Serikali italipa lini malimbizo ya mshahara?

Administer

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
930
1,408
Naiuliza tu hii Serikali italipa lini malimbikizo ya mishahara ya walimu? Kuna awamu mbili ya madai ya malimbikizo ya mishahara ya walimu,kuna waliopanda daraja 2018 na 2019 hatujalipwa hadi leo hii. Kwa upande wangu ninadai shilingi laki nane. Kiasi hicho cha pesa kwa kada yangu hii ya uwalimu naona itanisaidia hata kununua kiwanja huku nilipo.

Viongozi wa serikali mliomo humu na wana CCM naamini kwa nafasi zenu ikumbusheni Serikali swala hili kwani linaweza kuwatia doa katika kipindi hiki.
 
Siasa kumbe ni babalao...!!

Ni mfumo wa maisha unaoathiri nyanja na sekta zote za kijamii katika taifa lolote...

Wanasiasa na siasa zao ndiyo wanaoamua huyu mwalimu, polisi, daktari, watendaji mbalimbali alipwe nini na kwa kiwango gani na kwa wakati gani na kwa sababu gani...

Mwalimu hoja yako umeileta in the right place and in the right time. Wahusika wataupata ujumbe, wata respond tu....
 
Naiuliza tu hii Serikali italipa lini malimbikizo ya mishahara ya walimu? Kuna awamu mbili ya madai ya malimbikizo ya mishahara ya walimu,kuna waliopanda daraja 2018 na 2019 hatujalipwa hadi leo hii. Kwa upande wangu ninadai shilingi laki nane. Kiasi hicho cha pesa kwa kada yangu hii ya uwalimu naona itanisaidia hata kununua kiwanja huku nilipo.

Viongozi wa serikali mliomo humu na wana CCM naamini kwa nafasi zenu ikumbusheni Serikali swala hili kwani linaweza kuwatia doa katika kipindi hiki.
Pambana na hali yako
 
Kwa awamu hii nasikia hata huko tu kupanda daraja na ukalipwa mshahara wa daraja jipya, shukuru Mungu kwani watu wamepitisha miaka 5 sasa daraja jipya hawalijui! Serikali hii na kitu kinachoitwa maslahi ya watumishi ni mbalimbali! Kuna taarifa kuwa angalau mwezi huu kuna nyongeza ya mishahara lakini nayo ngoja tusikie lazma itakuwa kiduchu maana mawaziri wote waliopewa jukumu la kushugulikia maslahi ya watumishi katika awamu hii ya serikali imeonyesha hakuna wanachohangaikia kuhusu watumishi, wao wakilipwa zao tu imetoka! Mwaka huu wapinzani wakijenga hoja nzuri wakashikilia bango kuboresha maslahi ya watumishi mathalani kuwalipa malimbikizo pamoja na kuwapandisha madaraja wote katika ngazi walizostahili kuwa, hapa CCM lazima ipoteze kura!
 
Back
Top Bottom