Serikali imetenga mil. 100 kwa mtu yeyote atakayefichua mtu aliyerusha bomu Arusha.

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,986
32,396
Wanaukumbi.

Serikali imetenga kiasi cha sh milioni 100 kwa mtu yeyote atakayefichua mtu aliyerusha bomu kwenye mkutano wa kampeni Soweto Arusha.

Serikali imesema itatumia vyombo dola kuakikisha inawatia mikononi wale wote waliohusika na tukio hilo.

SOURCE: BUNGENI.
 
Wameshindwa kuwatafuta waliowatesa kina Ulimboka, Kibanda, Kubenea.
Wameshindwa kuwatafuta wahusika wa bomu la kienyeji la Olasit (Victor Ambrose ni kiini macho).
Wameshindwa kumuweka ndani ya kizimba mlipuaji wa mwandishi na Mtanzania Davidi Mwangosi.
Je, hili mnategemea mtaliweza kwa hizo TSHs milioni 100??
La hasha hakika la hasha...achaneni kwanza na Siasa za Illuminati
 
wenyewe ndo wahusika wakuu hapo kuna mchezo wanaanza kukifanya dr.ulimboka alimkamata huyu chizi wa kenya olasti wameunda tume mpaka leo hakuna majibu serikal dhaifu pongezi
 
Kipande hiki cha Wilfred Lwakatare: Mrejesho kutoka mahabusu Segerea kinaujumbe unaomuhitaji kila Mtanzania kuusoma, kuutafakari kwa umakini na kuuelewa. Kama tunachokikosi maalumu, kilichosomeshwa kwa ghalama kubwa na kupewa vitendea kazi vya ghalama, iweje leo tena tunaanza kuomba waalifu ndiyo watajane kwa kuwawekea dau? Soma mwenyewe!



Wauaji wa Mwandishi wa Habari -Mwangosi??????


Muuaji wa Padre Ambrose????



Waliomwagia Shehe Tindikali????


Aliyerusha bomu kwenye uzinduzi wa Kanisa Arusha??????



Na huyu naye badala Dola ishughulike kuwatia nguvuni waliomdhuru, chama kimeamua kumfanya mwanasesele na mtaji wa Kisiasa!


Waliomjeruhi Kibanda????


Waliomdhuru Kubenea miaka kadhaa iliyopita wamewahi kukamatwa???


Je waliomteka na kumtesa Dr. Ulimboka nao bado wanatafutwa????


Ritz kwa ufupi tuipende nchi yetu. Tuwe wakweli kwa nafsi zetu na wazalendo kwa nchi yetu. Adui HAYUPO nje ya mwenye mamlaka na anayetangaza dau la kumtafuta. Na kujikamamwenyewe hawezi!
 
Last edited by a moderator:

Sasa serikali inatumia nini kati ya hivyo viwili PESA na VYOMBO VYA DOLA? Since when has our government got itself in bounty business....I wonder :shock::shock::shock:
 
kuna waliomwua padre Mushi kule Zanzbar na waliomjeruhi Padre Mkenda. Pamoja na hayo Haiwezekani kuwa Ulimboka alitekwa na kuteswa na mtu mmoja tu, mimi naishauri serikali imwachie huru huyo chizi kwani wanatumia gharama nyingi kumlinda wakati hahusiki wala hajui lolote.
 
Serikali dhaifu hata ikiapa mara mia kuwa itawatia mikononi wahalifu kamwe haitaweza na wala hatuwezi kuamini hivyo kwa kuwa ya soweto hayakuwa ya kwanza. Yametokea mengi na watz mashaidi na waliapa hivyo lakini mpaka kesho hakuna waliomkamata hata mmoja. Serilkali hii inaweza kutengeneza video feki na kuunda tume kwa maslahi ya kisiasa lakini si kukamata wahalifu.
 
Good motivation, sasa wale askari waliomukoa mlipuaji wajitokeze walambe hii bingo
 
Isije ikawa hiyo hela tayari inafahamika nani ataichukua na mgawanyo tayari ushaeleweka.
 
mimi nafikiri hiyo hera apewe rpc wa arusha na huo ulinzi kama atakuwa jasiri kuwasinitch wanzake na amini anajua tumpe ujasiri na kumwembea kwa Mungu kwa maamuzi magumu atakayofanya la sivyo ni kutwanga maji kwenye kinu
 
Kinachonichekesha umeleta hii thread huku ukimjuwa fika muhusika wa mauwaji haya ni nani, si lazima kumpata aliyerusha bomu lakini cha umuhimu who is behind this?

Hiyo millioni 100 imeshaliwa tayari hapa Serikali ya majambazi inataka kuhalalisha wizi wao wapuuzi kabisa hawa.
 
si IGP keshaunda kikosikazi wanacho kiamini? bwana.chagonja nadhani, hivi huyu si ndie aliye chunguza na kutoa report kuwa wafuasi wa CHADEMA ndio walimuuwa Mwangosi? Yaelekea ni mtaalamu kwelikweli na atakuja na majibu ya kupendeza kama kawaida yake. Hivi habari kuwa risasi zimeokotwa ni kweli?? sijaona hilo likiongelewa saana!
 
Wampe Mwigulu tu zote, wanahangaika kuuzunguka mbuyu?

 
Huu ni uhuni na upumbavu kama ushenzi uliotokea kwa kina Kibanda,Mwangosi,ulimboka na wakina Rage Kyle Dodoma walifanya uharamia na hawakuguswa, waanze na Guu la Chemba!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…