Serikali inaweza kulinda madaraka yake?

Serikali inaweza kulinda madaraka yake?

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2022
Posts
289
Reaction score
489
"Serikali ni watu waliochaguliwa na watu kwa manufaa ya watu"
Kwa mantiki hii serikali ni mali ya wote na haipaswi kumilikishwa kwa watu wachache.

Kikundi cha watu "Chama Cha siasa" kinachoshinda kuongoza serikali hakipewi hatimiliki ya taifa kuwa kitaongoza milele.
Iwapo serikali itawajibika kutenda sawasawa na yale umma unataka basi itajikatia tiketi ya kuongoza milele hata pasipo mabadiliko yoyote.

Lakini ikifika wakati serikali haitendi yale wanayoyataka wananchi basi wananchi watatwaa nchi yao na kukabidhi kwa watu wengine ili wasimamie mambo yaende sawa.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema iwapo wananchi wataona mambo hayaendi sawa ndani ya serikali watatwaa nchi yao. hii inamanisha kuwa serikali nguvu ya serikali ipo mikononi mwa wananchi wenye nchi yao.

Je serikali inaweza kulinda madaraka ambayo wananchi wanataka kuyatwaa mikononi mwao?.
Wananchi wakichoka na muenendo wa serikali yao hakuna anayeweza kuwazuia wataitana kwa nguvu na wataitwaa nchi yao kutoka kwa serikali iliyowapuuza na kuyumbisha maisha yao.

Hakuna serikali duniani iliyoweza kuwadhibiti wananchi walipoamua kusimama kwa pamoja na kudai mabadiliko.

© Peter Mwaihola
 
Back
Top Bottom