Serikali isidanganye umma pesa kuchotwa na kupelekwa china hadi sasa mabilion ya ESCROW yako wapi

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Tuhuma nyingi za kunyosheana vidole ndani ya serikali hazijaanza leo angalia watu wote waliotuhumiwa katika kadhifa mbalimbali za uporaji wa fedha za umma nini walifanya-

Mfano pesa za escrow bilion zaidi ya 350+ zimeliwa na wajanja watuhumiwa wapo wapi na wanafanya nini, hapa mjue fedha zililiwa lakini wahusika wapo na wanadunda hakuna cha kuwafanya.

Juzi malipo yamefanyika na serikali kulipa kampuni ya symbion hata bunge kushirikishwa kuhusiana na pesa hizo hakuna, watu walipiga kelele hadi leo kimya bilion zaidi ya 350 zimeliwa

Wakati mama anaingia madarakani march 2021 alitangazia umma kuwa kuna fedha zimepigwa BOT Aliunda tume hadi leo nini kimefanyika.

Wakuu namalizia kwa kusema ccm ni chaka la majizi ndani ya nchi hii hakuna msafi wapo kwa ajiri ya kutuhumiana tu!

Wanachojuwa ni kupeana vyeo tu na wakikosana wanararuana wenyewe. nchi hii tunaaminishwa na viongozi hao kuwa ni maskini kumbe umaskini ni wa kutengeneza, nchi ambayo ni maskini haiwezi kununua magari ya MAWAZIRI NA MA RC kuanzia milion 500+ huku wananchi wake wakiishi kwa mlo mmoja.

Katiba mpya ni muhimu sana ingawa pamoja na kuwepo hiyo sijui kweli sheria zitafanya kazi ya kuwajibisha watawala naona kenya yanayoendelea! Katiba yao inafanya kazi kwenye chaguzi lakini kwenye kubana majizi ya mali za umma naona hakuna wakumfunga paka kengele wote ni makambale.
 
Ujanja huu wa ccm wananchi tuukatae fedha za umma hawana huruma nazo tutaendelea kuwatazama hadi lini !
 
Hayo hayawezi kuzungumziwa kwa sababu yanawahusisha wazee wa Msonga wanaoendesha nchi kwa remote control
 
Ndege wanaofanana huruka pamoja. Hakuna msafi hata mmoja ndani ya ccm na hakuna anayeweza kumwadibisha mwingine sababu wote wanajuana matendo yao na madudu yao hivyo hizo ni mbwembwe tu za kuwazuga watz.
 
Hakuna wa kumfunga paka kengele mana wote ndo walewale na wanajuana.
 
Wakuu namalizia kwa kusema ccm ni chaka la majizi ndani ya nchi hii hakuna msafi wapo kwa ajiri ya kutuhumiana tu!
ccm ni ukoo wa panya; baba mwizi, mama mwizi, kaka mwizi, dada mwizi, mjomba mwizi, shangazi mwizi, babu mwizi, bibi mwizi. By; Mh Nassari mbunge wa Arumeru
 
Baada ya chawa aliowaagiza kumchafua Jiwe kushindwa vibaya; ameamua aingie frontline mwenyewe. Je, atafanikiwa? Tuendelee kutafuna 🍿 🍿 🍿
 
Back
Top Bottom