Serikali imetutendea ukatili kuwabeba Matajiri

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
"Tafadhali chukua tu hivi vitunguu nahitaji pesa kwa ajili ya mafuta ya taa, keshokutwa ukipita hapa utanilipa hiyio pesa".

Ni kauli ya Mama wa Kijiji cha Kilombero, kilometya chache kutoka Kasulu Mjini mwaka 2008 wakati nikipita kuelekea Kigioma Mjini. Mama huyo, akiongea kwa lugha ya Kiha alijaribu kuniomba ninunue vitunguu alivyokuwa akiuza barabarani na wenziwe. Mimi na wenzangu hatukuwa tunahitaji kununua vitunguu ila mazao mengine.

Kauli ya mama huyo imenijia tena mwaka huu baada ya Serikali kuamua kupandisha kodi ya mafuta ya taa ili kupambana na uchakachuaji! Nimewafikiria ndugu zangu wa Vijijinini: Kasuku, Iyengamurilo, Kisumwa, Nanguruwe nk.

Yaani Serikali imeamua kuwasaliti wananchi wake wengi (asilimia 70) wanaoishi vijijini ili kuwapendezesha wafanyabiashara wasafirishaji Mafuta na sisi wenye kumiliki magari kwa hasara ya Watanzania walio wengi.

Uamuzi huu ambao umefanya bei ya Mafuta ya taa kuwa kubwa kuliko dizeli na petroli na kuwaumiza watumiaji mafuta ya taa na kutishia zaidi uhai wa misitu kwangu umenifanya nijiulize kuwa je; nchi hii ni ya Matajiri na wafanyabiashara tu? Wao wakikohoa na kulia Serikali inasikia kilio chao haraka; lakini Wakulima na Wanavijiji wanalia machozi ya damu, serikali haisikii wala haioni.

HUU NI UKATILI WA HALI YA JUU
 
hayo ndiyo majibu rahisi ya serikali yetu,eti ya kumaliza tatizo la uchakachuaji wa mafuta!
 
Back
Top Bottom