina langu ulipeleka wewe na uknaiona ninalia sana hahahahahahahah siku ikitokea nitakuwa nakaribia kufwa eti nalilia ukuu wa wilaya, hapana mkuu inawezekana unajisema mwenyewe, eti unategemea mimi niondoke hapa downtown nikawe mkuu wa Wilaya ya Mkarama? hahahahahaha


Le Mutuz
 
Back
Top Bottom