Serikali ipi imehamia Dodoma?

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
17,368
33,009
Kila siku mambo muhimu ya kiserikali yanafanyika Dar es Salaam, lakini tumeambiwa na kutangaziwa kuwa serikali na bwana mkubwa Rais wamehamia rasmi Dodoma.

Mawaziri wanaapishiwa Dar

Mabalozi wanaapishiwa Dar

Mabalozi wa kigeni wanawasilisha hati zao za viapo Dar

Rais muda wote yupo Dar

Mkataba wa Barrick a.k.a Acacia na Serikali/Twiga umesainiwa Ikulu Dar

Makamu wa Rais muda wote yupo Dar

Jaji Mkuu na viongozi wa vyombo vya usalama muda wote wapo Dar

Waziri Zungu karipoti Dar kwa ofisi ya Makamu wa Rais

Waziri Jafo naye yupo Dar

Mimi naomba kueleweshwa Dodoma wamehamia kina nani? Ni serikali ipi imehamia Dodoma?
 
Kwa mifumo ya mawasiliano E Gov , ugatuzi madaraka, mbali ya Wabunge nani Mtanzania anahitaji kufika wizarani kwa lipi!?Tumepoteza pesa bure maamuzi Dom, hapakuwa na uhitaji as planned earlier.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sisi ni waumini wa sera za mwalimu Nyerere,tutatekeleza kila alichopanga kufanya,kiwe na faida au kisiwe na faida, sasa naelewa why wazungu wanapenda kusafiri sana duniani,exposure ni darasa on its own
 
Kuweni na Subira, akishazindua rasmi hiyo Interchange ya Ubungo atarejea rasmi Makao Makuu ya Nchi. Najua hata wewe mleta uzi unajua wazi utamu wa ule upepo unaovuma kutoka bahari ya Hindi.
 
Back
Top Bottom