Serikali inapowanyima wananchi kutumia raslimali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali inapowanyima wananchi kutumia raslimali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Alexism, Sep 17, 2011.

 1. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Miaka mingi imepita serikali nchini ya uongozi wa ccm kuwanyima na kuwakataza wananchi kutumia ziwa victoria kupata kitoweo muhimu samaki kwakuwapa wawekezaji wakishirikiana na polisi mamlaka ya kuwakataza wananchi kuvua samaki huku wakisingizia eti wabongo unafanya uvuvi alamu.

  Katika harakati la kutekeleza hayo doria na misako ilianza vijijini hasa vilivyo karibu na ziwa, kwenye masoko au magurio pamoja na ziwani.
  Nikilitokea mpaka leo tunaskitika na kubaki maskini na kuliangalia ziwa kama rahana kwetu.

  Kupitia hizo oparetion mfano kwetu BK tuliita KAYUNGI kwakuwa jamaa aliyekuwa mstari wambele arijulikana hivyo

  1.Ajira zimepungua hasa kujiajiri

  2.Vifo vya wavuvi hasa majini sababu ya purukushani

  3.Umaskini umeongezeka hasa wa kipato

  4.Kupanda gharama za mboga

  5.Wananchi kugeuka wanyama wala mabaki scavanger(MAPANKI)

  6.Wavuvi kupata vilema vya kudumu sababu ya kupigwa

  7.Ongezeko la ualifu kwani ajira hamna

  8.Familia kutengana au kutelekezwa kwani maisha magumu

  9.School drop-out kwani wazazi hawamudu mahitaji ya shule

  10.Kuwazalilisha wananchi kwa kupigwa na kula mapanki

  11.Ukiukwaji wa haki za raia na binadam

  JE HAYA YAENDELEE AU YAKOME NA NANI WAKUWAJIBIKA NA KUWAJIBISHWA KWA HAYA.

  Nawasilisha
   
 2. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  1. Hakuna sehemu yoyote ya Ziwa victoria ambayo ameruhusiwa kuvua mgeni(sio raia), wafanyabiashara ya kuchakata samaki (fish proccessors) hawaruhusiwai kuvua kwa mujibu wa sheria wavuvi wanao ruhusiwa ni watanzania wa kawaida na ndiyo wanaovua.
  2. Ajira kwa ziwa victoria imeongezeka zaidi mwaka 2004 kulikuwa na wavuvi 30,000 mkoa wa kagera 2010 wako wavuvi zaidi ya 70,000 (Source Fisheries Frame Survey, 2004 and 2010)
  3. kupanda gharama za mboga hiyo ni kutokana na market forces na exchange rates kwani sangara ananunuliwa kwa Dola (main Fisheries Produce Export in Lake Victoria)
  4. Toa takwimu wavuvi wangapi wamepata vilema vya kudumu kutokana na kupigwa kwenye Operation Kayungi
  5. Hakuna ukiukwaji wowote wa haki za raia uliokuwa ukifanyika kataika operation hizo kwani kulikuwa na Mahakama ikiendesha kesi hizo na kuna watu waliokuwa wakiachiwa huru baada ya kutopatikana na hatia.
  Fanya utafiti kabla ya kuzungumza hali ya upatikanaji wa samaki imepungua kwa sababu uvuvi unafanyika kwenye eneo hilohilo na idadi ya wavuvi inaongezeka kwa hiyo output/person imeshuka kutokana na kuongezeka kwa wavuvi8 na eneo la kuvua ni limited haliongezeki. Upungufu pia unatoikana na samaki kuwa na soka kubwa nje ya mkoa na nje ya nchi.

  (Nimeshiriki hizo operation 2004-2009 mie pia ni mwana harakati sikuwa tayari kuona uvunjifu wa haki za binadamu ukifanyika)
   
 3. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Mkuu sikushangai kabisa kusema hivyo kwani posho uliyokuwa ukipewa inakufanya useme hivyo.
  1.Ajira unasema zimeongezeka duh ama kweli kijiji chetu Maruku walio kuwa wanavuvi takribani 35 leo watano ndio wanaendelea na hiyo kazi ndo ongezeko la ajira mkuu
  2.Ukiukwaji wa haki za raia na binadamu ni pamoja na vitisho,kupiga pamoja na kuchoma nyavu na mitungi bila fidia
  MKUU nakuomba utuambie masoko yaliyo kuwa maarufu kuhuza mboga hiyo kwa raia wenye kipato kidogo leo mangapi yanafanya kazi,mfano AMUGEGE -ITAHWA,Maruku,Kabugaro,Gera-Katoma,Kemondo, nk.Je wananchi wa Bukoba mfano wanakula mapanki au hamna,je niuzalilishaji au nikanuni za soko horera?Wananchi hao wakitaka hiyo minofu ni mahari gani waipate na gharama yake? Hizo data za kupika na Vic fish zimejumuisha wote walioajiliwa na ambao wamejiajiri na watu wangapi walikuwa wanafanyakazi ya uvuvi kabla ya operation Kayungi na wasasa nimekupa mfano kijijini kwetu.
  Tunawajua nyinyi ambao mnajiita wanaharakati kumbe mnatafuta ugali na data zenu zisiso reveal ukweli ila kuwasaidia kupata ugali na kuwaadaa wananchi.Lkn ata mkuu wa inji aliwai kataa kuwa hakuna mtu anayekula mabaki ya mifupa ya samaki na kusema wanaokula ni wendawazimu,tunashukuru kwa matusi hayo sisi tutakula ila mwisho wake hautakuwa mzuri.Tetea tena mkuu na data zako.
   
