Mazindu Msambule
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 7,508
- 6,892
Sawa kabisa Mkuu, ila haionekani kama wana nia hiyo Na TCRA inaonekana kwa DSTV hawana meno
Mkuu, kwani biashara si ni huria, TCRA wafanye nini while DSTV wanapata wateja? kama kungekua hakuna alternative then TCRA wangelaumika hapa, kama vipi we toka tu mwenyewe na jiunge na wengine, isije ikawa wengine wapo DSTV kwasababu ya kuosha jina mtaani kwamba wanamiliki TV za bei mbaya, hawa ndio ambao TCRA waki implement hizo sheria mnazo taka watakuja na kupiga kelele, mi nashauri, we HAMIA TU Airtel basi!
sasa na mimi nisiyekuwa na DSTV wala Zuku na hivyo vin'gamuzi vingine....just moved house and I'm kind of thinking to buy one of them ...my question is..Will I be able to view DSTV channels without having the so called ungo or i have to negotiate on their terms and conditions? I'm finding it a bit hard to understand how it is going to work...another thing is...why do they charge people into foreign currency rather than local currency..Jamani serekali hawalioni hilo? sio wao tu though ..kuna maduka kibao mjini wanacharge kwa dollar. However, i'm not real blaming them...it is simply our fault.
Hiyo ni kampuni ya hamy mpungwe na mkapa kelele zetu ni bure kabisa
Kwa maana ya ubora na value bado hao star-times and etal bado wananjunga na wako kichina/asia zaidi. Ila DSTV wanapackage tofauti manake ukitaka super sports lazima utalipa zaidi mazee na lazima ufanye uchaguzi sahihi unaweza pata hiyo huduma bar kwa bei poa usiforce sana.
Starehe siku zote inagharama ukitaka kula lazima uliwe.
Ndugu wanabodi nashangazwa sana kwa msimamo wa kampuni ya Multichoice ambayo inatoa huduma ya kuonyesha chanel za TV za digitali nchini kwa kupitia DSTV.
Kampuni hii haijaonyesha nia au tuseme imekataa kuweka chanel za kitaifa za hapa nyumbani ambazo ndizo zinatupa habari za hapa nyumbani.
Nashangazwa sana na msimamo huu pamoja na ukimya wa serikali hasa kupitia TCRA na wizara husika ambao ndio wanapaswa kulinda maslahi ya wananchi wake.
Inavyoelekea baadhi ya viongozi wa serikali wana maslahi binafsi kwenye kampuni hii. Iweje kampuni zingine kama Star time na Zuku waweze kuingiza chanel zetu za kitaifa kama ITV na Star Tv kwenye bundle zao lakini DSTV wakatae? Hakuna mantiki yoyote ya kutoziingiza hizi chanel kwani ni chanel ambazo si za kulipia.
Hii ina maana watu tulio na DSTV baada ya tarehe 31 mwezi huu hatutaweza kuona chanel zetu labda kama utanunua king'amuzi kingine ambacho nacho uwe unakilipia. Na kama TV yako haiwezi kuchukua ving'amuzi viwili basi itakubidi ununue TV nyingine! Au uondoe deki nk
Pia ingawa hawa jamaa wanatoa huduma kibiashara lakini bei zao ni kubwa mno tofauti hata ukiwa huko kwao SA na hata huwezi ukalinganisha na watu wanavyotozwa huko ulaya au marekani ambako wao ndio wenye kipato kikubwa. Huduma za TV ni chanzo cha taarifa na elimu (information & education) kwa karne hii kama ilivyo simu za mkononi si anasa tena Bali ni huduma muhimu kwa wananchi.
Pamoja na kwamba hawa Multichoice wana miaka 15 wakitoa hii huduma ya DSTV na sasa hivi wana wateja wengi ambapo ingewezekana kupunguza bei kwa kiwango kikubwa lakini bei zao zimebaki kuwa za kiwizi. Sasa hivi wanatudanganya kwa kupunguza asilimia 10!
Pamoja na kwamba kujiunga na DSTV ni hiari kama ilivyo kujiunga na makampuni ya simu za mkononi hii haihalalishi wizi kwa mteja na kichwa ngumu kukataa kuingiza TV zetu za kitaifa za kitanzania na serikali yetu ikiwaangalia na kuendelea kutoza gharama ya wastani wa 120,000 kwa mwezi ambayo ni sawa na elfu 4 kwa siku!
Mkuu, nakushauri achana nao if your less satisfied with their service.
120,000 * 12 = 1,440,000/=
STAREHE GHARAMA.
TBC ipo inapatikana.
majambazi hao mi nipo startimes namwemwelekaaaaa
TBC inapatikana Channel Number ngapi kwenye DSTV?
Wakuu ni kweli kwamba Dstv ni expensive( ila ni kwa anayetaka na si lazima) ila hivi tatizo ni Dstv au mamlaka za nchi hii? Hapa bongo gharama za cmu ni kubwa sana na bado hayo makampun ya cmu yanachangia kiduchu kwenye pato la taifa, the same goes to sekta ya madini, bandari na takataka nyingine za kutosha.
Tujiulize,hivi ni kwa nini nchi zisizo na bandari(land locked countries kama Zambia,Rwanda,Uganda) na nyingine zinatumia bandari yetu kwa kiasi kikubwa kupitishia bidhaa zake (kama Zambia) zinakua na bei nafuu katika hizo bidhaa kuliko hapa zilikopitia?
Hivi tatizo ni Dstv au mamlaka zetu? Kama huko kwingine mnakosema (kama South Africa) kwamba Dstv ni affordable kuliko hapa then tatizo si Dstv ila ni mamlaka zetu.
Personally, Dstv wako poa sana hata customer servise yao ni bomba probably kuliko makampun mengi yaliyopo bongo na hii PVR decoder ni noma mazee, inaipa uhai TV!