SERIKALI imetoa namba ya simu bure itakayotumika kutoa ripoti ya wahujumu wa sukari,

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
SERIKALI imetoa namba ya simu bure itakayotumika kutoa ripoti ya wahujumu wa sukari, namba hiyo ni 0754 38 79 28, ambayo* itakuwa wazi kupokea taarifa za walanguzi wa sukari.Pia imeahidi kutoa zawadi nono kwa mtu* ye yote atakayetoa taarifa za kufanikisha kukamatwa kwa* mtu au watu wanaovusha sukari nje ya nchi na kuwaacha wananchi wakisumbuka.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri* wa Kilimo Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe alipofanya ziara ya kushtukiza katika Jiji la Dar es Salaam kukagua na kuona hali na mwenendo wa sukari jana.

Ziara hiyo aliifanya wilayani Temeke katika soko la Kipati Mbangala na la Temeke Sterio na kutangaza vita na wahujumu wa sukari wanaovusha nje ya nchi na kwamba lengo la kutoa namba hiyo ni kutaka ushirikiano kwa wananchiTaarifa iliyotolewa na wizara hiyo jana jioni ilisema Waziri Maghembe alijionea hali ya sukari ambapo aliweza kutembelea maduka zaidi ya 10 ya rejareja na jumla, ambapo alibaini bei tofauti ya sukari kutoka duka moja hadi lingine.

Bei ya rejareja ilikuwa kilo moja iliuzwa kuanzia Sh1,900 hadi 2,200 na bei ya jumla katika mfuko mmoja ilikuwa inauzwa kutoka Sh95,000 hadi 105,000 kwa mfuko wa kilo 50.

Pia Waziri alishuhudia baadhi ya wafanyabiashara kutokuwa wawazi na kukosa uaminifu, ambapo katika Soko la Kipati Mbagala mfanyabiashara wa jumla aliweza kumdanganya Waziri kuwa hana sukari, lakini baada ya kuingia katika ‘stoo’ yake Waziri aliweza kubaini kufichwa kwa mifuko mitatu ya kilo 50 kila mmoja, ikiwa imefunikwa na vitu vingine.

Waziri Maghembe hakuishia hapo alikwenda* katika ofisi za kampuni ya kuzalisha Sukari ya Kilombero eneo la Kamata kubaini ukweli wa tatizo la sukari liko wapi.Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya Kilombero, Bashir Haruni alimwambia kuwa kiwanda chake kinaendelea na uzalishaji wake kama kawaida na kwa siku wanazalisha tani 500.

Alimhahakishia Waziri Mghembe kuwa, hakuna tatizo lolote, ila tatizo liko kwa wafanyabiashara wa kati na wala si* kiwanda chake kwani hakihusiki kabisa na uhaba huo wa sukari hapa nchini.Haruni alimwambia Waziri kuwa kila mkoa una mawakala na wote wanauziwa sukari kwa* kupewa mgao wao kama ilivyo ada.

Haruni aliahidi kuipa Serikali ushirikiano wa hali ya juu katika kukabiliana na hali hii na pia kutoa taarifa za hali ya uzalishaji wa sukari na usambazaji wake.Waziri hakuishia hapo alikwenda duka la Shoprite ambalo ni Super Market kuangalia bei ya sukari ili kujiridhisha na hali halisi ya bei zake na aliridhishwa na hali ya uwapo wa sukari na bei zake.

“Hatuoni sababu kwa nini Watanzania katika dunia ya sasa wapange foleni kununua sukari wakati viwanda vyetu vinazalisha kama kawaida,” alisema Waziri Maghembe.Katika kukabiliana na hali hii ya* sitofahamu ya zengwe la sukari hapa nchini, waziri aliwaomba Watanzania** kutoa ushirikiano kwa Serikali ili kukomesha hali ya magendo ya sukari kwa wanaopeleka nchi ya nje, kuwafichua wote wanaohusika.

Ziara hii ya Waziri* Maghembe imekuja siku moja baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa ziarani mkoani Mara, kutoa mwito wa kuwasaka wahujumu wa sukari hapa nchini hadi kwenye bohari zao kuona kama kweli hakuna sukari* au wanaficha.
 
Wasituzingue washushe bei ya vyakula ili kupunguza ukali wa maisha wanaoathiriwa ni huko vijijini wangapi wana simu? Wangegawa simu na kuwatilia vocha pia.
 
112 imewashinda hiyo ya kuriporti sukari wataweza kuimantain?
Kwanza hiyo simu itaongeza tu matukio ya rushwa, polisi wetu wenyewe njaa kali na wanahongeka kirahisi
 
Hii nayo ni siasa aina ya mchezo wa kombolela. Unamwambia mwenzio fumba macho ili ukajifiche kisha unamwambia njoo unitafute. Serikali inafahamu kuwa tatizo la uhaba wa sukari linaanzia kwenye mikataba baina yake na wazalishaji. Inafahamu fika kuwaruhusu/kuwalazimisha wazalishaji kuuza asilimia 80 nje ili kupata fedha za kigeni. Na inafahamu kuwa sukari nyeupe yote inayozalishwa ndani hakuna hata kilo moja inayouzwa Tanzania. Yote inaenda nje. Waziri naye anafahamu fika kuwa iko sukari inayoingia kwa magendo mikoa ya kusini toka Malawi na inauzwa kwa bei chee sana na kuvuluga cartel ya wazalishaji magamba na serikali imejiunga na cartel kuhakikisha sukari ya bei nafuu haiingii Tanzania. Katika haya machache tu unaweza kupata sura halisi ya usanii wa akina Maghembe.
 
So ridiculous. I can go without sugar for years, but i can not go without sembe, rice, maharagwe, mafuta ya kupikia etc. Huwezi kufanya ziara Dar na kukonkludi kuwa hali ya Dar ndio ya Tanzania nzima. Kama kuna uzemebe waadhibiwe wazembe na sio wafanya biashara wadogo wanaoganga njaa, juu ndio kumejaa wasiowaaminifu, sio chini.
 
Eti wawawajibishe ili wajiharibie ama? Wangapi waliolitia hasara taifa wamewashitaki?
 
Hongera serikali yetu kwa kuliona hilo. Jana nilifarijika sana baada ya kuona ziara ya kushtukiza ya Maghembe, nikasema yes
 
Hapa Moshi kaimu Mkuu wa Mkoa aliyesitaafu aliwaita TPC wajieleze kulikoni sukari hakuna madukani.....alishangaa kuambiwa uzalishaji ni kama kawaida na bei ya kiwandani ni shs 72000. Mchezo uko kwa mawakala
 
Pinda hatumii akili, turipoti nini wakati bei ya sukari mtaani sh 2500.ingekua lowasa ungekuta kishatembelea viwanda na mawakala wa sukari kujua supply chain ikoje tatizo lipo wapi?pinda aulize kilombero na mtibwa white sugar inapotelea wapi?maana walala hoi tunapewa brown sugar tuu
 
Na hii ya mahindi yanayoenda kenya kwa kusindikizwa na police wanachukua uamuzi gani?
 
Back
Top Bottom