Serikali inawaibia watumishi, watumishi wanaiibia serikali. Nini suluhisho?

Usitetee ujinga mkuu tuna marafiki na ndugu zetu hasa kada ya elimu baada ya siku mbili za kupokea mshahara anakufata na kukupiga mzinga umpe buku tano, una shangaa jamaa kapokea kabla yangu na mshahara ananizidi lakini hana pesa.

Mikopo na maslai duni ndio vyanzo vya maisha magumu ya watumishi wengi na ni kweli wengi ni wapigaji ndio utaona ana nyumba mara gari.
Kwa mtumishi wa kawaida kama hujapiga dili huwezi kumiliki gari. Nikisema gari namaanisha gari sio hizi za ml.3 za kumnyang'anya mbongo mwenzako.
Ni nani akope akatwe miaka 5 kisa gari huku anajua kuwa ataishi kwa msoto mpaka deni liishe?.
Kama unamadili unayapiga huogopi makato yoyote
 
Hulka ya wizi ni jadi yetu,hata watafiti wa nje waligoma kuamini kwamba mishahara ya umma kuweza kukidhi yaani ikutane mwisho wa mwezi. Serikali inawaibia watumishi,watumishi nao wanaiibia serikali either dili au mda kwa wasiokuwa na madili.Mtumishi nae anaibiwa na mfanyakazi wa nyumbani kwa kubana matumizi ganji hata kuwalisha watoto viporo au kununua masalo,mboga zilizolala hata kama akibaki na buku kwa mwezi ni nyingi.
Dawa ni kupiga dili tu
 
Kuna kipindi nilikuja likizo Dar. Sasa katika kusalimia salimia ndugu jamaa na marafiki, nikakutana na jirani yangu wa zamani sana, dogo tumekua pamoja.

Akafurahi sana kuniona baada ya miaka zaidi ya 10 nilikuwa sijaonana naye.

Nikawa nalalamika vurugu za uendeshaji magari Dar. Nikawa natafuta mtu wa kuniendesha.

Akaniambia usiwe na shaka, nitakuzungusha Dar ujisikie uko likizo. Akanipa miadi tukutane anipe kijana dereva aniendeshe mjini. Ilikuwa nina hamu ya kuona Sabasaba imeendeleaje baada ya miaka zaidi ya 10 bila mimi kuwa Dar. Basi tumekutana, nikafikri ananipa dereva halafu yeye tutakutana jioni (alikuwa kazini). Kumbe mwenzangu naye anajiunga kwenye msafara.

Sasa mimi nilikuwa likizo, naweza kuranda mchana, yeye anatoka kazini anaaga ilikuwa kama saa tano sita hivi. Nikamuuliza, unaondoka kwenda lunch halafu utarudi? Akasema hii kimoja hii.

Nikamuuliza, hapa kazini kwako (shirika moja kubwa sana la umma) haitakuwa noma unaondoka kihuni hivi bila udhuru wala ruhusa?

Akasema wao wana "system" ya kulindana, hivyo hakuna neno. Akiondoka wenzake watamlinda, na yeye huwa anawalinda hivyo hivyo.

Huyu ni kijana ambaye alililia sana kupata kazi, akapata hiyo kazi, sehemu nzuri sana. Hata mishahara yao si mibaya hivyo.Kwa viwango vya Tanzania ni moja kati ya mashirika ya umma yanayolipa vizuri kabisa.Alivyopata kazi akawa kabadilika.

Mpaka haya nikaona mimi anavyotoka kazini yeye.

Nikakumbuka msemo mmoja ulisemwa kuhusu wafanyakazi wa serikali.

Wanasema kwamba "serikali inatudanganya kwamba inatulipa mshahara, na sisi tunaidanganya tunafanya kazi".

Nikakumbuka wimbo wa Profesa Jay wa "Bongo Dar es salaam" aliposema kwamba, aliye uziwa dhahabu bandia, amepewa pesa bandia, mambo yamekuwa droo.

Tatizo ni kwamba, kwa huyu kijana, sifikiri kwamba alilipwa mshahara mdogo. Hilo shirika alilofanyia kazi ni kati ya mashirika ya umma yanayolipa vizuri kabisa.

Mara nyingine hii hali inakuwa ni utamaduni tu.
 
Kama nimekuelewa vile mwanajamii mwenzangu
 
Back
Top Bottom