Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
SERIKALI imetoa namba ya simu bure itakayotumika kutoa ripoti ya wahujumu wa sukari, namba hiyo ni 0754 38 79 28, ambayo* itakuwa wazi kupokea taarifa za walanguzi wa sukari.Pia imeahidi kutoa zawadi nono kwa mtu* ye yote atakayetoa taarifa za kufanikisha kukamatwa kwa* mtu au watu wanaovusha sukari nje ya nchi na kuwaacha wananchi wakisumbuka.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri* wa Kilimo Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe alipofanya ziara ya kushtukiza katika Jiji la Dar es Salaam kukagua na kuona hali na mwenendo wa sukari jana.
Ziara hiyo aliifanya wilayani Temeke katika soko la Kipati Mbangala na la Temeke Sterio na kutangaza vita na wahujumu wa sukari wanaovusha nje ya nchi na kwamba lengo la kutoa namba hiyo ni kutaka ushirikiano kwa wananchiTaarifa iliyotolewa na wizara hiyo jana jioni ilisema Waziri Maghembe alijionea hali ya sukari ambapo aliweza kutembelea maduka zaidi ya 10 ya rejareja na jumla, ambapo alibaini bei tofauti ya sukari kutoka duka moja hadi lingine.
Bei ya rejareja ilikuwa kilo moja iliuzwa kuanzia Sh1,900 hadi 2,200 na bei ya jumla katika mfuko mmoja ilikuwa inauzwa kutoka Sh95,000 hadi 105,000 kwa mfuko wa kilo 50.
Pia Waziri alishuhudia baadhi ya wafanyabiashara kutokuwa wawazi na kukosa uaminifu, ambapo katika Soko la Kipati Mbagala mfanyabiashara wa jumla aliweza kumdanganya Waziri kuwa hana sukari, lakini baada ya kuingia katika stoo yake Waziri aliweza kubaini kufichwa kwa mifuko mitatu ya kilo 50 kila mmoja, ikiwa imefunikwa na vitu vingine.
Waziri Maghembe hakuishia hapo alikwenda* katika ofisi za kampuni ya kuzalisha Sukari ya Kilombero eneo la Kamata kubaini ukweli wa tatizo la sukari liko wapi.Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya Kilombero, Bashir Haruni alimwambia kuwa kiwanda chake kinaendelea na uzalishaji wake kama kawaida na kwa siku wanazalisha tani 500.
Alimhahakishia Waziri Mghembe kuwa, hakuna tatizo lolote, ila tatizo liko kwa wafanyabiashara wa kati na wala si* kiwanda chake kwani hakihusiki kabisa na uhaba huo wa sukari hapa nchini.Haruni alimwambia Waziri kuwa kila mkoa una mawakala na wote wanauziwa sukari kwa* kupewa mgao wao kama ilivyo ada.
Haruni aliahidi kuipa Serikali ushirikiano wa hali ya juu katika kukabiliana na hali hii na pia kutoa taarifa za hali ya uzalishaji wa sukari na usambazaji wake.Waziri hakuishia hapo alikwenda duka la Shoprite ambalo ni Super Market kuangalia bei ya sukari ili kujiridhisha na hali halisi ya bei zake na aliridhishwa na hali ya uwapo wa sukari na bei zake.
Hatuoni sababu kwa nini Watanzania katika dunia ya sasa wapange foleni kununua sukari wakati viwanda vyetu vinazalisha kama kawaida, alisema Waziri Maghembe.Katika kukabiliana na hali hii ya* sitofahamu ya zengwe la sukari hapa nchini, waziri aliwaomba Watanzania** kutoa ushirikiano kwa Serikali ili kukomesha hali ya magendo ya sukari kwa wanaopeleka nchi ya nje, kuwafichua wote wanaohusika.
Ziara hii ya Waziri* Maghembe imekuja siku moja baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa ziarani mkoani Mara, kutoa mwito wa kuwasaka wahujumu wa sukari hapa nchini hadi kwenye bohari zao kuona kama kweli hakuna sukari* au wanaficha.