Serikali inakigugumizi gani juu ya migogoro ya wakulima na wafugaji, Morogoro

philltaya

Member
Sep 5, 2015
53
11
Najiuliza hivi serikali inajua kinachotokea Morogoro kupigwa kwa wakulima wawili na wafugaji kwa vijiji viwili tofauti mmoja Doma na mwingine Menge/Vianzi wilaya ya Mvomero? Wafugaji nguvu ya kufanya hivyo wanaitoa wapi?

Kuna mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa tafadhari tupieni sana jicho wilaya ya Mvomero hasa kijiji cha Menge/Vianzi wafugaji wanafanya makusudi kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima na ukatili mkubwa na sheria zinaonekana kama hazina meno kwao.

Nimetuma post hii kwa uchungu kwakuwa kijiji hiki hakijafikiwa na serikali kikamilifu na ndiyo maana wafugaji wanapuuzia matamko ya serikali, na kufanya ukatili kwa wananchi, kiongozi wa kijiji ni wa hovyo kabisa na ndiyo huyo huyo amepita kwenye kura za maoni kiongozi atakaye ona hii post tafadhari tuondolee uzia hapo kijiji kwetu, ardhi ni nzuri kwa kilimo chochote lakini hatuwezi kufanya shughuli za kilimo ipasavyo kwakuwa ng'ombe zinashinda mashambani na mapoli yapo.

Ni mimi mkulima sina pa kupazia sauti yangu zaidi ya jukwaa hili
 
Back
Top Bottom