Serikali imesitisha ajira eti haina pesa

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Stress... Mfukon sina mkwanja! Wananiambia nijiajiri,wananiambia mimi sio mbunifu,lakini cha kushangaza wao wameajiriwa,na wapo tayari hata kulisha watu vinyonga ngozi zibanduke ili waendelee kukaa kwenye ajira zao,wakifukuzwa leo wanapata presha baada ya mwaka wanakufa,wameajiriwa miaka 30 iliyopta na bado wanaogopa kujiajiri leo! Mie je? PROPAGANDA,Miaka 50 ya uhuru,serikali imesitisha ajira eti haina pesa.
 
Waambie ndugu mana naona maandalizi yamiaka yao hamsini wanayapeleka kwakasi kwelikweli !! Alafu wanadai hela hawana!!
 
Hii ndio Tanzania zaidi ya uijuavyo, sherehe za miaka 50 ya uhuru kwa kila wizara na taasisi zake zinafanyika, vijana wansota mtaani....
 
zito mwongo, serikali ina hela kama mwarabu.
source: mustafa mkulo
 
Haaaaaa Arab Money lol wameanza kusherekea miaka 50 ya uhuru tangia january du si mchezo bwana TZ ina hela wewe si umeona wamekopa bank za ndani kulipa mishahara haaaaaa bado tu kuuza makameroon tupate msaadaaaA
 
duu tunaosubiri hazina itoe ajira tulie tu ila wanapesa ya kusheherekea miaka 50 ya uhuru na kuwakarimu wageni
 
kama kawaida, porojo nyingi kuliko vitendo. Kiukweli mazingira ya kujiajiri bongo ni mfu sana. Ishu kubwa hapa ni mitaji.
 
Kwa sistimu ya mashines za TRA tulijua tu haitafika mbali. 1. kutumia huduma za mteja wao mkuu Vodacom. 2. Kuanzisha kitu ambacho hujawaandaa wadau vilivyo. 3. Kucheza na urafiki wa wafanya biashara. Hasa ktk suala la umeme toka enzi za awamu ya 3 kwa kuogopa kushindwa uchaguzi. 4. Hatuna viwanda.

Sasa kama wao wanashindwa kuajiri nani ataajiri?
 
duu tunaosubiri hazina itoe ajira tulie tu ila wanapesa ya kusheherekea miaka 50 ya uhuru na kuwakarimu wageni

Hii ni aibu sana kualika mgeni Prince eti kuja kusherehekea nanyi! Matangazo ya mawizara kwa kukata maungo ndani ya malori mitaani inatuonyesha upungufu mkubwa wa fikira. Matangazo haya yapelekwe vijijini sisi tunajua tayari
 
Hayo ndiyo mafanikio ya magamba wanayotaka tusiyabeze. Wee ndugu vipi huyaoni hayo "mafanikio"?

Back
Top Bottom