Serikali iwamulike hawa manabii

Serikali iwamulike hawa manabii

Yesu hakuacha kanisa la wezi waliofungua benk kwaajili ya kuuibia wananchi napia sio kila mtu anafanya utumishi wa Mungu ametoka familia maskini jaribu kutuonyesha mali walizonazo na ushahidi kwamba waliwaiibia waumini wao.
 
Watumishi wa kweli wa MUNGU humtanguliza MUNGU WA KWELI na kinachofuata ni Wanadamu baadae vinginevyo. Ni kama ilivyo kwenye mstari wa Amri za MUNGU alizo tupatia. Sasa hawa wasio wa MUNGU hutanguliza vya mwili. Yaani wamenenepa sana kimwili kuliko kiroho.

Fikiria tu wakati wanaonyesha mazingaombe yao anakuwa na kiburi hata kuwadharau madaktari. Ukweli miujiza ya MUNGU ipo, ila ya hawa wengine sio ya MUNGU bali ni utapeli tu.


Mtu wapi imeandikwa kuwa unanyunyuziwa maji na kuweweseka, au kusukumwa kwa kidole bila ya kutaja hata jina lililo kuu. Alafu wengine wanauliza mapepo maswali meengi na kuamini kuwa mapepo yanasema ukweli. Kumbe shetani ni baba wa uongo. Pepo likimdanganya kuwa nimetumwa na jirani, unaanza kufoka kwa jirani, kumbe ni uongo wa shetani. Nabii unaongea na mapepo na kuyaamini?. Nyie ni sawa na wapiga ramli.

Mod. naomba usini ban

Na wengine niambieni
 
Angalia yule mama alitoa senti na ndiye aliyebarikiwa kuliko walivyotoa matajiri. Sababu alitenda haki ya kutoa alichonacho na kuwa na furaha na amani.

Wale matajiri walitoa kiasi kikubwa na hawakuwa na furaha sababu hawapendi kupungukiwa. Sasa hawa jamaa zenu wanapenda tu wanaotoa pesa kubwa na kuona kuwa ndio wa kubarikiwa. Na masikini akitoa alichonacho hathaminiwi, wala hatembelewi na nabii.

Nabii hawajui hata kwa majina wahumini masikini, bali kwenye smartphone yake kuna majina ya matajiri, na anawasiliana nao tu, hasa kufuatilia michango.

Mie ni niambieni
 
Acha mtapeliwe si mnasali ktk makanisa ya wanadamu baala ya kanisa alililoacha Yesu ambalo ni Catholics! badala yake mnatapeliwa kule 'mlima wa baridi', 'kanisa la kufukua', 'kanisa la efwatwa' kwa 'mzee wa upwakwa' 'kanisa la kikobe' nk

Thibitisha mkuu hayo matamshi yako?? kanisa aliloacha yesu ambalo huwasalia wafu?? na kuwaita watakatifu mfano.mtakatifu nyerere! kanisa ambalo mmehararisha pombe! kanisa mnalosalia ibada za sanamu zilizochongwa kwa ustadi wa wanadamu na mnazisujudia!! kanisa ambalo mtu huingia kanisani na mzigo wa mapepo na kutoka hvyohvyo kwa sababu ya ibada zenu za kukalili!! kanisa aliloliacha yesu???

mbona mitume wake kumi na mbili aliowaacha aliwaachia msaidizi ambaye ni roho mtakatifu ambaye kupitia huyo wengi wa wasioamini walipoamini hao mitume waliweza kuwashushia huyo msaidizi na wao kuanza kunena kwa lugha mpya,je ni kanisa gani la katoliki wanaonena kwa hiyo lugha??? kanisa ambalo sijawahi kuona wakiwaponya watu mizigo yao au hata kutoa pepo??

mbona Yesu mwenyewe aliweza kutoa pepo na hata mitume wake walikuwa wakitoa watu pepo na kuponya watu,je ni kanisa gani hilo ambalo yesu aliliacha ambalo hawasemi kwa lugha mpya kumaanisha roho mtakatifu yupo ndani yao! na kanisa gani hilo ambalo hawatoi pepo na kuharibu kazi zote za shetani???? nyie ndo wale mnaofata mapokeo ya wanadamu na si biblia, hivi ni wapi kwnye biblia walikuwa wanawabatiza watoto wadogo???

kwa maana kubatizwa ni kuzaliwa kiroho kwa mara ya pili na hiyo huja baada ya mtu kumkiri na kuamini kuwa yesu ni bwana na mwokozi wako ndipo mtu hubatizwa,sasa nyie inakuwaje mnawabatiza watotonwadogo ambao hawajui chochote??? ndo maana yesu pia alibatizwa alipokuwa mtu mzma. Ndugu narudia tena kusema ukiwa unaandika kitu uwe unafikiria mara mbili.
 
1. Serikali inaingiliaje uhuru wa watu kuabudu?
2. Unadhani ni wote manabii wanaochukua fedha za watu?
3. Kwa mtazamo wako unadhani ni kazi rahisi kuibuka tu na kusema wewe au fulani ni nabii?
4. Kama ni wa uongo na wamekuja kulaghai watu kwa nini uhangaike nao sasa hivi wakati Biblia imabainisha wazi wapi wanaenda baada ya maisha haya ya chini ya jua?
 
Mi nafikiri kila MTU anaki na imani take.lakini msihukumu maana mtahukumiwa
 
Wewe umepotoshwa, halafu unataka kupotosha wengine! Acha upotoshaji wewe, tafuta Kitabu cha BWANA ukasome! (ISAYA 34:16). Yesu hakuacha kamwe kanisa la Catholics! Yesu hakuwa Mkatoliki. Yeye alibatizwa katika maji tele (MATHAYO 3:13-17), tofauti na Wakatoliki. Vilevile, tofauti na Wakatoliki wanaopinga juu ya kuokolewa, Kanisa aliloliacha Yesu lilikuwa la watu waliookolewa: MATENDO YA MITUME 2:47,"...Bwana akalizidisha KANISA kwa wale waliokuwa WAKIOKOLEWA." Eti Makanisa ya wanadamu! Kwa taarifa yako, Mungu anafanya kazi na wanadamu (1WAKORINTHO 3:9; EZEKIELI 22:30). Tangu Kitabu cha MWANZO, Mungu anatajwa kufanya kazi na wanadamu, ambao hata taasisi zao hazitajwi: Nuhu, Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Musa, Yoshua, Eliya, Elisha, Yohana Mbatizaji, Petro, Yohana, Paulo n.k.

Wewe unamtumikia nabii gani mpendwa? Au tupo wote kule mlima wa maji? ubarikiwe sana mtumishi.
 
Soma Matendo ya mitume yote na barua zote za mtume Paulo

Mimi huwa nasoma vizuri sana bible na sijawahi kuona mahali pameandikwa kanisa katoliki na mwanzilishi ni Yesu Kristo, ndiyo maana nikakuuliza unioneshe specific verse!
 
Back
Top Bottom