 4. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Masoko ya ndani yameshindwa kuhimili kwa sababu ya bei ya viwandani ni kubwa kwa hiyo wavuvi wanpeleka samaki zao viwandani, kuuza samaki mmoja kwa 1000(tsh) sokoni au kuuza Kilo ya samaki Kagera fish 2800 (tsh) hata ungekuwa wewe unafanya biashara ungeuza wapi?
  Leo ukiangalia maendeleo ya watu binafsi wengi wa Bukoba kuanzia Mwalo wa Kabidi hadi Kyasha yametokana na Uvuvi.
  Uvuvi huu usiokuwa regulated umesababisha kupungua kwa samaki mfano mwaka 2004 kulikuwa na samaki sangara zaidi ya tani 700,000 ziwani mwaka 2009 kulikuwa na samaki sangara 314,000 hii inatokana na kuvua bila kikomo na kuvua samaki wachanga matokeo yake ni kuisha samaki, mwaka 2004-2009 hakuna hata mtumbwi mmoja uliochomwa na nyavu zilizochomwa ni zile zlizokuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria ya uvuvi na. 6 ya 1970 na baadaye sheria na. 20 ya 2003
  Ni kweli mapanki yanaliwa na wananchi, ila siyo yalioza, kuna mjasiliamali mmoja pale Buhembe (kama sikosei) anatengeneza hayo mapanki kwa kiwango cha hali ya juu na mwingine yuko Kyakairabwa wote hawa wanauza ndani na nje ya nchi hayo mapanki
  Data hizo hazihusiani na Vic fish kwani vic fish imeanza kazi kagera Nov 2007,
  Niliondoka kagera 2009 sijafika huko hadi
   
 5. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  nguvu tunazo,uwezo tunao na nia pia tunayo lakini hatupewi dhamna hiyo
   
 6. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Hampewi dhamana kwasababu mnamwagia watu tindikali
   
 7. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Mkuu tunaposema MAPANKI maana yake ni mabaki ya mifupa ya samaki ambayo wewe umeyasifia eti yanatengenezwa kwa uzuri,lini mabaki au mizoga hiyo ikawa mizuri acha kututonesha vidonda.
  Labda nikupe taarifa ambazo ata wewe wawezekana ulipewa lkn usingeweza kuzitoa.Polisi wakimkuta mtu anawauzia samaki tena ambao ni wakubwa wanamunyanganya hao samaki na kuwaza kwa wafanyabiashara wanauza viwandani this eye witness KYASHA-BUHEMBE.Je unajua kuwa hata hayo mapanki polisi walikuwa wakikukuta nayo unanyanganya na yanamwagwa chini mpaka tulipo piga keleke kuhusu ili.
  Mkuu tunaposema wananchi kupata benefit kutoka kwenye rasilimali ni pamoja na kuitumia hiyo resource,kuhuza maana kipato nk.
  Unabidi ujue kuwa sisi waanga wa haya matukio na sera pamoja na data za kupika ni sisi wala nyie wakuja mnachukulia kawaida.
  Kwa sasa hakuna mwananchi mwenye kipato cha chini anayemudu kula samaki ata na mapanki hayo ni issue.DAGAA WATAKASIRIKA SIKU SIYO NYINGI TUTAENDA VIC FISH,KAGERA FISHARIES KUKACHUKUE MINOFU TUWACHIE MAPANKI.
   
 8. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  kwa hali hii nadhani tunaweza kuelewana maana isue yako ilikuwa kuwazuia watu kuvua ziwani, lakini comment yako unasema POLISI wana wanyanganya na kuuza huo ni ubadhirifu wapolisi kama kawaida yao au wakubambike bangi, au kesi yoyote nakubaliana nawe ila Idara ya Uvuvi inayosimamia uvuvi iko makini haijawahi kuwaagiza wafanyakazi wake wawanyang'anye wavuvi samaki aliyeidhinishwa labda awe amevuliwa kwa utaratibu usioruhusiwa na kuhifadhiwa ikitoke akifanya kinyume chake hatua huchukuliwa (kagera zilichukuliwa hatua 2006). Nakushukuru kwa kupiga kelele na leo kuna mabadiliko kwenye mapanki (maana samaki wote ni mizoga hufa bila kuchinjwa), kwani tumeshiriki kuyafanya yawe kama ilivyo sasa. Suala la kwenda Vicfish na Kagera fish kuchukua minofu nalo siwezi kulisemea ni uamuzi wa wananchi maana hata Libya wamekwenda Ikulu wakachukua nchi.
   
 9. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Unataka ulipwe kwa kutumia kokoro?
   
 10. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Acha kupotosha mada!
   
 11. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Maada itabaki pale pale hachana na hawa wapotoshaji.
  Mkuu kampuni gani inayosafirisha mapanki kwenda kuwauzia wazungu?Nimekuuliza masoko mangapi bado yanafanya kazi yakuwauzia wananchi samaki alafu mialo mingapi inamilikiwa na wananchi ambayu ilifungwa na imefunguliwa?Mzee wadata wangapi wamewezeshwa katika mpango huo ili kuweza kuvua kwa utaaram na kiasi gani cha samaki ambacho kimenunuliwa na wananchi kama kitoweo?
   
Loading...