Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,955
Habari wanajukwaa!
Ninapenda kueleza au kuonyesha jinsi serikali inavyowaibia watumishi nao watumishi wanavyogeuza kibao na kuanza kuiibia serikali na mwisho wa picha kila mmoja anamlalamikia mwenzake kwamba hajatimiza wajibu wake. Kile kitendo cha mtumishi au serikali kutokuwajibika vyema kwa mwenzake ndio ninakiita wizi. Naomba nisieleweke vibaya.
Nambari 1: SERIKALI INAVYOMWIBIA MTUMISHI.
Hapa simaanishi kuwa serikali inavamia na kumpora mtumishi au kumchukulia mali zake kimya kimya la hasha. Pale serikali inaposhindwa au inapogoma kumlipa mtumishi wake mshahara ambao ungemfanya aishi mwezi mzima bila stress, inaposhindwa kumpangia nyumba ya kuishi au kumkopesha fedha ya ujenzi hapo tunasema serikali imemwibia mtumishi kwa kutumia mamlaka yake. Mtumishi anapokosa usafiri au nauli ya kumfikisha kazini hapo tunasema mtumishi ameibiwa muda wake.
Mfano: Mtumishi anayelipwa around 300,000 - 1M unadhani take home yake itakuwa sh.ngapi?
Je, huyu hataiba muda wa serikali, hatadokoa % ikiwa yeye ndiye signatory wa manunuzi?.
Ikiwa mtumishi anasimama kwenye daladala Gongolamboto hadi posta mpya huyu atahudumia wananchi kwa upendo na furaha?. Lazima aangalie huku na kule ili apate fedha ya kujikimu nyumbani na nauli ya jioni.
Nambari 2: Hii nimeigusia hapo juu.
Mtumishi au watumishi wengi wa umma ni wezi. Kazini wanawaza kupiga dili tu ili wajikwamue kimaisha. Kile cheo au nafasi iliyomkalisha ofisini ni kama rehani tu kwake. Ile kazi aliyoajiriwa nayo inakuwa nambari 2 na nambari moja ni kupiga dili.
Kuna sekta kama elimu hasa walimu hawa hawana mazingira ya kupiga dili kulingana na mazingira yao badala yake huiibia serikali muda na kwenda nje kujitafutia riziki. Pia huiibia serikali kwa kutoa elimu duni kwa wanafunzi. Inafika wakati kijana wa kidato cha 4 wa st. Kayumba anazidiwa uelewa na mtoto wa darasa la 5 wa St.Marry.
Miradi haikamiliki kwa wakati kwasababu ya wizi wa watumishi wa umma.
Note: Serikali ndio inapaswa kuwa ya kwanza kuwajibika kwa watumishi then watumishi wawajibike kwa serikali.
Majuzi nilichukua risiti za Bank kama 2 walizozisahau watumishi kwenye ATM, zinatia aibu.
Mtumishi anakimbia kuelekea kunako ATM mshahara umetoka kumbe kuna laki na thelathini tu. Huyu mtu analipwa kiduchu sana hata kama amekopa bank. Yaani 130000 ndio 1/3 ya mshahara wake.
Vuta picha huyu anasomeshaje, anakulaje ndani ya mwezi mzima, anasafiri vipi?