Serikali itafaidikaje na Takwimu ya udini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali itafaidikaje na Takwimu ya udini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by QUALITY, Jun 26, 2012.

 1. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  jana katika taarifa ya TBC1, Shekhe Simba alitoa kauli ya kuwataarifu waislam kushiriki katika sensa baada ya serikali kukubali kuingiza kipengere cha dini katika hojaji ya sensa inayotarajiwa kufanyika August 2012.

  Swali kwa serikali ni kwa namna gani tutatumia takwimu za udini wa mtanzania katika kumletea maendeleo? Au imefanyika kuiridhisha dini fulani ili sensa iweze kufanyika?

  Quality
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,831
  Trophy Points: 280
  mimi wakiniuliza dini yangu ntawaambia MTANGANYIKA
   
 3. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Sasa wewe umekerwa !? Kutakuwa na option mbili, aidha useme una dini na ni ipi ? Au huna dini. Chagua moja !
   
 4. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Kuna faida nyingi katika hizo "data" ambaye anae zihitaji hizo data ataziomba zikiwa ni official data toka serikalini. Kama kampuni inataka kufungua biashara fulani na ikagundua kuwa wateja husika (majority) inaingiliana na imani zao, ikaacha au ikabadilisha, je hujaona hizo busara? !
   
 5. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  na vita ya udini na kuchoma makanisa ikishamiri, wataangalia nani wengi?

  Kwani kama dini yangu hindu... nikitaka takwimu za wahindu wote nikiwa mhindu, nitazikosa?
  Au unataka kusema waislamu wakitaka kujua wako wangapi kwa kutumia machinery zao hawawezi kupata takwimu hizo?
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,831
  Trophy Points: 280
  Kiti moto huliwa na bia hunywewa na watu wa dini zote na ni biashara zenye faida kubwa bila hizo data........ntajie bidhaa nyingine inayoguswa na dini
   
 7. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,285
  Likes Received: 807
  Trophy Points: 280
  Tunakuza matatizo tu, unajua ugomvi wa Sarai na Hajir, ugomvi wa nani bora Ishmail na Isaack au nani bora Israel na Palestina
  Hivi sisi wabantu hatuna imani zetu au nyingine zaidi ya hizo 2 ?
  Matokeo yake baada ya Sensa mtayaona hasa baada ya waliozitaka Data hizo kuziona tofauti na wanavyotaka
   
 8. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ninhakika kuwa hawatapata majibu yaliyosahihi. (errors 66%). not reliable data

  Quality
   
 9. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Dini zote hazinywi bia wala kula kiti moto ! Wasabato masalia pia wamegomea kiti moto ! Utakuwaje na dini halafu ufanye vinavyokatiliwa na dini !? Utakapotaka kubadilisha mitaa ya Zanzibar kuwa Sinza ndogo, lazima utapata matatizo ! Hebu fikiri kidogo kabla ya kuropoka !
   
 10. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Hilo wewe linakusumbuwa nini !?
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,831
  Trophy Points: 280
  Nimekuomba unitajie bidhaa ambazo huuzwa kwa misingi ya imani ya mtu ukashindwa(mimi nimekutajia).......wewe unakimbilia kudai naropoka..sasa utuambie huyio mfanyibiashara anataka kutumia takwimu za kidini kupanga biasha gani? Mchele wa kiislamu na mchele wa kikristo upo?
   
 12. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #12
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Wewe una kerekwa na nini hasa na hizi takwimu kupitia sensa !? Nini kinapungua kwako ? Hofu yako ni juu ya nini !? Yaani mnashangaza kweli na hayo madonge yenu
   
 13. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #13
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  kusema mtu ana Dini halafu anakula kiti moto, huko sio kuropoka !? Hiyo list ya bidhaa itajustify nini kwako ? Serikali itapata hasara kwa kuwa na takwimu za idadi ya watu na dini zao ? Serikali ilijuaje Tanzania ina makabila zaidi ya 120 ?
   
 14. Keen

  Keen JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 620
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuna faida nyingi za kujua dini za watu. Pamoja na kuwa serikali ilisema mwanzo kuwa maendeleo hayapangwi kwa dini za watu, lakini kuna "interventions" nyingi ambazo zinaweza kufanyika kiurahisi kwa kutumia dini au viongozi wa dini kuwahamasisha waumini wao kufanya madadiliko fulani kwa ajili ya kujiletea maendeleo. Tafiti zimeonyesha kuwa dini imekuwa na uhusiano wa karibu na mambo mengi ya maisha ya kijamii, kiuchumi, kiafya, nk. Kwa mfano, kuna dini zingine zina imani ya kukataza waumini wa wasiwapeleke watoto wao kupata chanjo fulani, au kwa mfano ikitokea kuwa vijana wanaoathirika kwa madawa ya kurevya ni wa imani (dini) fulani kuliko dini zingine, then inaweza kuwa rahisi kuchukua hatua kupitia makanisani kwao kubadirisha tabia za hao vijana. Kwa ujumla, pamoja na kuwa mimi si mwislam naungana nao kudai kuwepo kwa swali la dini katika dodoso.
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,831
  Trophy Points: 280
  Sasa unaenda kwingineko kabisa........hebu soma vizuri mawazo yako mwenyewe katika thread number 4
   
