Serikali inahusika kujenga minara ya simu?


tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Messages
14,929
Likes
5,125
Points
280
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2008
14,929 5,125 280
Juzi wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu bungeni, mbunge mmoja anaitwa Kakoso (sijui anatoka jimbo gani) alimuuliza waziri wa mawasiliano na uchukuzi Prof Makame Mbalawa ni lini serikali itajenga mnara wa simu kwenye vijiji fulani vilivyopo jimboni mwake.

Prof Mbalawa akamjibu kwamba serikali 'ipo kwenye mchakato' wa kutumia hela za ndani kupeleka mawasiliano kwenye vijiji hivyo.

Hivi serikali inahusikaje ktk ujenzi wa minara ya simu za mkononi kama sio kuwapaka wananchi mafuta kwa mgongo wa chupa?
Ni lini hasa serikali itaacha kuwadhihaki wananchi kwa kuwaona mazezeta?

Minara ya simu inayojengwa na makampuni ya simu husika (vodacom, airtel, tigo, zantel, sasatel, etc) inaingiaje kwenye siasa uchwara za serikali?
 

Forum statistics

Threads 1,250,604
Members 481,419
Posts 29,738,564