Serikali inavunja ndoa za watumishi wake

akajasembamba

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
1,004
1,471
Miaka ya mwanzo ilikuwa utaratibu wa lazima kwamba mume ambaye ni mtumishi wa Serikali anapohama basi lazima mkewe kama naye ni mtumishi anapoomba kumfuata huko alikohamia lazima apewe naye transfer kumfuata, lakini kwa sasa utaratibu huo umekufa kabisa. Spouse anapoomba kumfuata mwenza wake hujibiwa hakuna nafasi na atapewa vitisho kwamba achague kazi au mume! Lakini hapo hapo watumishi wengine wenza wao wanapohamishwa na wao wakiomba uhamisho maombi yao hukubaliwa haraka haraka.Uhamisho wa sasa unafanywa kwa kujuana, upendeleo,rushwa(ya pesa na ya ngono) Maana ya NDOA ni kuishi wawili sasa ni NDOA gani ambayo Mume Yupo Mtwara na Mke Kagera! Au serikali yenyewe inaona wenye haki ya kuishi na wenza wao ni vigogo tu ambao wake zao hutafutiwa nafasi popote pale waume au wake zao vigogo wanapohamia lakini watumishi wa chini huambiwa hakuna nafasi na hukaa miaka tele mbali na wenza wao. Kuna matukio ya wakubwa kuwahamisha waume vituo ili wapate nafasi za kujivinjari na wake wa watumishi hao. Serikali inajua kuajiri tu watumishi bila kujali hao watumishi nao walizaliwa na wanahitaji malezi ya wazazi wawili! Mtu anapokaa mbali na mwenza wake obviously ataelemewa na vishawishi ambavyo kama angekuwa na mwenzake angeweza kuvihimili, katika zama hizi za ukimwi tuzidi kuona siyo kuvunjika ndoa tu ila vifo zaidi!
 
Umetonesha vidonda maan wengine tangu tuoe hatujawahi kuishi pamoja na familia zetu kwa sababu ya kazi. Serikali iangalie upya suala hili vinginevyo.......
 
Vishwawishi vya nini wakati unatoka kazini hoi unafikia kupika maana mkeo hayupo??? Mie nadhani unavitafuta mwenyewe hivyo vishawishi maana kama utatoka kazini hoi ukafikia kuoga, kupika, kula na kulala sidhani kama utavipata vishawishi maana naona ni ngumu mie mbona naweza wajameni????
 
jamani mazingira ya kisera yaliyokuweepo nyakati hizo za nyuma yameishabadilika. pia ni muhimu tujifunze kuwa na self control kwenye mambo ya mapenzi.
 
Hayo mliyoyasema dada zangu yatawezekana iwapo hormones za uzazi za huyo aliyehamishwa mbali na mwenzi wake zitasimama kufanya kazi kwa kuwa yuko mbali na mwenzi wake, vinginevyo hii kitu ni "next to impossible".Mbona wao wanaohamisha wenzao hawakai mbali na wake au waume zao,si wangeonesha mfano kwanza wao?
 
Ndugu umeongea point ya msingi sana, naomba hili lisiongelewe tu hapa jf bali liwekwe wazi hata kwenye vyombo vya habari vingine maana hii inauma sana! Imefikia sehemu vijana wengi wanaogopa kuoa wafanyakazi kwa sababu ya kuhisi kwamba watamis haki yao ya ndoa make mwanaume akiwa mtwara mke kagera kuonana itachukua muda sana!
 
Sidhani kama ni kweli kwa kila mtu. Kwako inawezekana lakini kwangu haiwezekani na ndio sababu ya kuwepo mume na mke. Zaidi ya hapo ni kuhujumiana na kudhulumiana tu
 
Ndugu umeongea point ya msingi sana, naomba hili lisiongelewe tu hapa jf bali liwekwe wazi hata kwenye vyombo vya habari vingine maana hii inauma sana! Imefikia sehemu vijana wengi wanaogopa kuoa wafanyakazi kwa sababu ya kuhisi kwamba watamis haki yao ya ndoa make mwanaume akiwa mtwara mke kagera kuonana itachukua muda sana!

Sitii neno hapo!
Kweli...kweli...kweli .
 
Mkuu mazingira ya sasa yamebadilika kubaliana nayo tu na muamini mkeo au mumeo basi. Kuhusu sijui uko Kagera na wewe Mtwara. Kuna jamaa yangu mie anafanya kazi Dar na Mkewe yupo Japan sasa huyo unasemaje? Come on grow up and get a life!!!
 
Eti ee?
 
Vishwawishi vya nini wakati unatoka kazini hoi unafikia kupika maana mkeo hayupo??? Mie nadhani unavitafuta mwenyewe hivyo vishawishi maana kama utatoka kazini hoi ukafikia kuoga, kupika, kula na kulala sidhani kama utavipata vishawishi maana naona ni ngumu mie mbona naweza wajameni????

Denamsi,hivi unarudi kazini hoi alafu mama mwenye nyumba/mtoto wake wa kike anakupokea na kukupa msosi,lazima uingie kishawishini.
 
Issue hii ni nyeti na sio suala la kuangalia mke na mme tu na mambo ya kutiana, kuna issue ya watoto ambayo kwangu ni muhimu sana. Child development ni muhimu sana, na role ya baba na mama ni nguzo kuu.

Wewe unayetoa mfano wa mme Dar na mke Japan na kufananisha issue ya Mtwara vs Kagera ni wazi hujui usemalo.
 
Hayo mliyoyasema dada zangu yatawezekana iwapo hormones za uzazi za huyo aliyehamishwa mbali na mwenzi wake zitasimama kufanya kazi kwa kuwa yuko mbali na mwenzi wake, vinginevyo hii kitu ni "next to impossible".Mbona wao wanaohamisha wenzao hawakai mbali na wake au waume zao,si wangeonesha mfano kwanza wao?

haswa kama huwa unakula na kushiba
 
Huo utaratibu haujafutwa. Slogan iliyopo ni kwamba si lazima mke tu bali mume anaweza kumfuata mke. Naona mtoa mada mada kazungumzia upande mmoja tu. Na wewe mume kwa nini ukubali kuhama, kwa nini usiwe wa kwanza kukataa kama unaipenda familia yako. Tatizo ile dhana ya kuwa mwanamke ndo anamfuata mume inasababisha yote haya.
 
We mwenzio hapo alipo tayari ana maumivu yakumkosa mamaa alafu unataka kumuongezea presha juu?Muonee huruma bwana!
lizzy hujambo? Username yako ilikuwa ni kifupisho cha mpenzi wa zamani ndo maana nalipenda. Alikuwa amefungasha huyo, usipime!!
 
Back
Top Bottom