Serikali imeziagiza mamlaka za miji nchini kuwavunjia watakaojenga maeneo yasiyopimwa

nanawoo

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
1,268
1,215
lukuvi2.jpg

Serikali imeziagiza mamlaka za miji nchini kuwavunjia mara moja watu ambao wananzisha ujenzi katika maeneo ambayo hayajapimwa kwani kwa sasa Serikali imeweka mazingira rafiki ya watu kumiliki ardhi.

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe.Willium Lukuvi ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea taasisi ambazo zipo chini ya wizara yake na zinashiriki maonesho ya biashara ya Dar es Salaam.

Nao baadhi ya wasimamizi wa Taasisi hizo ambazo ni Shirika la Nyumba la Taifa na kampuni ya Nyumba ya Watumishi wamesema wamekuwa wakifanya kazi zao kwa weledi ili kuwapatia Watanzania makazi bora.

Chanzo:ITV
 
Waache kutafuta kiki kwa sehemu zisizo na kiki. Data huu ni ulevi wa Madaraka. Hebu niambieni mini IPI, majiji yapi, na mikoa IPI ilishafanya upimaji maeneo yao yote hats kuzunguka eneo LA mji wenyewe? Mifano: Dar es Salaam imepimwa kwa asilimia ngapi? Arusha, Mbeya, Kwanza na Dodoma tuu he, imepimwa kwa kiwango gani? Unakuta hats eneo lililopo 10Km kutoka katikati ya mji halijapimwa. Chamsingi wapime kote then watu washindwe kuendeleza. Kingine kwa maeneo yaliyopimwa mfano ulikuwa na shamba, kimantiki wakupe offer ya kulipia gharama ya upimaji tu, ila kinachoendelea ni manyanyaso kwa wananchi, vinatoka viwanja 4, anapewa kimoja tena akilipie kama ananunua, huu ni uonezi sana
 
Hii nchi rahisi sana kutengeneza waasi hawa wanasiasa ndio watunga sera na wapanga kila kitu wanaachia kutekeleza mipango miji hadi raia wanajenga tu nao wanachukua kodi na majengo kila mwaka! Baadae mtu anaibuka tu eti wavunjiwe. Hivi hawa mbwa wanajua ni kiasi gani watu wanatafuta pesa kwa ajili ya kukidhi mahitaji unajibana sana hata mtu kufikia kujenga? Ipo siku yao
 
Kwa huko Daressalam sidhani kama itabakia nyumba (ila chache tu ),kama watasema wafanye ivyo
 
Nafikiri hawa mawaziri na mabosi wao hawajui kinachoendelea huku chini... Nafikiri waziri Lukuvi atafute ndugu yake asiye na ubini wa jina la Lukuvi amtume aende ardhi ajaribu kufuata hizo taratibu na gharama halafu aone majibu yake...
 
Yaaniii ni maajabu ya karne,Kimara Bonyokwa toka tupimiwe mwaka 2012 mpaka Leo atuelewi hatma yetu, wamepima wamevuluga mpaka Leo awajarudi wengiwao tunaona siasa tu za viongozi!

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
 
Hii nchi rahisi sana kutengeneza waasi hawa wanasiasa ndio watunga sera na wapanga kila kitu wanaachia kutekeleza mipango miji hadi raia wanajenga tu nao wanachukua kodi na majengo kila mwaka! Baadae mtu anaibuka tu eti wavunjiwe. Hivi hawa mbwa wanajua ni kiasi gani watu wanatafuta pesa kwa ajili ya kukidhi mahitaji unajibana sana hata mtu kufikia kujenga? Ipo siku yao
watu wa serikalini wengi wao wana uwezo mdogo wa kufikiri,kwa kuwa miaka nenda rudi wanafanya kitu kilekile,kuamka mapema,kwenda kazini,kusaini,kazi zilezile ambazo hadi saa 4 zinakua zimeisha,kwa miaka 30 unakua umetengeneza mlemavu wa akili
 
Nafikiri hawa mawaziri na mabosi wao hawajui kinachoendelea huku chini... Nafikiri waziri Lukuvi atafute ndugu yake asiye na ubini wa jina la Lukuvi amtume aende ardhi ajaribu kufuata hizo taratibu na gharama halafu aone majibu yake...
huko tabora eneo la kiloleni zinatakiwa kuvunjwa nyumba zaid ya 1000,wanaambiwa wamevamia eneo l shirika la reli kwa ramani ya mjerumani ilhali ardhi ndiyo waliowagawia viwanja na kodi wanachukua,ikiwa ramani hiyo itafuatwa ni kwamba mji wa tabora utapasuliwa zaidi ya nusu na kuwafanya wenyeji kuwa wageni kwenye mji wao
 
