Serikali imetoa Picha rasmi ya Rais Dr. Magufuli

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
DSC_0001.jpg


Picha Rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli itaanza kuuzwa Januari 08, 2015, katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) Mtaa wa Samora.

Kila nakala ya picha hiyo itauzwa shilingi Elfu Kumi na Tano tu bila fremu. Picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere itauzwa shilingi Elfu Tano tu. Aidha, Picha hizo zitauzwa katika Ofisi za Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).

Picha hizo zinatakiwa kutundikwa katika ofisi zote za Serikali, Taasisi za Umma, Mashirika na Ofisi binafsi. Kila ofisi inatakiwa iwe na picha ya Mhe. Rais pamoja na Baba wa Taifa.

Serikali inatoa onyo kwa wale wote wanaosambaza picha isiyo rasmi pamoja na Serikali kutoa taarifa kusitisha matumizi ya picha hiyo na wanaotengeneza picha ukubwa ambao siyo rasmi.

Hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Idara ya Habari(MAELEZO) ndio yenye Haki miliki ya picha hiyo.
 
Mbona ni mbaya kuliko ile ya kwanza?
Anafanana na hayati Laurent Kabila!
 
K
Wamekosea hapo kwenye ramani ya africa imepinda sana..
wanza kwa nini aweke ramani ya Africa???? Mie naona angevaa ramani ya Tanzania au ile beji yenye rangi za bendera ya Tanzania. Poor him hashauriki ndio tatizo labda.
 
naomba kuuliza hivi hata katika zile OFISI zote za Lowassa na yeye pia ATAZIWEKA au? manake nimesikia kuwa kuwekwa kwa hizo picha za Marais waliopo MADARAKANI ni LAZIMA na siyo HIARI. kuna mtu nina UHAKIKA hizo picha ZITAMUUMIZA mno na si ajabu kila akiwa anaiona tu basi anamwita Daktari wake aje amtibu.
 
Last edited by a moderator:
Kuna mmoja waliwahi kubadili picha yake walisema ilipigwa wakati wa msongo wa mawazo ya kampen, nilijiuliza ina impact gani kwa jamii sikupata jibu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom