Angeweza kama angekuwa nje wa mfumo wa kifisadi wa CCM.
Ni kweli tuna vijana wazuri kama kina January Makamba lakini wanaharibiwa na mfumo.
Hivi WAKUU mna matumaini gani na huyu January Makamba? Hivi lini Shetani akazaa Malaika? Huyu ni zao la Kifisadi na atadumu hivyo!!! Si tuliletewa nakala kivuli hapa jamvini ya dada yake kuomba pesa kwenye makampuni ya madini ili ndugu yake atumie kupata ubunge? Mbona mnasahau wkuu? Sasa katika hali hiyo unategemea atapata wapi ujasiri wa kuwatetea WaTanganyika mbele ya waliyo mwezesha kupata ubunge? Yeye atakuwa mtumwa wao milele.
Tumefika hapa tulipo, na tutaendelea kuumizwa na wanao itwa wawekezaji hadi pale tutakapo amka na kujua haki zetu. Tufike mahala tukatae kunyonywa na hao wanao itwa WAKWAPUAJI. Tuna viongozi wasio na uwezo. Wamepewa uongozi kama fadhila, hivyo wanaogopa kupingana na masilahi ya walio weka madarakani.
Hakuna cha mfumo wala nini. Kilichopo mbele yetu ni Uongozi wa maslahi binafsi. Mbona kina Mwakyembe wanachanja mbuga ki ukweli, si wapo kwenye mfumo wa CCM?
Tuamke waDanganyika saa ya ukombozi ni sasa, na tuache kulalama bila kuchukua hatua.
Mimi sio kwamba sina uwezo wa ku-join DsTv (ninao). Lakini kwa kutambua unyonyaji huu, nimeamua kuwa mmoja kaiti ya walio amua kukataa unyonyaji wa hali ya juu wa aina hii: Amua sasa na ikatae DsTv kama una uchungu na pesa yako. Vinginevyo endelea kuliwa.
Tatizo haliko DSTV bali channel zenyewe zinatakiwa. Zijiorodheshe na kulipa hakuna dezo
Hapa ujue wakionekana dstv ni kuwa watu wengi zaidi wataona hizi tv so matangazo yao pia
So walipe wataonekana
TV za kenya zote K24 , citizen , ntv . Kbc , nk zipo ndani ya dstv
Hivo ndio ukweli
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
DSTV wahusika sana, imagine now nipo kwenye TV yangu naangalia Kombe la klabu bingwa duniani. Isingekuwepo ningeangalia wapi? Hayo ya cost nayawaza baadaye sana, cha muhimu nipate service ya uhakika na kwa wakati ninaoihitaji.
Wataachaje kuhalalisha wizi kama huu wakati wenyewe wanaiba kwenye madini na ufisadi uliokubuhu serikalini. Jakaya kikwete na serikali ya Chama Cha Majambazi ni janga la kitaifa.
TBC inapatikana Channel Number ngapi kwenye DSTV?
Ndugu wanabodi nashangazwa
sana kwa msimamo wa kampuni ya Multichoice ambayo inatoa huduma ya
kuonyesha chanel za TV za digitali nchini kwa kupitia DSTV.
Kampuni hii haijaonyesha nia au tuseme imekataa kuweka chanel za kitaifa
za hapa nyumbani ambazo ndizo zinatupa habari za hapa nyumbani.
Nashangazwa sana na msimamo huu pamoja na ukimya wa serikali hasa
kupitia TCRA na wizara husika ambao ndio wanapaswa kulinda maslahi ya
wananchi wake.
Inavyoelekea baadhi ya viongozi wa serikali wana maslahi binafsi kwenye
kampuni hii. Iweje kampuni zingine kama Star time na Zuku waweze
kuingiza chanel zetu za kitaifa kama ITV na Star Tv kwenye bundle zao
lakini DSTV wakatae? Hakuna mantiki yoyote ya kutoziingiza hizi chanel
kwani ni chanel ambazo si za kulipia.
Hii ina maana watu tulio na DSTV baada ya tarehe 31 mwezi huu hatutaweza
kuona chanel zetu labda kama utanunua king'amuzi kingine ambacho nacho
uwe unakilipia. Na kama TV yako haiwezi kuchukua ving'amuzi viwili basi
itakubidi ununue TV nyingine! Au uondoe deki nk
Pia ingawa hawa jamaa wanatoa huduma kibiashara lakini bei zao ni kubwa
mno tofauti hata ukiwa huko kwao SA na hata huwezi ukalinganisha na watu
wanavyotozwa huko ulaya au marekani ambako wao ndio wenye kipato
kikubwa. Huduma za TV ni chanzo cha taarifa na elimu (information &
education) kwa karne hii kama ilivyo simu za mkononi si anasa tena Bali
ni huduma muhimu kwa wananchi.
Pamoja na kwamba hawa Multichoice wana miaka 15 wakitoa hii huduma ya
DSTV na sasa hivi wana wateja wengi ambapo ingewezekana kupunguza bei
kwa kiwango kikubwa lakini bei zao zimebaki kuwa za kiwizi. Sasa hivi
wanatudanganya kwa kupunguza asilimia 10!
Pamoja na kwamba kujiunga na DSTV ni hiari kama ilivyo kujiunga na
makampuni ya simu za mkononi hii haihalalishi wizi kwa mteja na kichwa
ngumu kukataa kuingiza TV zetu za kitaifa za kitanzania na serikali yetu
ikiwaangalia na kuendelea kutoza gharama ya wastani wa 120,000 kwa
mwezi ambayo ni sawa na elfu 4 kwa siku!
Kama huna uwezo acha kutumiaDSTV. nenda zuku ama startimes na agape
Dstv kama kampuni inataka sana kuweka local channels ila kuna disagreement fulani ambazo nadhani watakubaliana tu sooner or later.
Kitu chochote kisichokuwa na mpinzani ni tatizo. Kufa kwa GTV ilikuwa pigo sana. Bei wanazotoza hawa jamaa ni biashara kichaa kabisa. Dawa yake na hivi ving"amuzi vianze kuonyesha michezo mbalimbali ikiwemo ligi kubwa duniani na wasibaniwe na wakubwa maana wakubwa wanapewa matangazo ya DSTV bure
Wakuu ni sikum10 tu zimebaki serikali kuzima mitambo ya analogy na si serikali wala Multichoice wametangaza hatma ya subscriber wa DSTV kama wataweza kuendelea kuangallia TV za kitaifa zinazoonekana bila maliponau la.