Hii nchi rahisi sana kutengeneza waasi hawa wanasiasa ndio watunga sera na wapanga kila kitu wanaachia kutekeleza mipango miji hadi raia wanajenga tu nao wanachukua kodi na majengo kila mwaka! Baadae mtu anaibuka tu eti wavunjiwe. Hivi hawa mbwa wanajua ni kiasi gani watu wanatafuta pesa kwa ajili ya kukidhi mahitaji unajibana sana hata mtu kufikia kujenga? Ipo siku yao
Mkuu sahihisho hapo tafadhali. Hakuna haja ya kuasi maana uasi wanaokufa kwenye hilo vurugu lake ni maskini wenzio na wale waliokuudhi wanalindwa mbali huko,
Dawa sahihi ni kumdungua unaemtaka na anaestahili mbele za MUNGU kudunguliwa, usitupe maskini wenzio adhabu ya mtu mwingine
Ni kweli kwenye ardhi hapo ni mahala pengine, wanapodhulumu , dah MUNGU anawaona,

Tukisema kuna watu wamelewa madaraka mnasema tumewatukana. Haya, avunje tu kwani hakuna namna. Watu hawataki kuondoka mjini wanawanyima wakuu kuvuta hewa safi. Vunjaaaa, Bomoaaaaa
 
huko tabora eneo la kiloleni zinatakiwa kuvunjwa nyumba zaid ya 1000,wanaambiwa wamevamia eneo l shirika la reli kwa ramani ya mjerumani ilhali ardhi ndiyo waliowagawia viwanja na kodi wanachukua,ikiwa ramani hiyo itafuatwa ni kwamba mji wa tabora utapasuliwa zaidi ya nusu na kuwafanya wenyeji kuwa wageni kwenye mji wao
Nafikiri utakuwa mkwara haitawezekana may be kuna makosa sehemu. Ila nyumba 1000 ni kama kata nzima. Waone huruma huyo mjerumani aliondoka Tanganyika 1919. Naamini serikali yetu sio katili namna hiyo.

I makinikia 17
 
nyumba zimepigwa x tayari,wamepewa notisi ya mwezi,wamefungua kesi mahakamani,nadhani itakua imeanza leo
 
Nadhani anamaanisha nyumba zinazojengwa hivi sasa ndio zizingatie mipango miji. Hawawezi kuvunja squatter zilizopo kwa sababu kisheria ni lazima walipwe fidia kwanza, kitu ambacho kwa sasa ni kigumu.
Kama ninavyodhani ni sahihi basi hata mimi naunga mkono. Makazi holela yanaongezeka kwa kasi zaidi kuliko makazi yaliyopangwa. Hii ni hatari kwa siku zijazo.
Jambo la muhimu upande wa serikali ni kuhakikisha viwanja vinakuwepo sokoni muda wote na sheria zifuatwe ili kuepuka kuuzia viwanja vyote madalali.
Gharama za fidia ni kubwa na wakati meingine ndo huwa zinachelewesha upimaji. Hapa lazima kuwe na maelewano mazuri kati ya serikali na wamiliki wa maeneo. Serikali isifanye miradi ya upimaji kwa faida ili wanaoachia maeneo yao nao wanufaike.
 
huko tabora eneo la kiloleni zinatakiwa kuvunjwa nyumba zaid ya 1000,wanaambiwa wamevamia eneo l shirika la reli kwa ramani ya mjerumani ilhali ardhi ndiyo waliowagawia viwanja na kodi wanachukua,ikiwa ramani hiyo itafuatwa ni kwamba mji wa tabora utapasuliwa zaidi ya nusu na kuwafanya wenyeji kuwa wageni kwenye mji wao
Mimi ndio maana naichukia ccm kuliko shetani wanawavunjia masikini tena msikini kbs mtu hela ya kula hana itakuaje kulipa kodi ya nyumba? Kuba classmate wangu huko kiloleni wana nyumba nne ndani ya mtaa mmoja zote zimewekwa X.. mtu anamkopo kiloleni watu wameishi miaka zaidi ya Sabini Leo unamwambia abomoe!! Huyu lukuvi sifa zitamponza!!
 
bahati mbaya walojenga hizo nyumba washafariki,warithi wao wana umri 60+..na pale kiloleni pamejengwa kimpangilio na viwanja vyote vinalingana,hiyo siyo bahati mbaya bali serikali ilihusika..leo wanataka kubomoa
 
Back
Top Bottom