Vision 2030
JF-Expert Member
- Dec 10, 2017
- 407
- 250
1.Ieleweke kwamba hakuna Serikali yoyote duniani yenye uwezo wa kumtimizia kila hitaji lake mwananchi.Hata kule tulikoiga hii mifumo ya kuendesha nchi zetu wanakwama katika hili.
2.Awamu zote zilizopita tumekuwa tukifanya mambo kwa njia zilezile tukitegemea matokeo tofauti
3.Mtumishi anapostaafu akiwa na miaka 60 maendeleo makubwa sana anayokuwa amefanya si zaidi ya nyumba 2 ambazo hajazimalizia vizuri na kagari kamoja kabovu.
4.Watumishi wanatumia muda mwingi na rasilimali zao kuwaandaa watoto wao kuwa watumishi,kuoa na kuolewa hivyo kuendelea kutengeneza kizazi cha masikini.
5.Mtumishi akipewa muda mchache wa kufanya kazi miaka 10 mpaka 15 maximum atatumia muda mwingi kujipanga na kutobweteka hivyo kuwa na mtaji + kinua mgongo ambacho kitakuwa kizuri atakwenda mtaani kuongeza injini ya uchumi(sekta binafsi) na kutengeneza ajira za kutosha.Sio unampa Mtumishi fedha nyingi akiwa amechoka kimwili na kiakiri anazipoteza zote kwa kuwa hajawahi kuzishika na hajui azifanyie nini"
6.Kwa kufanya hivyo Mtumishi akistaafu akiwa na miaka 45 hatakuwa na pension ya kila mwezi kama inavyofanyika sasa.
7.Kwa kufanya hivyo Serikali itapunguza sana unemployment katika nchi.Wengi watapata mitaji kupitia kipindi ambacho wataajiriwa na kuanzisha shughuli za muda mfupi ambazo zitakuza sekta binafsi.
8.Sekta binafsi itaimarika sana kuliko muda wowote tangu nchi ipate Uhuru.
9.Serikali itakusanya sana kodi kuliko kipindi chochote toka Tanzania ipate Uhuru mwaka 1961.
10.Kutakuwa na ushindani wa huduma na matumizi makubwa ya tekinolojia.
11.Serikali haina cha kupoteza kwa kufanya hivyo maana watumishi wa Serikali ni wachache sana hawafiki milioni moja,wakati watanzania wote tunakaribia milioni 60.
12.Kunaweza kuwa na option kwa maeneo mengine ya kitaaluma ambayo ni gharama kwa nchi.
TUJADILI BILA KUWEKA MASLAHI BINAFSI MBELE.