Serikali iwastaafishe watumishi wake wasio productive

Serikali iwastaafishe watumishi wake wasio productive

cc Rais Magufuli
TAMISEMI
Halmashauri
Serikali kuu
Kuna wazee katika halmashauri zetu ambao unakuta wamebakiza miaka miwili mmoja au hata mitatu, sasa hawa watu kwakweli kutokana na maisha ya kufanya kazi serikalini kutokua katika kiwango cha umoja wa kimataifa katika mishahara cha kuishi above dollar moja, unakuta hawa watu wengi wamechoka kimwili na kiakili, '' sio wote''but ni wengi sana.

Sasa unakuta kazi hawafanyi na baadhi ni wakuu wa vitengo kazi hazifanyiki kwa wakati espeially hii kasi ya Mh raisi kasi yao ni ndogo mno kama mjuavyo serikalini kazi zinafanyika kutokana na uamuzi wa mtumishi yeye ndio anaamua lini afanye sio u urgency wa hio kazi.

Sasa hawa utakuta wanaenda tu kuzuga pale ofisini wataonyesha sura zao then hao wanaendelea na mishe zao ukiwauliza wanakwambia tunasubiri muda wetu iushe tu retire tupate mafao yetu na wengi wameisha calculate kabisa kwa hio akili yake yote imehamia kwenye mafao.

Sasa mi nilikua ninaomba baadhi yao badala ya wao kusubiri huo muda serikali iwasaidie kuwa staafisha mapema ili wenye nguvu waendelee na kazi na pia kupunguza gharama ya mishahara ya hiyo miaka mitatu na vile vile kulisaidia taifa liweze kusonga mbele fasta maana hawa wazee ni vikwazo kwakweli kwa utendaji wa kazi, tafadhali TAMISEMI saidieni hawa wazee wapate mafao yao ndio only thing they are waiting for.

Hizi mada zitakua zinaendelea kidogogkidogo tunajaribu kufanya research kwa nini hatuendelei Africa(Tanzania case study) sasa moja ya sababu ni utendaji kazi wa watumishi sasa hako ni ka line kamoja ili watu wasiboreke na kuchoka nitakua napakua kidogokidogo na wengine pia tunachangia mawazo yetu tuisaidie nchi yetu iendelee tuivunje hii chain ya kutokuendelea tutagusa kila sehemu, economical, political, social, envoronmental, kila sehemu.
Yeah Tukianza na wewe
 
Naona kuna ukweli....kwa mtazamo wangu serikalini asilimia kubwa ni mizigo....no productivity...no creativity
 
Huku Jeshi la Magereza wapo kibao wana vyeo vikubwa sana ila kazi yao kunyanyasa maaskari wa vyeo vya chini.
 
Naunga mkono hoja
Pasco
Pasco na wewe usiwe unaunga mkono hata hoja muflisi! Hii hoja si imetolewa na mtu aliyekatwa kichwa hii? Hivi anaelewa umri wa kustaafu kwa hiari ni miaka 55 na kwa lazima ni miaka 60? Basi amshauri Magufuli apunguze umri wa kustaafu uwe miaka 45 basi ili naye aweze kupata ajira. Mwaka huu vijana mtarusha mno mawe na mtatembea na bahasha mpaka mkongoroke, siku mnapata ajira serikalini mtakuwa mmechoka ile mbaya! Mjomba amesema ajira basi mpaka miaka yake mi-5 au 10 iishe!!
 
usiongee vitu ambavyo huvijui na hauna uhakika hebu tembelea halmashauri kadhaa na sio hizo tu na sector nyingine za serikali ndio uje mwage povu lako
 
usiongee vitu ambavyo huvijui na hauna uhakika hebu tembelea halmashauri kadhaa na sio hizo tu na sector nyingine za serikali ndio uje mwage povu lako
Vuta subira mdogo wangu, watakuwa wanapungua taratibu mara muda wao wa kustaafu ukifika! Wakikwambia uwalipe hiyo miaka yao iliyobaki ili waachie nafasi utaweza? Mmeshauri na Angella Kwamba mkatafute shughuli za kufanya, msisubiri ajira za Magu ambazo hazijulikani zitatoka lini!! Hata wewe utafikisha tu hiyo miaka 58, tukuone kama utaachia ngazi mapema!!
 
Back
Top Bottom