Ile dhana ya kwamba makampuni mengi ya kibiashara kufunga biashara zake na kupunguza wafanyakazi limenikuta mbashara sasa.
Ni baada ya kampuni moja ninayofanyia kazi kuanza kupunguza wafanyakazi na kufunga baadhi ya vituo vya kibiashara kutokana na kodi kua kubwa huku mauzo yakipungua kila kukicha ingawa tuko katika kipindi kigumu kutokana na janga la korona.
Serikali tunaomba ilejelee tena swala la kodi sababu makampuni haya yameajili watanzania walio wengi ambao wanaendesha familia kwa kutegemea hayo makampuni. Sasa yanavofunga biashara na kuondoka kuna watu tunapoteza kazi wakati huo serikali haiwezi kutuajili wote, sekta binafsi ni chachu ya maendeleo popote duniani.
Kulipa kodi ni muhimu kwa kila mwananchi na nchi haiwezi kujiendesha bila kukusanya kodi yenyewe ni sawa lakini pia lazima kodi ziwe rafiki kwa walipaji, chukulia leo hii mo dewj afunge biashara zake ni watanzania wangapi watakao athirika pia nchi itakua imepoteza hata kile kidogo ilichokua inakusanya kutoka kwake. Hivyo, ni lazima bunge na serikali kwa ujumla wakae chini tena watafakali mstakabali mzima wa masuala ya kodi.