Serikali Impe Ulinzi Said Bahanuzi!

Serikali Impe Ulinzi Said Bahanuzi!

Jamani TUACHE UTANI KWENYE MAMBO YA MUHIMU. KUNA WATU WANAHASIRA NA BAHANUZI BALAA KWA KUKOSA PENALTY JANA.WANAWEZA KUMDHURU JAMAA KWA HIYO SERIKALI INA JUKUMU LA KULINDA WANANCHI WAKE!! NATOA HOJA.

hao watakuwa wajinga tu,kwan n yeye peke yake aliyekosa penati?kwann wasiwadhuru wale waliosababisha mpaka wakafika penati ya sita?wanaofikiria hayo ni wajinga wanywa viroba
 
Mi nashauri wamuache huko huko,maana kiukweli m ndo mtu kwanza kuwa na hasira nae
 
Tutamkalia kikao kumjadili wakiwekwa bench wanalalamika wakipewa nafasi mchecheto kibao

tena ingalikuwa ni mimi ile penati ningeitifua juu zaidi ya pale pembeni alipopiga. Yaani nyie mnaona game la kumpima bahanuzi ni ile ya jana. AkAE BENCHI MECHI KARIBU ZOTE ZA LIGI HAAFU ACHEZE GAME GUMU KAMA LILE KWA NINI ASIWE NA MCHECHETO!!!!! TUKUENI BANA. NYIE VIPIIIIII. ACHENI HIZO. MUACHIENI UHAI WAKE BANA SIYO FRESH. HATA KATIBA INATOA UHURU WA KUISHI.
 
yanga hatuna mambo hayo ya jabu tunajua mpira ukoje,hakukusudia kukosa so tutamsamehe bure kwenye penalty kuna mambo mawili kupata na kukosa,wanakosa akina ronaldo na ronaldinho na wanasamehewa itakuwa yeye!!!


asamehewe kwa kosa gani?
 
kwa baadhi ya comment za wachangiaji wanafikiri kukosa penalty ni kosa kumbe ni moja ya matokeo ya mchezotu

Watakuwa wanakosea sana. kwa namna alivyoipiga ile penati alidhamiria kufunga ila ikaenda nje. sometimes kuna kijiuzembe hutokea hasa kwa wale wanaotaka kupiga penati kwa madoido sana mara nyingi hukosa na kimsingi huwa wanakuwa wamrfanya uzembe kwani hata upigaji wa penati una principles zake
 
Watakuwa wanakosea sana. kwa namna alivyoipiga ile penati alidhamiria kufunga ila ikaenda nje. sometimes kuna kijiuzembe hutokea hasa kwa wale wanaotaka kupiga penati kwa madoido sana mara nyingi hukosa na kimsingi huwa wanakuwa wamrfanya uzembe kwani hata upigaji wa penati una principles zake
by the way nia yake ilikuwa ni kufunga not otherwise.
 
ndo mana mimi sipendi kucheza mpira, tangu nione yule mchezaji wa Colombia (Eskoba) ameuawa kisa tu kajifunga kwenye kombe la dunia, sitaki kifo cha kijinga.

Yani ni bora niende kuandamana na CDM ili polisi waniue kwa risasi au bomu kuliko kuuliwa na mashabiki wenye hasira
 
Sie Simba tunashangailia tu, manake mkitaka kuvunja recodi yetu tuliyoweka kule Misri miaka kadhaa iliyopita tukatinga semis...So bora mmefungwa manake maneno yangezidi huku kitaa....Mukiuana mtajuana wenyewe, records zetu nje ya mataifa bado UNBREAKABLE.
 
Yule kocha Mbelgiji wa Yanga, Tom Saintfiet, alisema kuna wachezaji Yanga kazi yao ni kubadili mitindo ya nywele tu, na alikuwa anampiga kijembe Bahanuzi!
 
Sie Simba tunashangailia tu, manake mkitaka kuvunja recodi yetu tuliyoweka kule Misri miaka kadhaa iliyopita tukatinga semis...So bora mmefungwa manake maneno yangezidi huku kitaa....Mukiuana mtajuana wenyewe, records zetu nje ya mataifa bado UNBREAKABLE.
mlipofika nusu fainali mlipewa zawadi gani??
 
kwani Bahanuzi ndie pekee aliekosa penati katika mechi ile? Acheni ungese wa ku mnyanyapaa Bahanuzi.
 
Kuna vitu kiukweli hua vinatia sana hasira,kinachotakiwa ndugu zangu watani zangu ni kushukuru tu na kuangalia yajayo.hata hivyo mnahitaji pongezi za dhati.
 
Kaulize Benchi la ufundi. Manake hata records haujui maana yake.

kwa hiyo mliweka rekodi tu. hamkupata zawadi yeyote(teh teh).watu wanaweka rekodi kuchukua makomba nyie mnaweka rekodi kuingia nusu fainali.
 
Habari ndiyo hii…
 

Attachments

  • 1394446463411.jpg
    1394446463411.jpg
    54.8 KB · Views: 103
Mnamuonea bure Bahanuzi, tena wengine wameenda mbali wanadai eti si raia!. Mbona Twite kakosa? Oscar Joshua je? Kanda2 ovyo sana
 
Back
Top Bottom