Serikali itabakia Dodoma?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2006
Posts
4,192
Reaction score
678
Kwanza kabisa kama mtanzania niungane na watanzania wenzangu katika kuombeleza msiba huu mzito uliolikumba taifa letu.

Tumeona na kushuhudia juhudi za mwendazake Rais John Pombe Magufuli kuifanya Dodoma kua Makao makuu ya serikali, mengi yamefanywa kuanzia miundo mbinu, kuhamishwa taasisi nyeti za serikali pamoja na rais na viongozi wakuu wa serikali kuhamia Dodoma.

Jee baada ya kifo chake ari na kasi ya kuifanya Dodoma kua mji wa Serikali na makao makuu itaendelea?
 
Ingependeza hilo fungu tuwekeze katika kilimo, tupate malighafi viwanda na ajira. Taasisi ambazo bado waendelee huko waliko,dunia sasa ni ya mtandao,mgawanyo madaraka nani, wangapi wanahitaji kwenda kwa waziri wizarani?? Ikulu??
 
Hayakuwa maamuzi sahihi ya kupeleka watu kule Dodoma ndoa zimevunjika watu wamekufa kwa presha kisa mtu anataka sifa tu eti kafanya kitu ambacho Baba wa Taifa alishindwa matokeo yake anawapeleka watu kule yeye anakimbilia kutibiwa Dar, tulikosea sana watanzania
 
fedha nyingi sana zimeekezwa dodoma, Jee ndio safari ya kua mji imefia hapa ?
 
Ikulu ya dodoma igeuzwe chuo kikuu cha ufundi afrika mashariki itoe elimu kuanzia veta Hadi PhD.Ikulu mbili ni gharama ibakie ya dar tu.
Uwanja wa ndege wa Chato wapewe jeshi Ili isipotee.Uitwe Magufuli airwing.
 
Ikulu ya dodoma igeuzwe chuo kikuu cha ufundi afrika mashariki itoe elimu kuanzia veta Hadi PhD.Ikulu mbili ni gharama ibakie ya dar tu.
Uwanja wa ndege wa Chato wapewe jeshi Ili isipotee.Uitwe Magufuli airwing.
😀😀😀😀😀😀😀
 
Wengine huku wameshapata nyumba ndogo na wamezaa kabisa sasa ni bora wakawaacha tuu huku
 
itategemea na utashi wa Mama yetu na wasaidizi wake wa karibu - hata kama ni kurudi Dar basi itakuwa kwa style ya kimya kimya - si lazima hadi utangaziwe !!

Ila nafikiri kwa Project zenye manufaa kwa taifa hasa hizi mbili SGR na Bwawa la Umeme basi tuzimalizie tu - zingine zisizo na tija tuachane nazo - ile midege mikubwa iliyopaki tunaweza kuiazimisha kwenye airline nyingine ama tukaipiga bei tukapeleka hela kuboresha mambo mengine kama elimu na bima ya afya kwa kila mtanzania.
 
Ile idea ya kufanya mji wa Serikali Dodoma kwa jina lake la MAGUFULI CITY LIENZIWE.

Mengine Ni ZIADA TUU .
 
Wengine huku wameshapata nyumba ndogo na wamezaa kabisa sasa ni bora wakawaacha tuu huku
nasikia watu wameshachaguana huko, aliyeacha mume dar na aliacha mke dar basi ni ndoa mwendo mdundo !! mambo ni rahaaa !! wakitoka ofisini wanapitiana - yaani kama kile kipindi cha boy friend / girl friend - maisha hani-muni
 
Hawajawahi kupenda Dodoma na vumbi lile kila uchao wako Dar hata huyo aliyewahamisha alikua Dar na Kafia Dar.mambo yakulazimishana ni magumu sana ,pia mtu kujiona ana akili kuliko wengine woooote ni mbaya sana
 
Hawajawahi kupenda Dodoma na vumbi lile kila uchao wako Dar hata huyo aliyewahamisha alikua Dar na Kafia Dar.mambo yakulazimishana ni magumu sana ,pia mtu kujiona ana akili kuliko wengine woooote ni mbaya sana
kwa kweli ukifikiria kwa kina sana huenda Mwenyezi Mungu katutua mzigo watanzania... wengi wamelia mno !!
 
... tulishaambiwa suala la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi lilishatungiwa sheria na "hakuna mwingine yeyote awezaye kulibadilisha"; serikali itaendelea kubaki Dodoma ni issue ambayo imesilibwa kwa "mihuri ya moto".
 
Kuhamia Dodoma kulikuwa kinadharia zaidi.
Mambo yote ya serikali yalikuwa bado chanzo chake ni kutokea Dar
Hata kuugua , kufariki na kutangazwa kumetukia ndani ya Dar.
 
off course sio swala la Utashi ni lakisheria lakini kule kukaa hakuna kipupwe panahitaji moyo
 
Hivi kuna nchi ya maana ambayo ilikua ishahamishia ubalozi wake Dodoma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…