Wewe umepotoshwa, halafu unataka kupotosha wengine! Acha upotoshaji wewe, tafuta Kitabu cha BWANA ukasome! (ISAYA 34:16). Yesu hakuacha kamwe kanisa la Catholics! Yesu hakuwa Mkatoliki. Yeye alibatizwa katika maji tele (MATHAYO 3:13-17), tofauti na Wakatoliki. Vilevile, tofauti na Wakatoliki wanaopinga juu ya kuokolewa, Kanisa aliloliacha Yesu lilikuwa la watu waliookolewa: MATENDO YA MITUME 2:47,"...Bwana akalizidisha KANISA kwa wale waliokuwa WAKIOKOLEWA." Eti Makanisa ya wanadamu! Kwa taarifa yako, Mungu anafanya kazi na wanadamu (1WAKORINTHO 3:9; EZEKIELI 22:30). Tangu Kitabu cha MWANZO, Mungu anatajwa kufanya kazi na wanadamu, ambao hata taasisi zao hazitajwi: Nuhu, Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Musa, Yoshua, Eliya, Elisha, Yohana Mbatizaji, Petro, Yohana, Paulo n.k.