Serikali inaiua historia ya Dar es salaam

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,246
401
Kila kukicha majengo marefu yanashindana kuibuka katika jiji la DSM! Yanaweza yakawa ni maendeleo ; lakini ama kwa makusudi kabisa (na ndivyo ninavyoamini) au kwa kutojua maendeleo haya yanaua historia ya Jiji letu la DSM.

Ni jambo la kushangaza majengo haya marefu na mapya yanaibuka mahali ambapo majengo ya zamani, yaliyojengwa kwa ufundi mkubwa na ‘design' ya aina yake, yamebomolewa!! Uko wapi uhifadhi wa historia ya Dar es Salaam?

Miji mingi mashuhuri duniani imehifadhi historia ya miji hiyo na vimekuwa ni vivutio vya utalii kwa nchi husika. Watu wanatembelea nchi hizo kuangalia, pamoja na mambo mengine, majengo ya zamani yalivyo sisi tunayabomoa!!! Kwa mfano, Zanzibar kuna mji mkongwe, India kuna Old Delhi na New Delhi, Ubeligiji kuna old Brussels na New Brussels, Cyprus kuna New Nicosia na old Nicosia miji hii imewekewa sheria ya kuihifadhi lakini Dar-es-Salaam sehemu ambayo ingekuwa old Dar es Salaam inabomolewa kwa kasi ya ajabu! Maofisi yanaendelea kulundikana sehemu moja na kusababisha msongamano mkubwa barabarani wakati ambapo mji ungeweza kupanuliwa, maofisi yakasambaa, msongamano wa magari ukapungua, na mji mkongwe wa Dar es Salaam ukawepo na kuhifadhiwa kuwa kivutio cha watalii. Hivi serikali yetu ikoje?
 
Ningekuwa cartoonist ningechora afisa wa mipango miji akiwa na masikio yaliyozibwa na dollar. Lugha yao ni hela sio historia, historia haiwezi jenga nyumba, haiwezi somesha mtoto, haiwezi nunua gari. Lakini at the botttom line ni mfumo uliopo sasa hivi from top to bottom money is da language
 
Hii ndio safari ya kuua historia na utalii kiujumla, vizazi vyetu vitaambulia historia tu.
 
Hii ndio safari ya kuua historia na utalii kiujumla, vizazi vyetu vitaambulia historia tu.
hapo kwenye red ni Historia ya kwenye vitabu tu. Vizazi vyetu vijavyo vikitaka kuona historical sites itabidi waende Zanzibar; Dar mji utakuwa mpya kila siku.
 
Back
Top Bottom