 16. M

  MBOMBO Member

  #16
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanasheria watoe michango apa... Ila mimi nafkiri jibu ni rahisi. Tanzania ni JAMHURI inayoongozwa na katiba. HAINA DINI (haiongozwi kwa misingi ya dini) ila watu wake wana uhuru wa kuamini katika imani zao ili mradi hawavunji sheria, Serikali inaheshimu imani na uhuru wa wa TZ.
  Sensa inahusu TAIFA sasa suala la kujua dini ya mtu la kazi gani...? Someni mantiki haswa ya kujua idadi ya wadini fulani na impact yake. Angalieni yanayotokea Nigeria sasa... Nafkiri watu tuwe na mtazamo kama wa mzazi na watoto wake, ambao licha ya tofauti zao kielimu, kipato, kimaendeleo nk. wote hubaki wa BABA MMOJA
   
 17. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #17
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Mbona mnakwepa swali la msingi, hivi idadi ya watu na dini zao inavuruga vipi utaifa ? Je wapi wameathirika kwa takwimu kama hizo !? Mbona zipo taasisi zimenukuliwa zikitoa takwimu za kuhusu dini zenye utata, je ni vibaya tukiwa na takwimu rasmi zinazotambuliwa na serikali !?
   
 18. M

  MBOMBO Member

  #18
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani wewe kuwa mtanzania haitoshi kukutambulisha na watu wakifanya kazi zao ipasavyo utapata kila kitu....? Kwa nini hatujifunzi kitu kwa kusoma herufi "USA" UK " UAE n.K...? Unafkiri hizi umoja zingefikia kuongoza dunia kimaendeleo kama zingeongea lugha ya udini,nk...? Alafu angalia DRC, Sudani, Nigeria na wengine na madhara ya udini, ukabila nk...? Afu mkumbuke Gadafi aliyeona mbali kutaka USA (United States OF AFRICA) walichomfanyia.." Msione vitu kijuu juu, siku zote mtu anaetaka kukusambaratisha lazima aangalie wapi akigusa nyie mtakosa umoja ili afanye anachotaka. Wew unafkiri WASUDANI wanavyogombana kwa kutumia dini na Urangi, ni wasudani wanaofaidika baada ya kugawanywa nchi kwa misingi ya dini na jee ni dini ilikua inatafutwa au ni Mafuta, na je wanaofaidi ni kina nani...?
   
 19. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,313
  Likes Received: 3,079
  Trophy Points: 280
  Suala la kipengele cha dini katika sensa ni muendelezo wa malalamiko ya Waislamu nchini kwamba Wakristo wanapendelewa katika mambo mengi, kutia ndani nafasi za kazi za kuteuliwa, chuo kikuu nk, japo wao (Wakristo) ndio wana idadi ndogo nchini. Ikitokea kwamba kweli Waislamu ni wengi Waisalamu wanataka kudai kufuata ratio ya idadi ya Wakristo/Wasilamu katika mambo ya uteuzi na nafasi nyingine.

  Waislamu wanaamini kwa dhati kwamba wao ni wengi nchini kuliko Wakristo, hasa ukizingatia Tanzania ni pamoja na Zanzibar.

  Suala la kujiuliza ni kwamba, vipi ikiwa Wakristo wataonekana ni wengi zaidi, Waisalamu watakubali suala la wingi wa Wakristo liwe kigezo cha kutumika katika uteuzi wa kazi na nafasi za chuo kikuu nk?

  Believe me, ikionekana Wakristo ni wengi zaidi ya Waislamu, kuna watu watasema sensa imechakachuliwa.
   
 20. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #20
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Ulizia "fitna" ya Sudan aliitengeneza nani ! Ili uelimishwe. Hakuna udini pale. Nigeria kuna fitna ya dhulma na si dini. Fitna ya Angola si Savimbi wala dini, ulizia aliye ipanga. Iweje Waarabu maisha yao ni bora kwa mafuta, lakini Wanigeria kuna umaskini wa kupindukia !?
  Bado nakuuliza idadi ya watu na dini zao athari yake ni nini !?
   
Loading...